Tuesday, March 25, 2008

Sinema ya Mall Cop

Hapa niko Holding Area nangojea kuitwa kwenye seti. Kwa nyuma kabisa ndo walikuwa wanapaka watu make-up na kutengeneza nywele na sehemu ya kubadilisha nguo. Holding ilikuwa kwenye tent iliyowekwa kwenye parking lot ya Mall.
Mimi na Mwanangu


Wadau, hamkujua kuwa nilifungua miezi mitatu iliyopita! Jina la mwanangu ni Prop.

Ukweli huyo ni mdoli. Jana, nilikuwa extra kwenye sinema 'Mall Cop aka. Untitled Kevin James Project.' Hatujui itaitwa nini ikitoka mwakani.

Kulikuwa na hizi baby strollers kama 5 zenye midoli halafu Prop Master (anayegawa vifaa), alikuwa anachagua watu wa kuwa Moms. Ukichaguliwa unapewa stroller. Wengine walipewa shopping bags zilizojaa vitu kama makaratasi na chupa tupu. Sasa sinema ikitoka utaona huyo mtoto anasukumwa na watu mbalimbali, lakini kwa asiyejua wanavyotengeneza sinema utadhani kila mtu ana mtoto wake. Partner wangu kwenye set alikuwa mwanaume wa kizungu anaitwa Steve.

Tulikuwa extras zaidi ya 250 ilikuwa shuti kubwa Burlington, Mall, huko Burlington, Massachusetts. Tulifika kwenye set saa 11:30 (5:30am) na kuruhusiwa kuondoka saa 1 jioni (7:00PM). Siku ilikuwa ndefu. Na miguu wa watu iliuma maana kazi yetu ilikuwa kutembea mle kwenye seti na kujifanya ni shoppers.

Tulikuwa na yule Kevin James, wa ile show, The King of Queens. Yeye ndo stelingi. Nilipita nyuma yake. Sijui kama nitaingia kwenye final cut yaani picha ambao watu wataiona kwenye sinema.

11 comments:

  1. Kwanza kabisa umependezaa,harafu nakupongeza kwa kujitokeza kushiriki hiyo shooting . Yaani wanawake kama wewe nawapenda kwa kuwa active namna hiyo,keep it up utafika mbali na kuzidi kuwa inspiration kwa wapenda maendeleo.

    ReplyDelete
  2. Endelea na moyo huo. Safi sana! Iko siku tutasikia umepata role kubwa. Hongera!

    ReplyDelete
  3. Gud Job...mwanzo huo maanake watu wote unaowaona wamefanikiwa wameanzia chini kama wewe usikate tamaa utafika 2..

    ReplyDelete
  4. Kwa mara ya kwanza na thubutu kubonyeza kizenji keyboard yangu ili kukupongeza wewe dada chemi!

    I am impressed...!What I can say bravo chemi, I am proud of you!

    I always call "a spade a spade, not a big spoon"

    ReplyDelete
  5. Iam proud of you DADA CHEMI keep it up.what else can I say keep making us proud of you.

    Love u

    Manka Mushi

    ReplyDelete
  6. Kama pesa zenyewe Chemi ndiyo unazihangaikia hivyo heri urudi Tanzania kulima

    ReplyDelete
  7. chemi we lazima utakuwa muhaya.

    ReplyDelete
  8. Binafsi ni naamini unaweza na utafika mbali sana sana.

    Mungu awe na wewe uwe mbunifu zaidi.

    Haupo peke yako Da Chemi.
    Tupo pamoJAH!

    Tutafika tu

    ReplyDelete
  9. Popote alipo Mbongo anawakilisha Bongo(kwa mema na yenye haki lakini), basi wewe wakilisha na mimi nakutakia kila la kheri.

    ReplyDelete
  10. Dada Chemi wala usimjali huyo anonymous number 6 aliyesema eti bora urudi kulima ndio hao wasiopenda maendeleo . We anonymous number 6 acha kuwa na mawazo finyu.

    ReplyDelete
  11. Whoa! Hongera sana dada Chemi!
    I have many reason to be proud of you, yaani unaka'baby alafu bado unachapa kazi kwenda mbele?...safi sana!

    ReplyDelete