kuanzia kushoto (Elliot, Chris, Katharine & Taylor)
Haya wapenzi wa American Idol, pigo lingine! Chris Daughtry, aliyetabiriwa kushinda mwaka huu katolewa jana! Majaji, na watazamaji walibakia kushangaa. Tulisikia watu waliokuwa studi wakilia, "Noooooo!"! Lakini haikufikia mshangao kama siku ile alivyotolewa Dada Mandisa.
Sasa wamebakia Taylor Hicks (mwenye mvi), Eliiot Yamin (MYehudi na anaumwa ugonjwa wa kisukari), na yule dada aliyesoma Boston Conservatory, Katharine MacPhee. Nani atashinda! Inabidi tungojee May 24th kupata jibu.
Lakini ukweli watu wengi wanashangaa maana kwa wanaume waliobakia hakuna ambaye ungeweza kusema atakuwa ni Idol. Kwanza Taylor ana miaka 29 na ana mvi kibao wengine wanamwita, 'The Old Guy' (Mzee). Lakini jamaa ana character, utampenda tu, ni mcheshi sana na lazima akimaliza kuimba utabakia aunatabasamu. Sasa huyo Elliot wengine wamesema ana sura mbaya, halafu wanamchukia kwa vile Myehudi. Ndio Marekani bado kuna chuki dhidi ya waYehudi. Halafu Elliott mara nyingi anaonekana mwoga na kutoka majasho akiimba. Lakini ana sauti nzuri kiasi.
Haya nimchambue huyo Katharine MacPhee. Hao mibaba wa kizungu inasema, "She's Hot!" Yaani mzuri mno! Mara wapambe wa American Idol wamvalishe nguo mbaya mara nini, lakini bado wanasema ni mzuri mno. Ana sauti nzuri kushinda wanawake wa kizungu wote waliokuwepo mwaka huu. Lakini watu wanachoona ni uzuri wake. Na wiki hii Katharine ndo aliimba vibaya kuliko wote. Alisahau na maneno ya wimbo. Lakini kapita shauri ya uzuri.
Wiki iliyopita alitolewa mweusi pekee aliyebaki, Paris Bennett. Huyo alikuwa na sauti nzuri kuliko wote katika mashindano safari hii, lakini nilijua hatafika mbali, maana bibi yake ni mwimbabji mashahuri na anatuzo za Grammy. Watu walikuwa wanalamika kuwa kwa nini Paris awe kwenye show wakati ana ndugu ambao wanaweza kumsaidia kupata mkataba.
Lakini kulikuwa na njama ya kutoa weusi mapema. Mwanaume mwenye sauti bora kuliko wanaume wote, kijana mweusi Gedeon, alitolewa kwenye Top 24. Na watu walisema kuwa si siri kuwa mwaka huu Producers wa show wanataka mwanaume mzungu ashinde. Kwanza walimpampu huyo Ace kuwa sex symbol, mpaka kumfanyia camera angles na ma close up! Lakini hazikusaidia katolewa wiki kadhaaa zilizopita! Jamaa hakuwa na sauti nzuri, na hata huo uzuri wa sura sijaona. Lakini nasikia anatakoa kwenye gazeti la 'Playgirl' kwa hiyo huenda ni kweli ni sex symbol ana uzuri sehemu nyingine.
Haya, tutaona mwaka huu nani atashinda na kuungana na klabu ya American Idols. Washindi wa miaka ya nyuma ni Kelly Clarkson, Ruben Studdard, Fantasia Barrino, na Carrie Underwood.
Ukweli American Idol umekuwa ni nani anapendwa zaidi, na siyo nani ana sauti bora. Mnaonaje?
Mie niliacha kuangalia alipotolewa Paris. Lakini kwa kuwa hii maneno ni kama hobi nikawa nampigia upatu Chris. Naye sasa katolewa. Pata potea hii sio mchezo. Nabashiri mzee mwenye mvi anafagiliwa sana na huenda akashinda.
ReplyDeleteDada Chemi tungependa kuchangia ila bahati mbaya suala lenyewe hatulielewi vyema.Nashauri utuelekeze labda ni nini na namna ya kufuatilia katika luninga au kwenye internet.Vinginevyo nashukuru umerudi tena baada ya kimya kirefu.
ReplyDeleteMi nasubiri matokeo hapahapa kwako!
ReplyDeleteAsanteni, Kaka John na Kaka Tamba kwa michango yenu. Nami nadhani Taylor (mwenye mvi) atashinda.
ReplyDeleteAnonymous kwa habari zaidi za American Idol nenda http://www.americanidol.com.
Lakini kwa kifupi American Idol ni TV Show ambayo nia ni kumchagua mwimbaji bora Marekani. Hao waimbaji si wataalamu bali watu wa kawaida tu. Umri wao ni kati ya miaka 16-28. Maelfu ya watu wanaenda mbele ya majaji halafu waimbaji bora na wabaya (kama William Hung) wanachaguliwa kuendelea. Wakishapunguzwa kufika 24 ndo watazamaji wanarushusiwa kupiga kura kwa njia ya simu. Mwenye kura nyingi ndo mshindi.
chemi ndugu yangu wengine hayo mambo hatuyapati huku; ndo mana tamba anasema (nami najiunga nae) kuwa tutasubiri humu humu mwako
ReplyDeleteNakushukuru dada Chemi.Sasa nimepata pakuanzia kwani vinginevyo ingekuwa ni kuangalia picha wakati wewe ni kipofu.Au kusikiliza mchezo wa redio wa lugha usiyoijua.Asante sana.Hebu endelea kutupa vitu vipya.
ReplyDelete