tag:blogger.com,1999:blog-17229004.post8833849516388935984..comments2024-03-22T03:02:53.585-04:00Comments on Swahili Time: MBunge Adai Naibu Spika Mhe. Job Ndugai Ameshindwa Kuendesha vikao vya BungeChemi Che-Mpondahttp://www.blogger.com/profile/16717731951202118305noreply@blogger.comBlogger1125tag:blogger.com,1999:blog-17229004.post-66810184891655099452011-08-11T15:17:51.612-04:002011-08-11T15:17:51.612-04:00Nilisikiliza na kuangalia kwenye luninga tukio lot...Nilisikiliza na kuangalia kwenye luninga tukio lote...Mh Nyika aliomba "ruksa aombe Mwongozo" kwa kupitia Kanuni ya Bunge akitaka ufafanuzi juu ya kipengele cha Katiba ya Nchi...Lakini Naibu Spika hakumpa ruksa kuomba Mwongozo badala yake akajifanya aliisha jua Mh Nyika alitaka kuomba Mwongozo gani anakajitolea eti kutoa maelezo juu ya matakwa ya kipengele cha Katiba...Huu ulikuwa upotoshaji wa lengo la Mh. Nyika kwa makusudi ili hasipate ruksa ya kuomba Mwongozo.

Pale Mh Ndugahi alionyesha wazi wazi kuwa hakutaka Mh Waziri Mkuu abanwe kuhusu msimamo wake kuhusu sakata la umeya wa Arusha na kuhusu alichozungumza na viongozi wa Kitaifa wa Chadema. Leo kwa mara ya kwanza nimeshuhudia Ndugu Ndugahi na Ndugu Pindi wakicheza karata ya ushabiki na ubabe wa chama cha CCM kama nilivyozoea kuona Ndugu Nape na Mh Chatanda yule Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Tanga wanavyofanya siku zote..Inaelekea Mh Pinda ameamua kurudi nyuma na kucheza mchezo wa akina Nape na Chatanda wa kudhani sakata la umeya litaisha kwa ubabe ukipokezana na kuwaonga kwa vyeo wasio na uadilifu ndani ya Chadema Arusha mjini.

Mh. Pinda alinisononesha kujiingiza kwenye siasa uchwara kama akina Nape na Chatanda. Nilimuonea huruma sana. Labda mtoto wa mkulima na yeye anaanza kuota ndoto za kuwa ngombea wa kiti cha urais 2015 na anabidi akubalike kwa watetezi wa siasa uchwara nadni ya chama chake masikini!! Kama kinachoitwa uchanguzi wa meya Arusha haukuwa na utata sasa maridhiano na wale madiwani wa Chema waliofukuzwa yalikuwa ya nini, yarabhi? Na kama Chadema wamekosea katika kuwafukuza wale madiwani wao waliopewa uongozi katika halmashauri kama zawadi na CCM sasa CCM si isherehekee kuvipata viti hivi vya umeya kiulaini kwa kuwasimamisha hao hao madiwani waliofukuzwa na Chadema, au siyo?

Hivi chama cha siasa kikimfukuza diwani au mbunge si yuko huru kuamia chama kingine na kama bado anapendwa si atashinda kiti husika kwa kishindo?Mbona sasa Waziri Mkuu anawashauri madiwani wale waliofukuzwa eti waende mahakamani kudai haki? Haki gani tena? Si angewashauri wajiunge na CCM na CCM iwateue kugombea na watashinda bila wasiwasi kama kweli wananchi husika wanaona Chadema iliwafukuza kwa kuwaonea? Mh Pinda leo amejisogeza karibu na wakina Ndugahi, Nape na Chatanda wa CCM ambao bila shaka yoyote Mh Rostam Aziz , licha ya madhambi yake yote, aliwapatia aliposema ni watetezi wa "siasa uchwara" ndani ya CCM.Anonymousnoreply@blogger.com