Monday, April 10, 2006
Umeona Phat Girlz?
Kama hamjaenda kuona sinema mpya, Phat Girlz, nawashauri mkaione. Mchezaji mkuu wa hiyo sinema ni mwigizaji na mcheshi, Mo’nique. Nilienda kuiona wiki iliyopita na kwa kweli nilifurahi sana kuona hiyo sinema na hasa zile scene zilizohusu Afrika na mila za Nigeria. Sehemu ya picha ilipigwa Lagos, Nigeria. Hii sinema ilitungwa na kuwa directed na dada Nngest Likke ambaye ana asili ya Eithiopia.
Wahusika wakuu katika filamu hiyo ni Jazmin Biltmore, rafiki yake Stacey, ambaye naye ni menene kiasi, halafu binamu yake Jazmin, Mia. Huyo Mia ni mwembamba, hana matako na anajiona mzuri mno kwa vile yuko shepu hiyo ambayo Hollywood insema ni nzuri. Ila ku-maintain hiyo shepu anaishi kwa kula karoti, lettuce na maji tu.
Sinema inanza na Dada Jazmin akiwa ndotoni. Wanaume wazuri wazuri wanamtaka kimapenzi. Baadaye tunagundua kuwa ni siku nyingi tangu aonje penzi. Jazmin anatamani sana aweze kuvaa nguo saizi 5. Lakini kama alivyo anavaa saizi 20+. Ana kula vidonge vya kupunguza unene kama pipi lakini hazimsaidii. Anafanya kazi na rafiki yake Stacey kwenye duka la kuuza nguo, inaitwa Bloomfeld’s.
Basi wanalalamika kuhusu jinsi hakuna nguo nzuri dukani kwa ajili ya wanene. Nguo zenyewe ni mbaya mbaya, hazipendezi, au kumfanya aliyevaa apendeze. Na Jazmin ana kipaji cha Designing, na ndoto yake ni kuwa na line ya nguo zinazopendeza kwa ajili ya wanene.
Basi siku moja anaingia kwenye mashindano ya kupata safari kwenda kwenye Spa/Hotel Palm Springs. Kwa bahati nzuri Jazmin anashinda. Yeye, Stacey na Mia wanaenda kustarehe kwa wiki moja kwenye hiyo Spa. Kufika huko wanakuta kila kitu kiko kwa ajili ya wembamba, hata zile massage tables, na robes. Basi Jazmin akiingia kwenye Spa, hao wembamba wanatoka kuonyesha hasira na unene wake.
Wanaenda kwenye Bwawa la kuogelea. Basi Mia kavaa bikini yake anajiona kapendeza kweli kweli. Yuko karibu uchi na bikini enyewe ni kama lithong. Kuna baba mweusi anaogelea, na Mia anamtamani kweli kweli. Na yule baba anatazama tazama walipo akina Jazmin, basi Mia anadhania lazima anamtazama yeye kwa vile ndo mwembamba kati yao. Yule baba anatoka kwenye maji na kuelekea kwa akina Jazmin. Jamaa ni mzuri kweli halafu mwili wake fiti. Mia anajua kuwa anamfuata yeye, basi yule baba anawasalimia na anamw-ignore Mia. Hawezi kutoa macho yake kwa Jazmin. Jazmin mwenyewe anapumbazwa maana hawezi kuamini kinachotokea. Anakosa maneno ya kusema. Yule baba ni Dr. Tunde, na kumbe yuko Palm Springs na wenzake kutoka Nigeria kwa ajili ya Mkutano wa madaktari.
Marafiki wawili wanamfuata Tunde kwa akina dada hao. Hapo inachekesha maana wanaongea kikwao huko wakimgombania Stacey. Hakuna anayemtaka Mia kwa vile ni mwembamba mno. Wanamwita kibiriti. Jioni wote wanaenda kwenye party ya waNigeria na yule Daktari aliyemwambulia Mia anaona haya na kuwaambia waNigeria wenzake kuwa ni mgonjwa wake. Na yule ambaye amempata Stacey anamsifia, mpaka Stacey anaondoa haya aliokuwa nayo. Basi Stacey akishavua haya loh, anaelekea kama anajaribu kulipiza siku alizokaa bila kupata penzi.
Basi hiyo scene ya Party utafurahi, maana wanaonyesha vyakula vya KiNigeria. Ugali wao ndo 'fufu' kuna samaki ya kukaanga, nyama choma, mboga za majani. Party inafanana na Party tunazofanya za waBongo. Halafu kwenye scene hiyo wameweka ule wimbo wa Kasongo. Cheki Jazmin na Tunde wanavyocheza. Jazmin na Tunde wanakuja kupendana lakini Jazmin anakuwa na wasiwasi kuwa haiwezi kuwa kweli. Yeye anaamini kabisa kuwa mwanaume mzuri hawezi kumpenda kwa sababu ni mnene. Mpaka Jazmin anamwaidi Tunde kuwa atakuwa saizi 5. Tunde anampa ukweli anamwambia kuwa hata siku moja hata kuwa saizi 5 kwa hiyo akubali hivyo.
