Sunday, July 26, 2015

Mtoto wa Whitney Houston Afariiki Dunia! Alikuwa na mialka 22 tu!

 Wadau, kuna habari ya kusiktisha leo.  Bobbi Kristina Brown (22) amefariki dunia leo.  Alikuwa mahututi tangu mwezi wa kwanza (Januari) alipokutwa amezama kwenye maji bafuni kwake.  Ajabu Bobbi Kristina ndiye aligundua maiti ya mama yake ikiwa imezama kwenye maji bafuni miaka mitanao iliyopita.  Kuna wanaodai mpenzi wake, Nick Gordon, kafanya njama amwue ili apate pesa zake.  Polisi bado wanafanyafanya uchunguzi.  

Mwenyezi mungu ailaze roho ya Bobbi Kristina ahala pema mbinguni. Amen. Pole sana Bobby Brown.

http://uptownmagazine.com/files/2012/11/Bobbi-Kristina.jpg
The Late Bobbi Kristina Brown (1993-2015)

_________________________________________

Kutoka: ET Online


Bobbi Kristina Brown, the daughter of late music legend Whitney Houston and R&B singer Bobby Brown, died on July 26, surrounded by her family, at Peachtree Christian Hospice in Duluth, Georgia. She was 22.
"She is finally at peace in the arms of God," the Houston family said in statement to ET. "We want to again thank everyone for their tremendous amount of love and support during these last few months."
On Jan. 31, Bobbi Kristina was found unresponsive in her bathtub and was then taken to North Fulton Hospital in Roswell, Georgia, where she was put on a ventilator to assist her breathing. She was later placed in a medically induced coma at Atlanta's Emory University Hospital.

VIDEO: Whitney Houston & Bobbi Kristina Brown: A Circle of Tragedy
Nearly two months later. she was moved to a rehabilitation center, where she remained until June 24, when she was moved to the hospice center.

Kwa habari kamili BOFYA HAPA:

Saturday, July 25, 2015

Sherehe za Arobaini ya marehemu Baba Yangu Dr. Aleck Che-Mponda Yafanyika Dar Leo!

Wadau, leo sherehe za Arobaini ya marehemu baba yangu mzazi, Dr. Aleck. H. Che-Mponda, zilifanyika mjini Dar es Salaam, pale nyumbani Tenki Bovu, Mbezi Beach Juu. Nafurahi mwanangu, Camara aliweza kuhdhuria pamoja na mdogo wangu Jessica.

REST IN ETERNAL PEACE DR. ALECK H. CHE-MPONDA (1935-2015)

Mapadre wa Anglikana waliosimamia Misa
Wapwa wa Marehemu
Father Haule wa Kanisa Anglikana Kawe akiongea

Ndugu wa Marehemu



Ndugu wa Marehemi


Nabii Fidel Castro

Wadau, Kumbe Rais Fidel Castro wa Cuba ni Nabii. Mwaka 1973 alitabiri kuwa Marekani itazungumza na serikali ya  komunisti Cuba wakipata Rais mweusi na Papa anatoka nchi za Marekani ya kusini. Ona Raisi wa Marekani ni mweusi, Papa anatoka Argentina!  Sasa kuna Ubalozi wa Cuba Washington D.C. na US wanatuma Balozi Cuba! Duh! Vita Baridi imekweisha sasa.


Friday, July 24, 2015

Ubaguzi Marekani - Kifo cha Sandra Bland

Wadau, marehemu Sandra Bland (28) alikamatwa na polisi mbaguzi huko Texas na kufungwa jela. Dhamana yake ilikuwa dola $5,000.  Kosa lake eti ilikuwa kutokutumia indicator akiwa anaendesha yake. Alikuwa anampisha polisi apite.  Polisi anadai kuwa alimpiga teke. Polisi wamekata hiyo video waliopiga la tukio na hakuna aliyona polisi akipigwa teke.  Waongo!  Sasaa wanadai kajiua.

