Thursday, June 08, 2006

Aftershock - Sinema kuhusu Unyanyasaji wa Weusi















Scene from Aftershock

Habari zenu wapendwa wasomaji? Leo nawajulisha kuhusu sinema inaitwa Aftershock. Film iko sponosred na History Channel na itaonyeshwa kwenye History Channel. Niliwajulisha kuwa nilifanya audition kupata nafasi ya kuigiza kwenye hiyo sinema. Sikupata pati niliyofanyia audition lakini nilipata part nyingine.


Basi juzi nilienda kwenye filming huko Sutton, Massachusetts. Ni kama maili 50 kutoka Boston. Eneo enyewe ni shamba kabisa. Yaani niliposhuka kwenye gari nilifurahi kuona miti mingi, majani, sungura, kuku wanatembea wanavyotaka! Upepo ulikuwa freshi kabisa safi mno! Ama kweli kukaa mjini kunachosha.

Haya kufika kwenye seti ya film, walikuwa wameweka matenti. Moja ya chakula, moja ya make-up, nyingine ya vifaa. Gereji ya nyumba iligeuzwa 'wardobe' (nguo). Nilenda sign-in halafu moja kwa moja nilipelekwa wardrobe kuvalishwa costume. Role yangu ni 'farm hand ' yaani ni 1867 Utumwa umeisha lakini weusi wanaajiriwa kwa hela ndogo sana, na bado kuteswa na kuuliwa ovyo. Walinivalisha sketi nyeusi ndefu, apron, sharti ya dume! Sikuvaa viatu. Baada ya hapo nikaenda make-up. Kwenda huko walinipaka make-up ya uchafu! Kwa kweli ukiona picha zangu kwenye hiyo seti mini na wenzangu ni wachafu kweli kweli! Tulikuwa wachafu mpaka watu walituogopa! Tulikuwa wachafu maana tulikuwa tunalima shamba, na ilikuwa na matope shauri ya mvua! Udongo ulikuwa umejaa wadudu na minyoo wale wakubwa wakubwa (earthworms).

Halafu kulikuwa na farasi mkubwa kweli kweli! Alikuwa anaitwa Barney! Basi alikuwa anapita karibu sana kwangu lakini ali-behave. Tukaanza kuwa marafiki mpaka hapo walipoanza kufyatua marisasi na kaanza kushutuka! Ikabidi wamwondoe kwenye seti. Kaanza kutoka mapovu mdomoni kwa woga!

Niliumwa na mdudu kwenye mguu walimeta EMT (paramedic)! Fikiria walikujwa na huduma ya 911 hapo hapo! EMT’s wawili walikuwa assigned kule kwa shoot yote, pamoja na zimamoto na polisi!

Nitawajulisha zaidi...

5 comments:

  1. Bilashaka tutakuwa tukisubiri kwa hamu sana wengi wetu

    ReplyDelete
  2. Kwa kweli hii blogu imenivutia sana!Kuna mambo mengi ya kuvutia.Kuhusiana na hiyo filamu kwa kweli tunaisubiri kwa hamu.

    ReplyDelete
  3. Hongera Chemi kwa kupata nafasi kama hiyo.Fanya kweli na huo ndio uwe mwanzo wa kupata nafasi zingine.

    ReplyDelete
  4. Chemi hii maneno ya mafilamu-filamu mie naizimikia kweli. Ila umeniacha neno 'audition' ndio nini. kuuliza sio ujinga wajameni.

    Halafu tunza ahadi yako ya kutu-update whenever you feel we crave to know how 'Aftershock' goes on. kazi nzuri na ninakufagilia.

    ReplyDelete
  5. Kaka John,

    Samahani sana. 'Audition' ni kama vile interview ya kazi. Unaenda wanakuuliza maswali na kupima uwezo wako kuigiza. Unambiwa usome script sawa vile na kama uko kwenye stegi. Lakini wanakuwa wanajua wahusika kwenye mchezo ni akina nani na wanapima kama utafaa kuigiza moja wao au la. Wanapima utaonekanaje kwenye camera. Wanakupiga mapicha ukiwa unasoma, halafu wanazilinganisha na auditon za wengine.

    Mfano: Sinema ya ROOTS, Morgan Freeman, Kenan Thompson, Fred Williamson, na LeVar Burton wanafanya audition. Hapo anayefaa ni LeVar.

    Nitawajulisha Aftershock itaonyeshwa lini. Kuna Trailer tayari, ngoja nitafute linki.

    ReplyDelete