Friday, March 14, 2008

Mwafrika ashinda Dola Millioni moja kwenye Lottery Boston!


Kushoto ni Bwana Samuel Gbotee, ambaye kashinda dola milioni moja ($1,000,0000) kwenye tiketi ya bahati nasibu ya Massachusetts. Alipata donge nono kwenye tiketi ya '$5,000,000 Jackpot ' ambayo inauzwa kwa dola $10 kila moja. Kwa muda wa miaka ishirini atalipwa $50,000 kwa kila mwaka. Alinunua tiketi yake kwenye kituo cha petroli huko Lowell.
Bwana Gbotee anatoka Liberia, kwa sasa anakaa Lowell, Massaschuetts.
Jaribuni bahati yenu!
Kwa habari zaidi BOFYA HAPA:

3 comments:

  1. Mimi ndiye nitakayefuatia kwenye donge nono lijalo, hapa nilipo tu napiga maktaimu, naisubiria siku yangu inakuja.

    ReplyDelete
  2. Nimenunua za aina nyingi! Sijawahi kuambulia zaidi ya dola mia! Huyo njemba ana bahati kweli!

    ReplyDelete
  3. Naweza kumpata swapi huyo Bwana Gbotee? Nataka kuwa mke wake wa pili!

    ReplyDelete