Thursday, December 07, 2006

Dar es Salaam kuna Joto!


Jamani Dar kuna joto! Loh! Unapigwa nayo ukishuka tu kwenye ndege. Siku mbili za mwanzo nilivyokuwa huko niliona joto kweli. Ni kweli kuwa Novemba/Desemba joto unazidi Dar, lakini kwa kweli nilikipata. Kwa siku nilikuwa na kunywa maji mengi kweli, na vinywaji vingine. Jamani nilitoka jasho zile siku za mwanzo.

Halafu mara nyingi umeme ulikatika kwa hiyo feni na Air Conditioning hazifanyi kazi, kwa hiyo unaendelea kuchemka. Unakwenda ofisini mwa mtu halafu unabakia kujipepea na gazeti shauri ya joto. Asubuhi, umeme ulikuwa unakatika saa 12 kamili. Basi unaamka kwa sababu feni chumbani unazimika na joto unaanza kuzidi. Hata hivyo siku zilivyopita nilianza kuzoea joto.

Haya nilivyondoka nilianza kusikia baridi kwenye ndege. Nilitamani ningebaki Bongo nifaidi joto. Na kufika Boston nilikaribishwa na snow (theluji)! Unatoka kwenye joto kuingia kwenye snow.

Basi nimerudi Boston na ka-tan. Nilikuwa navaa sleveless Dar, basi unaona kabisa mikono umekuwa Dark. Sehemu zilizokuwa zimefunikwa zilikuwa light. Wazungu kazini waliniuliza kama nimepata 'sunburn'. Nikawaambia hapana ni tan, na sisi weusi tunapata tan pia. Lakini wacha nifaidi hiyo Vitamin E ya jua, maana kipindi hiki cha winter jua unaliona tu. Mambo ya kukaa nje na mwili kuganda shauri ya baridi hatutaki.

13 comments:

  1. I'm Kortny,
    from Sri Lanka,
    and I'm 18 y.o

    Hi, Everybody
    I've studied English sinse Spring .
    It's so hard Language!
    I would like like to meet peple and practisice My English with them.

    Kiss!!

    ReplyDelete
  2. Hiyo ndio Bongo Dar es Salaam. Ndo maana miye najikalia Mbeya. Unitoe unipeleke wapi.

    ReplyDelete
  3. Business: The Economy Housing boom continues

    UK mortgage lending rose to its highest level in six years - further evidence of the strength of the housing market.
    Mortgage lending in June totalled ?11bn, up 21% compared to the previous month and 31% higher than the level one year ago.
    --------------





    ReplyDelete
  4. chemi!

    nyumbani ni nyumbani tu...

    ReplyDelete
  5. nasikitika sana hatukuonana ulipokuja. hata hivyo, i salute you, my dear sister kwa yote unayotupa...

    ReplyDelete
  6. mwaipopo umenisusa? nitembelee tu nkamu gwangu. siku hizi na-moderate for obvious reasons!

    ReplyDelete
  7. Michuzi,

    No problem, I will be back soon! I realize how much I missed Bongo! Will send you an e-mail!

    ReplyDelete
  8. Ndiyo Dar tulivyo, joto letu, mbu wetu, Kunguni, viroboto, chawa, ng'e wote tunaishi mnavyo. Mvua ikinyesha kidogo tuu, tabu! huendi dukani bila kuvua viatu, ukizubaa utakuta maji yameingia mpaka chumbani kwako, na bahati mbaya jirani yako ikiwa siku yake ya kuzibua choo, unalo.
    Simu ni nyingi sana, hata mwenye kipato cha USD3.00 kwa siku anamiliki simu na ana uwezo wa kuweka credit kila siku! mambo hayo. Usafiri ni kilekile mabasi yamekuwa mengi kwa idadi,unavijua vipanya, lakini uwezo wake wa kubeba abiria ni uleule iliyokuwa nao UDA miaka ya kati ya themanini huku Dar imekuwa mara tatu yake!.
    Jiji nalo halitaki kutanuka, zinakua townships tuu, lakini CBD ni ileile aliyoiacha mwingereza miaka 45 iliyopita, fikiria msongamano usio wa lazima ukiingia CBD! Hata masoko hayakui, bado watu wa maeneo yate ya Dar wanapendelea kununua bidhaa zao Kariakoo shimoni!. Machinga, kama unawajua, sasa kidogo wamepewa red card hawazagai sana kariakoo tumeonja mji usio na shughuli nyingi zisizo za lazima mjini.
    fikiria ukitembea barabara ya kibiashara hapo NY, barabara yenyewe ni kubwa na shughuli ni chache sana hata wachomoaji mifukoni,kama wapo, hawananafasi ya kukuchomolea. lakini huku kila uendapo unajihatarisha kuchomolewa au kupanguswa mdudu.
    Haya hayatoshi kuielezea Dar, lakini tulikuwa tayari kula majani ili raisi wetu apate ndege binafsi ya kisasa, ambayo tuliishia kubambikiwa, hatukujua kama kuna matumizi ya muhimu kama kununua mitambo ya kisasa ya kutengeneza umeme, ambayo sasa inatugharimu kiasi kikubwa kuliko tulichokataa miaka yote na bado hiyo mitambo siyo yetu!!!!. yote haya yanaendelea kwenye jiji liitwalo Dar ya wajanja wa kujanjiwa.... ............../

    ReplyDelete
  9. Kweli Bongo joto ndio hali halisi lakini ungekaa zaidi hata tusherehekee Christmas.
    Naomba ukija tena tuwasiliane: I want to know more about your film activities.
    Thanks.

    ReplyDelete
  10. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete