Saturday, August 20, 2016
Mama Bishanga Ndani ya White Party ya Birthday ya Rukia Hussein
Kwa Hisani ya Christina Marolen aka Mama Bishanga
MAMA BISHANGA NDANI YA WHITE PARTY YA BIRTHDAY YA RUKIA HUSSEIN
Rukia mtoto wa marehemu Sheihk Yahya Hussein aliangusha bonge ya white party kusherehekea miaka 50 ya birthday yake kwenye hoteli babu kubwa ya Marrioti, jijini Cleveland Ohio. Mambo yalikuwa mambo haswaaa!
Rumba lilinoga kwa nyimbo za nchi mbali mbali za Africa na hasa za maarufu home TZ za Bado, number one, bora uende, colors of African, na nasema nae taarabu ambao mume wa Rukia ilibidi awekwe kitini na kukatiwa mauno kisawasawa na mkewe na waalikwa akina Mama Bishanga, Prisca Zenda, Michelle Mujuni nk walipotupia mduara wa nguvu! Wapendwa angalieni picha mpate picha ya mambo yalivyokuwa bam bam!
HAPPY BIRTHDAY RUKIA MUNGU AKUONGEZEE UMRI, MAFANIKIO, NA
FURAHA YA MAISHA YAKO NA NDOA NA FAMILIA YAKO!
MAMA BISHANGA NDANI YA WHITE PARTY YA BIRTHDAY YA RUKIA HUSSEIN
Rukia mtoto wa marehemu Sheihk Yahya Hussein aliangusha bonge ya white party kusherehekea miaka 50 ya birthday yake kwenye hoteli babu kubwa ya Marrioti, jijini Cleveland Ohio. Mambo yalikuwa mambo haswaaa!
Rumba lilinoga kwa nyimbo za nchi mbali mbali za Africa na hasa za maarufu home TZ za Bado, number one, bora uende, colors of African, na nasema nae taarabu ambao mume wa Rukia ilibidi awekwe kitini na kukatiwa mauno kisawasawa na mkewe na waalikwa akina Mama Bishanga, Prisca Zenda, Michelle Mujuni nk walipotupia mduara wa nguvu! Wapendwa angalieni picha mpate picha ya mambo yalivyokuwa bam bam!
HAPPY BIRTHDAY RUKIA MUNGU AKUONGEZEE UMRI, MAFANIKIO, NA
FURAHA YA MAISHA YAKO NA NDOA NA FAMILIA YAKO!
Birthday Girl Dada Rukia Hussein Awasili |
Mama Bishanga (Kulia) na Birthday Girl |
Mashindano ya Miss Mwanza 2016
Usiku wa jana Ijumaa Agost 19,2016 kuamkia leo Jumamosi Agost 20,2016, kulikuwa na mtifuano mkali wa kumtafuta mlimbwende wa taji la MISS MWANZA 2016 ambapo warembo 16 kutoka wilaya mbalimbali mkoani Mwanza walijitosa kusaka taji hilo.
Ilikuwa ni furaha kubwa kwa mrembo, Mary Peter (katikati), pale alipotangazwa kuwa MISS MWANZA 2016. Pia mwendelezo wa furaha uliwaendea warembo, Victoria Boniphace (kushoto) aliyetangazwa Miss Mwanza nambari mbili na Winnie Shayo (kulia), aliyetangazwa Miss Mwanza nambari tatu.
Kinyang'anyiro cha Miss Mwanza 2016, kiliandaliwa na Kampuni ya "Big D Entertainment" na baada ya kinyang'anyiro hicho, unafuata mtifuano wa MISS LAKE ZONE 2016 utakaofanyika Septemba 10,2016 ambapo washiriki wa Miss Mwanza 2016 waliongia nafasi tano bora, wanashiriki moja kwa moja kwenye shindano hilo.
Na BMG
Miss Mwanza 2015, Donny Roberty (kushoto), akimkabidhi taji Miss Mwanza 2016, Mary Peter (kulia) baada ya kuibuka mshindi wa shindano hilo.
Washiriki wa Miss Mwanza, walioingia nafasi tano bora
Warembo walioshiriki Miss Mwanza 2016
Warembo walioshiriki Miss Mwanza 2016.
Warembo walioshiriki Miss Mwanza 2016
Majaji walikuwa na Kazi pevu kuchagua mshindi
Baadhi ya waliohudhuria kwenye tukio
Msanii Elizayo HB kutoka Jijini Mwanza akidondosha burudani kwenye Miss Mwanza 2016
Burudani za kiafrika pia zilikuwepo
Mkali wa Moyo Mashine, Ben Pol, alidondosha burudani poa sana
Ben Pol kazini
Kupitia BMG, Ben Pol, aliwashukuru wakazi wa Jiji la Mwanza kwa namna wanavyopenda kazi zake na kuahidi kufanya kazi nzuri zaidi.
Miss Mwanza 2016 aliiambia BMG kwamba, maandalizi yake mazuri ndiyo yaliyompa fursa ya kunyakua taji hilo na kwamba amejiandaa vyema kwa ajili ya taji la Miss Lake Zone 2016 na pia Miss Tanzania 2016.
Miss Mwanza 2016 nambari mbili akibonga na BMG. Anasema shauku yake ni kuongeza juhudi zaidi ili kunyakua taji la Miss Lake Zone 2016.
Friday, August 19, 2016
Benki ya Dunia Kuendelea Kusaidia Sekta ya Maji Nchini
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson
Lwenge akifungua kikao cha pamoja na
ujumbe wa Benki ya dunia, Wizara ya Maji ,Shirika la Majisafi na Majitaka
jijini Dar es Salaam (Dawasco ) na Mamlaka ya Majisafi na Majitaka jijini Dar
es Salaam (Dawasa) namna ya kutatua changamoto za usambaza Maji kwenye Jiji la
Dar es Salaam yakiwamo Mivujo na Miundombinu chavu , kilichofanyika Jijini Dar
es salaam.