Sasa, huyo Dylan aliua watu weusi 9 waliokuwa wanasali kanisani. Alikamatwa na kuvalisha vest ya kuzuia risasi na kupewa chakula cha Take Out!  Alikamatwa kwa adhabu kabisa!!!! Yaani nchi hii!

Saturday, July 18, 2015

Mwimbaji Banza Stone Afariki Dunia

The Late Ramadhani Masanja aka Banza Stone
Mwimbaji maarufu Banza, Stone (42). amefariki dunia leo hii nyumbani kwake Sinza, mjini Dar es Salaam.  Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahala pema poponi. Amen.



Kutoka THE CITIZEN


Dar es Salaam. Veteran dance musician Ramadhan Masanja aka Banza Stone, 42 (pictured) was yesterday afternoon pronounced dead at his family home in Sinza Dar es Salaam after a long illness.
After several false alarms about his death, the news was confirmed by his elder brother, Mr Jabir Masanja, who said the singer had been admitted to Mwananyamala Referral Hospital in Dar es Salaam.
The real cause of his death was not clear at the time we went to press, but in an earlier interview, Banza, who had been restricted to his bed, complained of a severe headache.
The ailment rendered the singer unable to walk or even feed himself properly without support.
News of the singer’s demise hit the social media at about 2.00pm with his legion of fans sending condolence messages to his family.
Radio DJ Fetty and presenter Anna Peter wrote on their Twitter accounts: RIP Banza Stone.
More condolence messages were from Mwana FA, Izo Bizzo and many others who expressed the loss of Banza Stone who many considered as dance music icon.
The singer whose career took off in the early 1990s was famed for hits such as ‘Mtu Pesa’, ‘Angurumapo Simba’,’Mtaji wa Maskini’ and ‘Elimu ya Mjinga’.
In a career that spanned over 20 years, Banza Stone ventured into music at an early age just after he had completed his elementary education in 1987 despite his parents’ disapproval  .
But his real debut into music was in 1990 after his earlier attempts to do hip hop proved futile.
Though many know him for his efforts that catapulted him to fame while at TOT Plus, before he made a career move to The African Stars ‘Twnga Pepeta and later Extra Bongo, he had worked with smaller bands before.
His struggles to make it took him to bands such as  The Heart Strings, Twiga Band, Achigo Band as a drummer and Afri-Swez.


Friday, July 17, 2015

Idd Mbaraka


Nawatakia wadua wote Iddi Njema!  Idd Mbaraka!

Sunday, July 12, 2015

Mzee Ojwang Afariki Dunia!


The Late Benson Wanjau aka Mzee Ojwang
Muigizaji maarufu wa kipindi cha runinga cha "Vitimbi" Benson Wanjau aka
"Mzee Ojwang" ameaga dunia.
Mzee Ojwang ameaga dunia muda mchache uliopita katika hospitali ya kitaifa ya Kenyatta mjini Nairobi Kenya.

Kwa habari zaidi BOFYA HAPA:

Nairobi, Kenya: Kenyan actor Benson Wanjau alias Mzee Ojwang died Sunday evening at the Kenyatta National Hospital where he had been admitted.
Read more at: http://www.standardmedia.co.ke/article/2000168994/end-of-an-era-mzee-ojwang-passes-on
Nairobi, Kenya: Kenyan actor Benson Wanjau alias Mzee Ojwang died Sunday evening at the Kenyatta National Hospital where he had been admitted.
Read more at: http://www.standardmedia.co.ke/article/2000168994/end-of-an-era-mzee-ojwang-passes-on
Nairobi, Kenya: Kenyan actor Benson Wanjau alias Mzee Ojwang died Sunday evening at the Kenyatta National Hospital where he had been admitted.
Read more at: http://www.standardmedia.co.ke/article/2000168994/end-of-an-era-mzee-ojwang-passes-on

