Tuesday, July 03, 2007

Wazazi Wangu safarini Boston

Kutoka Kushoto, Mhesimiwa Frederick Sumaye, Dr. Aleck Che-Mponda, mimi na mama yangu. Tulienda kumsalimia Mheshimwa Sumaye, ambaye kwa kweli alikuwa mkarimu sana. Msaidizi wake alitupikia mishikaki mitamu kama nyumbani. Mheshimiwa Sumaye amemaliza masomo yake Harvard University hivi karibuni.


Baba akiagana na Mheshimiwa Sumaye ambaye alikuwa jirani yangu hapa Cambridge, Ma. Ndo siku nilikabidhi kanda za sinema ya Tusamehe na Bongoland.

Baba na Mama wakiwa South Station, Boston Ma. kuelekea New York City ambapo walienda kusalimia ndugu na marafiki.


Dr. Aleck Che-Mponda akicheki sanamu ya mbwa aina ya St. Bernard huko Mohegan Sun.

14 comments:

  1. Sumaye ni mtu simple na mkarimu sana. Mimi nampongeza kwa kujiendeleza na kuonyesha mfano kwa watoto/vijana kuwa elimu haina mwisho. Kila la heri Mhe Sumaye!

    ReplyDelete
  2. Picha nzuri chemi
    hivi dingi (Baba) yako aliachana na siasa?? simsikii kabisa siku hizi. Good for him...

    ReplyDelete
  3. Da chemi, asante kwa kutuonyesha picha za wazazi wako, nimefarijika kwa kweli. Bahati mbaya, kwa mapenzi ya Mungu, mie wazazi wangu wote wawili walifariki nikiwa bado mdogo sana. Hivyo sijapata mapenzi ya wazazi wangu. Mungu awazidishie afya njema na Umri tele hadi wawe wikongwe wazazi wetu hao! MUNGU AWABARIKI JAMANI.

    ReplyDelete
  4. Kumbe yule mwanasiasa ndo baba yako ila siku hizi simsikiii au alisharudi CCM?

    Hivi Chemi, US unasoma au unakula mzigo ingawa naona kwa mwili wako huwezi beba maboksi lakini waweza kuosha vizee hahahahahaha

    Cheers ila ingia gym mama mwili mkubwa

    ReplyDelete
  5. Da Chemi, nimefurahi kuwaona wazazi "wetu".. maana mzazi wa mwenzio naye wako.

    Majirani zetu Chuo though long time. Inakumbusha mitaa ya Mlimani, Sinza Road, Simba road, Darajani , UDASA etc. jamani... hakuna awali iliyo mbovu..

    Mlimani kina mwl. Mndolwa, Elia, Mujwahuzi etc Mungu awabariki sana walimu hao kwa kututoa tongotongo.

    ReplyDelete
  6. Chemi naona ulikuwa na ugeni mzito. Hongera sana. Wazazi wako wamependeza.

    ReplyDelete
  7. Yaani ulimpeleka kucheza kamari...CHEKA!

    ReplyDelete
  8. Chemi your blessed, your parents (ours too) look strong and they should be nice too. My God bless the family.

    Vijana chukueni mfano ndoa zenu siku hizi ni za miezi tu na mnashindana eti harusi iwe ya gharama sana lkn za baba zetu zilikuwa simple, cheap na "hadi kifo kitutenganishe!"

    ReplyDelete
  9. Mswali mawili:

    (a) Sumaye alikuwa na msaidizi wa kumchomea mishikaki? Mbona alitangaza kuwa alikuwa akijipikia na kujifanyia kila kitu mwenywe bila msaidizi yeyote, na kwamba kila mtu alikuwa akimwita Freddie. Je huyu alikuwa msaidizi wa namna gani ambaye angemwita Freddie?


    (b) Baba yako Dr. Che-Mponda yuko wapi siku hizi? Nakumbuka aliondoka UDSM na kuanzaisha chama chake kwa kishindo. Tangu uchaguzi wa 1995 sijamsikia tena katika siasa, je kaamua kurudi kwenye chaki pale UDSM?

    Safari njema huko Dar.

    Usikose kuniletea konyagi. Mimi nipo Amherst; tutawasiliana.

    ReplyDelete
  10. Kumbe huyu mzee yupo, nakumbuka chama chake kilikuwa kinaitwa CCM-B sababu alikuwa hapingani na matakwa ya CCM.

    ReplyDelete
  11. Ila Chemi usije ukawa wewe ndo ulikuwa msaidizi wa Sumaye, na mimi Sumaye ninavyomwelewa kwa totoz lazima hukukatize kwenye anga zake. Any way sio mbaya lakini

    ReplyDelete
  12. Hivi Baba Che Mponda anafanya kazi gani? Historia yake ni mwanasiasa siyo? Hebu nieleweshe kidogo.
    Matt

    ReplyDelete
  13. Anonymopus wa 11:57PM, usiwe na wasiwasi. Sumaye alikuwa na msaidizi wa kiume.

    ReplyDelete
  14. Ni lini utajibu haya maswali?? Mengine ni so private hata usipojibu wengine hayatuhusu labda uombe e-mail address za waliouliza ili uwajibu. Lakini yote yaliyomuhimu tunaomba majibu

    ReplyDelete