Dar es Salaam.
KATIKA
kuhakikisha sekta ya Maji inakua kwa kasi na inatosheleza mahitaji ya sasa ya
huduma ya maji, Benki ya Dunia imejitolea kulisaidia Shirika la Majisafi na Majitaka
jijini Dar es salaam (DAWASCO), ili kusaidia katika upatikanaji wa huduma ya
Majisafi na Majitaka katika maeneo mbalimbali ya wakazi wa jiji la Dar es
salaam pamoja na Miji ya Kibaha na Bagamoyo mkoani Pwani.
Hayo
yamezungumzwa na Mwakilishi wa Benki ya Dunia nchini, Bi. Bella Bird, ambaye
alikuwa ameambatana na wajumbe wake katika kikao cha pamoja na Waziri wa Maji,
Mhandisi Gerson Lwenge, pamoja na Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es
Salaam (DAWASCO).
Kikao ambacho kililenga uboreshaji na upatikanaji wa huduma
ya Maji katika maeneo kadhaa ya jijini Dar es Salaam hasa maeneo ambayo
hayajafikiwa na huduma hiyo.
Aidha,
Mwakilishi huyo wa Benki ya Dunia, ameridhishwa na juhudi za makusudi
zinazofanywa na Dawasco katika kuwapatia wananchi huduma ya Majisafi, pamoja na
kupambana na kiwango cha Maji kinachopotea bila sababu ya msingi.
Ameeleza
kuwa Benki ya dunia imetenga fedha kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya Majisafi
na Majitaka ili kuimarisha uendeshaji wa utoaji wa huduma ya Maji kwa wananchi,
ikiwa ni pamoja na kutekeleza kikamilifu kampeni ya “Mama Tua Ndoo Kichwani” ili kuwapunguzia akina mama wengi tatizo la
Maji, kwani ndio wanaoonekana kuwa wahanga wakuu wa tatizo hilo.
“Nimeridhishwa
na utendaji wenu wa kazi, jinsi ambavyo mmejipanga katika kufanya kazi, hasa
juhudi zenu mnazoziweka katika kupambana na upotevu wa Maji na kuwapatia
wananchi huduma ya Maji” alisema Bi.
Bird
Naye,
Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco, Mhandisi Cyprian Luhemeja ameishukuru Benki ya
Dunia kwa ushirikiano mzuri waliouonesha, na kwamba kiasi cha fedha
kilichotengwa na Benki ya Dunia kitatumika katika kuboresha na kutatua
changamoto mbalimbali zinazolikabili shirika katika utoaji wa huduma ya Maji.
“Changamoto
ni nyingi katika utoaji wa huduma ya Maji, naamini kuwa kiasi cha fedha
kilichotengwa kitasaidia kuondoa changamoto hizo” alisema Mhandisi Luhemeja.
Benki
ya dunia imekuwa ikifadhili miradi mingi ya maendeleo hapa nchini ikiwamo
miradi mbalimbali katika sekta ya Maji, Nishati na Madini, Kilimo na Mifugo,
pamoja na Uchumi na Biashara.
Sunday, August 14, 2016
Saturday, August 13, 2016
Mwenyekiti Mpya wa CCM Dr. John Pombe Magufuli Apokelewa kwa Nderemo na Vifijo
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipungia wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa J.K. Nyerere, Jijini Dar es salaam kabla ya kwenda kuwahutubia wana-CCM wa Dar es salaam baada ya Ofisi Ndogo za CCM mtaa wa Lumbumba leo agosti 12, 2016.
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Dar es salaam.
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akifurahia burudani za aina mbalimbali wakati alipowasili Jijini Dar es salaam leo, akitokea Jijini Mwanza.
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipiga ngoma kutoka kwa moja ya vikundi vilivyokuwepo uwanjani hapo.
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiwapungia wananchi waliofika Uwanjani hapo kumlaki leo.
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongea na viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndehe wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es es salaam leo agosti 12, 2016.
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John
Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na baadhi ya wanaCCM pindi alipowasili Ofisi Ndogo ya Chama hicho, Mchana wa leo.
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John
Pombe Joseph Magufuli akiongozana na Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Abdulrahman Kinana, Naibu Katibu Mkuu Bara, Ndg. Rajab Luhwavi mara baada ya
kuwasili Ofisi ndogo ya CCM, Mtaa wa Lumumba Jijini Dar es salaam leo.
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John
Pombe Joseph Magufuli akisaini Kitabu cha wageni kwenye Ofisi Ndogo ya CCM, iliopo Mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam leo agosti 12, 2016
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John
Pombe Joseph Magufuli akikifanya Mazungumzo na Viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali, katika Ofisi Ndogo ya CCM, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam leo agosti 12, 2016.
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John
Pombe Joseph Magufuli akizungumza na Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Abdulrahman Kinana pamoja na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es salaam, Ndg. Ramadhan Madabiba.
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John
Pombe Joseph Magufuli akisikiliza jambo kutoka kwa Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Abdulrahman Kinana .
Mke wa Rais, Mama Jannet Magufuli akiwa na Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson.
Mke wa Rais, Mama Jannet Magufuli akiwasalimia wananchi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza.
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akihutubia wana-CCM wa Dar es salaam baada ya kupokelewa kwa nderemo na vifijo Ofisi Ndogo za CCM mtaa wa Lumbumba jijini Dar es es salaam leo agosti 12, 2016.
Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Paul Makonda akiteja jambo na Wakuu wa Wilaya za Ilala (Sophia Mjema) na Kindondoni (Ally Hapi).