Mh. Magufuli Mgombea Rasmi wa Urais Kwa Tiketi ya CCM

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jaaya Kikwete akionyesha kuwa mwenye furaha isiyo kifani baada ya Dk. John Magufui (kulia)  kutangazwa kuwa mshindi, na hivyo kupata ridhaa ya kupeperisha bendera ya CCM kaika uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwaka huu.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akimkaribisha jukwaani, Mke wa Dk. John Magufuli, Mama Janeth Magufuli
"Hili jembe" akisema Rais Kikwete wakati akiwa na Dk. John Maguli na Mama Janeth Magufuli baada ya matokeo ya uchaguzi wa kumpata mgombea wa CCM yaliyotangazwa na Spika wa Bunge Mama Anna Makinda leo mjini Dodoma
Rais Kikwete akionyesha zaidi furaha yake
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete (kushoto) akiwa na Mama Janeth Magufuli, huku Rais Kikwete akiendelea kufurahi

 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akimpongeza Dk. Magufuli

KABLA YA MATOKEO KUTANGAZWA
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwasalimia wajumbe na wageni waalikwa baada ya kuwasili katika Ukumbi wa kisasa wa mikutano mjini Dodoma leo kwa ajili ya shughuli ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi wa kumpata mgombea Urais kwa tiketi ya CCM ambao ulifanyika jana usiku.Kushoto ni Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal, Makamu Mwenyekiti wa CCM Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein na kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete baada ya kuwasili katika Ukumbi wa kisasa wa mikutano mjini Dodoma leo kwa ajili ya shughuli ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi wa kumpata mgombea Urais kwa tiketi ya CCM ambao ulifanyika jana usiku.Kushoto ni Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal, Makamu Mwenyekiti wa CCM Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein na kulia ni Makamu Mwenyekiiti wa CCM Bara, Phlip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akihamasisha wajumbe  ukumbini wakati wakisubiri kutangazwa matokeo hayo
Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idi akisoma taaifa ya serikali, kabla ya kutangazwa matokeo hayo
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akijadiliana jambo na Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohammed Shein wakati yakisubiriwa kutangazwa matokeo hayo. Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akieleza utekelezaji wa serikali wa ilani ya CCM wakati yakisubiriwa kutangazwa matokeo ya uchaguzi huo
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete na Katibu Mkuu wa CCM, Abdurahman Kinana wakitafakari mambo mbalimbali wakati wa kusubiri kutangazw amatokeo ya mgombewa urais kwa tiketi ya CCM katika uchagzi mkuu utakaofanyika mwaka huu
Mwimbaji Ali Star akiimba wimbo maalum wa CCM wakati wa shamrashamra a kusubiri matokeo hayo
Wajumbe na waalikwa wajikimwayamwaya ukumbini wakati wakisubiri matokeo hayo
Katibu Mkuu wa CCM mstaafu Mzee Wilson Mukaa akifuatilia hali ya mambo yalivyokuwa ukumbini wakati yakisubiriwa matokeo hayo
Spika wa Bunge Anna Makinda na Spika wa Baraza la Wawakilishi, Pandu Ameir Kificho, wakimkabidhi leo Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete matokeo ya uchaguzi wa mgombea Urais kwa tiketi ya CCM uliofanyika jana usiku
Spika wa Bunge Anna Makinda akitangaza matokeo hayo baada ya Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete kuyahakiki
Mgombea Urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka huu, kwa tiketi ya CCM Dk. John Magufuli (kushoto) wakati akisubiri kutangazwa kwa matokeo hayo
Walinzi wa usalama,  wakiwa wamemzunguka Dk. John Magufuli mara matokeo yalipoonyesha kuwa ameshinda na hivyo kuwa mgombea rasmi wa Urais kwa tiketi ya CCM leo
Dk. Magufuli akiwa 'amezongwa' na walinzi waliokuwa wakimpeleka jukwaani baada ya kuytangazwa kuwa ndiye mshindi
Dk. Magufuli akiwa 'amezongwa' na walinzi waliokuwa wakimpeleka jukwaani baada ya kuytangazwa kuwa ndiye mshindi
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akimsubiri kwa hamu Dk. John Magufuli wakati akipanda jukwaani
Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete akimkubatia kumpongeza Dk. Magufuli kwa kupata ushindi
Rais Kikwete akizidi kumpongeza Dk. Magufuli
"wewe ni jembe letu" akasema Rais Kikwete
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akimnadi kwa wajumbe Dk. Magufuli baada ya kutangazwa mshindi
Dk. Magufuli akimshuku Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohammed Shein kwa jinsi Chama kilivyosimamia uchaguzi na kumalizika salama
Dk. Magufuli akimsalimia Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimpongeza Magufuli
Baadhi ya wadau ndani ya ukumbi wakati wa kutangazwa matokeo hayo.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimpongeza kwa furaha, Mama Janeth Magufuli
Aliyekuwa akiomba ridhaa ya CCM kuwania Urais, Mwigulu Nchemba naye akiungana na wadau kufurahia Dk. Magufuli kuibuka mshindi

