Tuesday, January 22, 2008

Bi Ruby Dee ni mweusi pekee kuteuliwa kupata Oscar mwaka huu!


Leo asubuhi majina ya walioteuliwa kupata Oscar yalitangazwa. Bi Ruby Dee (84) ni mweusi peke yake kuteuliwa mwaka huu. Ameteuliwa katika category ya Best Supporting Actress. (naomba mnisaidie kutafsiri hapo) Mwigizaji Bora wa kike ........
Ametueliwa kwa kazi aliyo fanya katika sinema, American Gangster. Katika sinema hiyo alicheza kama Mama Lucas ambaye ni mama mzazi wa Frank Lucas, mhusika mkuu wa sinema hiyo. Nafasi hiyo ilichezwa na Denzel Washington.
Bi Ruby Dee ameigiza katika sinema nyingi tena vizuri sana lakini hii ndo mara ya kwanza yeye kuteuliwa. Tena ana miaka 84! Nangojea kusikia anasemaje kuhusu kuteuliwa kwake!

Hakuna sinema kutoka Afrika iliyoteuliwa mwaka huu.

Sherehe ya kutuza Oscar itafanyika Februari 24, mwaka huu huko Kodak Theatre, Hollywood.

7 comments:

  1. Like I said;no.African.nominated.

    Maybe next time Kanumba fans,maybe next time...and when I say 'next time',i'm referring to a time period where robots are a household standard.

    ReplyDelete
  2. Hawa waandaaji wa Oscars watakuwa wabaguzi.How come wamuone huyo Ruby Dee pekee ilhali Denzel wetu wa TZ amelishawasili huko mapema kwa ajili ya TUZO YAKE YA TATU....baada ya ile ya John Wayne,ile ya Universal,na sasa Oscars.....Kanumba must appeal.

    ReplyDelete
  3. ^ LOL I know right?They honestly thought dude was nominated for an Oscar,LMFAO

    But it's all good though,he still has the Universal Studios souvenir XD

    ReplyDelete
  4. Mbona huyu naye ni mzungu pia? Wewe chemi umeishi Afrika sasa kwanini unajifanya huwajui watu weusi?

    ReplyDelete
  5. Anonymous wa 5:29Pm, hapa Marekani ukiwa na tone ya damu nyeusi wewe ni mweusi. Ruby Dee ni African American.

    ReplyDelete
  6. Tafadhali usiniambie kuwa hii picha ameipiga akiwa na miaka 84! labda uniambie aliipiga zamani kidogo maana nikimfananisha na Shangazi yangu huku Bongo aliye na miaka SABINI na ambaye tunafanya kumbeba kumtoa juani...!!?!

    ReplyDelete
  7. Ndo faida ya Plastic surgery na botox! Huzeeki!

    ReplyDelete