Friday, December 15, 2006

Niliuliwa na Mzungu mwenye Hasira (Aftershock:Beyond the Civil War)




Jamani msishangae sana. Huu ni mguu wangu! Na bado niko hai. Nilikuwa naigiza katika sinema ya 'Aftershock:Beyond the Civil War' kama Field Hand. Hao field Hands walikuwa ni watumwa walioachiwa huru lakini bado walikuwa wanaishi katika hali ya kitumwa baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe (Civil War) 1865. Wakati wa filiming tulikuwa peku kwenye matope! Sinema ilipigwa mwezi wa sita na wa saba hapa Massachusetts.

Hiyo make-up ya damu feki ilipakwa kwenye mguu baada ya kulala chini! Nakumbuka Director David Padrusch anamwambia make-up lady, ongeza, ongeza damu haitoshi! Ai! Walinipaka mwili mzima. Niliona kinyaa maana hiyo damu feki inaonekana kama damu kweli. Na usoni pia nilipakwa madamu na majeraha, ilikuwa tuonekana kama tumepigwa risasi nyingi. Ni kwamba weusi wengi waliuliwa na wazungu wenye hasira baada ya hiyo vita.

Sinema ya Aftershock itaonyeshwa History Channel, Saturday December 30, 3:00PM (Eastern).

Cheki website yao kwa maelezo zaidi.

http://www.history.com/shows.do?episodeId=203497&action=detail

Pia unaweza kusoma habari zaidi ya experience yangu kwenye seti ya Aftershock hapa:

http://chemiche.blogspot.com/2006_06_01_chemiche_archive.html

Unaweza kuona Trailer kwenye You Tube.

3 comments:

  1. Wala usiogope ndo maana ya kuigiza! Mimi mzima kabisa!

    ReplyDelete
  2. Ahsante sana Dada Che kwa habari hii. Mimi nafuatilia sana historia ya watumwa waliotoka huku Afrika na kutumikishwa huko Marekani. Mbali na sababu zingine nadhani hii ilikuwa ni mojawapo ya vita vya wenyewe kwa wenyewe. Hizi aftershock za civil war bila shaka ziliua watumwa wengi waliokombolewa licha ya kunyanyaswa na makundi kama Ku Klux Klan. Lakini nilifurahi kujua kwamba kulikuwa na wazungu ambao walikuwa against ukandamizaji huu, k.m. waanzilishi na operators wa "Underground Railway System" iliyosaidia kutorosha watumwa wengi kuelekea kaskazini. Nina hamu kubwa ya kutaja kujifunza maisha ya hawa wenzetu kwenye miaka hiyo. Tafadhali Dada Che tutumie habari zaidi kuhusu hili.

    ReplyDelete