BAADA YA MAGUFULI KUWA MGOMBEA RASMI KWA TIKETI YA CCM
 Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohammed Shein akitoa maelezo alivyjipanga kuongoza tena mhulamwingie, kufuatia kuteuliwa tena kuwa mgombea wa Urais wa zanzibar kwa tiketi ya CCm katika uchaguzi utakaofanyika mwaka huu
 Aliyekuwa mgombea wa kupata ridhaa ya kugombea Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. Asha Rose Migiro akitoa shukrani zake, wakati wa kutangazwa matokeo ya mgombea urais kwa tiketi ya CCM na yeye kuibuka watatu kutokana na kupata kura chache Kushoto ni mumewe, Profesa Migiro
 Aliyekuwa mgombea wa kupata ridhaa ya kugombea Urais kwa tiketi ya CCM Balozi Amina Ally akitoa shukrani zake, wakati wa kutangazwa matokeo ya mgombea urais kwa tiketi ya CCM na yeye kuibuka wapili kutokana na kupata kura chachedhidi ya Dk. Magufuli
  Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM katika uchaguzi utakaofanyika mwaka huu, Dk. John Magufuli, akitoa maelezo yake alivyojipanga kuongoza nchi, baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa kupata nafasi hiyo matokeo ya uchaguzi uliofanyika jana usiku yalipotangazwa leo
  Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM katika uchaguzi utakaofanyika mwaka huu, Dk. John Magufuli, akimnadi Mgombea wake mwenza, Samiah Suluhu, baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa kupata nafasi hiyo matokeo ya uchaguzi uliofanyika jana usiku yalipotangazwa leo
 Samiah Suluhu akitafakari baada ya kuteuliwa na Dk. Magufuli kuwa mgombea wake mwenza

 Kisha akaonyesha furaha yake ya kuteuliwa huko kuwa mgombea mwenza
 Mama Janeth Magufuli akimpongeza samiah Suluhu. Kulia ni Mama Mwanamwema Shein
 Mama Salma Kikwete akiungana na Spika wa Bunge Mama Anna Makinda kumpongeza Samiah Suluhu
Mweneyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete akiufunga Mkutano Mkuu maalum, baada ya shughuli ya kutangaza matokeo ya mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM kumalizika leo, mjini Dodoma
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwapongeza Dk.Magufuli na Samiah Suluhu baada ya kuufunga mkutano huo.
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete na baadhi ya viongozi wa meza kuu, wakiwa katika picha ya pamoja na Dk, Magufuli na Samiah Suluhu baada ya kufunga mkutano huo
 Rais Mstaafu Ali Hassani Mwinyi akiondoka ukumbini huku akiwa amemshika mkono Dk. Magufuli. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO NA ADAM MZEE