Basi Mambo yanaenda vizuri mpaka hapo Jazmin anapojidhalilisha akishikwa na wivu. Kwa haya, Jazmin anakimbia na wenzake wanarudi kwao. Jazmin anajifungia chumbani siku kadhaa na anakuwa kama kachanganikiwa akili. Lakini anaamka na kuanza kujiamini. Ndo hapo anafanikiwa kupata line ya Nguo za akina mama wanene inayoitwa Thick Madame na kutajirika. Lakini bado anammisi Tunde, ndo anapanda ndege na rafiki zake na wanakwenda Lagos kumtafuta.
Sitaki kusema zaidi maana nataka muone wenyewe. Kuna vichekesho vingi katika hii sinema, na pia uta huzunika na jinsi jamii ya Marekani inavyowafanya watu kutokujithamini kwa ajili ya unene. Hii sinema ni nzuri maana inafundisha kuwa watu wajipende kama walivyo. Inasikitisha kuwa ilichukua wageni kutoka Afrika kuwafanya Jazmin na Stacey wajue kuwa ni watu wa maana duniani.
Jamii ya Marekani imejenga utamaduni ya kuchukia unene wote, yaani wanataka kila mtu awe mwembamba jambo ambalo haiwezekani. Watu wananjinyima chakula mpaka kupata utapiamlo. Hali inasikitisha. Pia unaona matangazo ya Gym, Vidonge vya diet, vifaa vya kufanyia mazeozi nyumbani, vyakula visivyo na mafuta, na mengine. Lakini ukicheki vizuri yote ni biashara. Je kuchukia unene ni matokeo ya ubepari, maana ukiangalia picha zilizopigwa Marekani katika miaka iliyopita utaona wakina mama wamejaa jaa, na waliitwa warembo. Cheki Marilyn Monroe, na Jayne Mansfield, lakini leo hii wangeitwa wanene. Hii wembamba mpaka mtu anabakia mifupa na ngozi si hali ya kawaida na wala hawapendezi na hawana raha.
Jambo lingine, wenye chuki na wanene na weusi wameipiga sana vita hii sinema. Wanaipigia kura mbaya bila kuiona. Inasikitisha. Nimesoma sehemu kadha watu wakitukana weusi, matako yao makubwa na mengine. Site ya Fox Searchlight ambao ni Distributor wa hii sinema walifuta Message Board ya Phat Girlz, maana ulijaa chuki dhidi ya weusi utadhania ilikuwa website ya wale wabaguzi wa rangi KKK. Bado kuna ubaguzi Marekani.
Nawakaribisha mcheki Blog yangu ya Kimombo http://chemiche.blogspot.com/ nimeandika zaidi hapo.
Chemi wewe ni mwandishi mzuri kwelikweli, tatizo lako ni obsession yako na matako. Yaani huwezi kuandika aya moja bila kutaja neno hilo. Hebu kuwa na simile ya Kiafrika, mara moja si mbaya, lakini kila makala yako, matako, matako, matako, duh! Kulikoni
ReplyDeleteHi lushinge,
ReplyDeleteSasa niyaiteje, makalio? Mimi namini ule usemi wa kizungu, "call a spade, a spade".
chemi,
ReplyDeleteUmekaa kwa wazungu sasa naona uzungu umekukolea :-) Sina tatizo unapolitumia neno nara moja au mbili. Tatizo langu linaanza pale neno hilo linarudiwa rudiwa kuonyesha msisitizo.Kuna post yako moja topic ilikuwa ni hiyo 'matako makubwa' hiyo nayo sina tatizo nayo maana ndiyo hoja ilikuwa imesimama hapo. Lakini ile ya Monique na audition yako na hii ya Phat girls naamini ilikuwa inatosha kabisa kutaja neno hilo mara moja. Hebu niambie nyumbani huku kama uko na watu wa staha unaweza kutaja neno hilo mara kumi kumi? Naamini hata kama unamwelezea mtu mwenye matako makubwa (kama mtungi wa maji wa Wakinga) huwezi kutumia hilo neno kama descrption yake. Watu wazima wana namna yao yakukubali, nafurahi umekubaliana na mimi maana kwenye post yako ya kukoswa koswa kubakwa hukulitumia japo naamini mbali ya vitu vingine, wowowo ndio lililokuponza hasa nyakati hizo ndani ya pt green short ya kijani:-)
Hi Lushinge,
ReplyDeleteKwa kweli ile blog ya kubakwa niliandika kabla sijasoma posti yako. Na sikuona haja ya kutaja matako kwani hapo issue ilikuwa mbele, uke,'K'. Lakini nikuulize unataka niiteje 'matako'?
Halafu je, maneno 'Matako' 'tako" ni matusi?
Nipe adjectives basi, makalio, mjalio, wowowo, siha, mzigo...ongeza basi.
Good design!
ReplyDeleteMy homepage | Please visit
Good design!
ReplyDeletehttp://juyjefig.com/kuwg/gzyc.html | http://wwpcvgvh.com/jxfh/gocc.html