Sunday, February 04, 2007

Huwezi kujua ajali itatokea lini

Ajali ni ajali. Hupangi itatokea lini au itatokea nini. Ukweli ukiamka huwezi kujua Mungu au shetani amekupangia nini siku hiyo.

Zaidi ya wiki mbili zilizopita nikiwa nakwenda kazini nilianguka kwenye ngazi za subway Central Square hapa Cambridge. Hata sikumbuki vizuri ilikuaje, sikuwa nakimbia wala kuwa na haraka, mwendo wa kawaida tu. Nilikuwa nateremka kwenda kwenye geti kusudi nisubiri treni. Ghalfla nilianguka, kwa bahati kuna ile sehemu pana ya katikati ndo nikaishia hapo na sikwenda chini kabisa. Ngazi zenyewe zimechongwa na mawe. Loh, magumu! Baada ya kuanguka nilishindwa kuinuka. Nikasema hayo ni malipo kwa ajili ya kucheka uile tangazo ya bi kizee akisema, “I’ve fallen and I can’t get up!) (nimeanguka na siwezi kuinuka), japo sijaiona miaka mingi. Mzungu mwanaume aliyekuwa anapanda zile ngazi alinisaidia kuinuka. Alivyokuwa ananinsaidia nikasikia maumivu makali kwenye mguu na kushindwa kutembea kabisa. Nikamwambia nadhani nimevunjika mguu. Huyo mzungu alipiga simu polisi, na polisi kaja, halafu wakaamua kuniitia ambulance.

Wale EMT (Emergency Medical Technicians) walinipakia kwenye kiti maalum ya wagonjwa na kunibeba mpaka kwenye stretcher barabarani ndo wakanipakia kwenye ambulance. Nikapelekwa hospitalini donidoni ikiwa inalia.

Basi mle ndani nikawa nalia. Niliamka mzima, sasa nimevunjika mguu! Nikawaza je, ningechelewa kidogo ningeanguka, je, ninegwahi kidogo ningeanguka? Je, nitakuwa mzima tena, je, nitaweza kucheza densi tena? Nikasema nina bahati lakini maana kuna wengine wanapata ajali ya gari na wanakufa. Au wanakatika kiungo. Fkiria mtu unaagana na mpenzi wako mtaonana au mtapigiana simu baada ya muda kadhaa, halafu simu inapigwa, mwenzako kapata ajali. Nilikuwa na mawzao mengi lakini nilishukuru kuwa sikumia kiasi cha kupoteza fahamu.

Hospitalini walinihudumia mara moja. Nilikuwa nimevaa suruali, walivyopandisha wakaona kuwa ngozi imechunwa kwenye gotii. Nilibakia kushangaa maana suruali haikuchanika. Baadaye walinipeleka X-ray. Bahati nzuri hakuna mfupa iliyovunjuika lakini nilikuwa nimeumia misuli tu kwenye goti. Wakanipa magongo, na madawa ya kupunguza maumivu na nikaenda zangu nyumbani kwa teksi. Nilikosa kazi siku mbili na bahati nzuri wikiendi ikaja. Nikapata nafasi nzuri ya kumpumzika. Baada ya hapo ikabidi nirudi kazini na magongo. Na mjue huko kwenye treni hakuna aliyenipisha kiti hata waliokaa viti maalum vya wagonjwa. Wengine wanakuaona halafu wanajidai wanasoma gazeti.

Lakini nashukuru sikuumia zaidi, na daktari kasema baada ya wiki kadhaa maumivu yatakwisha kabisa. Namshukuru Mungu kuwa sikuumia zaidi.

13 comments:

  1. ooh pole sana Chemi.tunamshukuru mungu hukuvunjika.naomba nikuulize kitu kidogo,ishu ya malipo ya huduma uliyopata ilikuwaje?nimesoma mfumo wa insurance wa marekani nikaona kuna hatari mtu akakosa huduma kama hayuko makini!

    ReplyDelete
  2. Hapa Massachusetts ukienda hospitalini ni lazima wakutibu. Ni sheria hiyo asante Gavana Dukakia miaka ya 80. Lakini kwa kweli kama huna bima, ni kazi maana wanaweza kukukalisha pale. Unaweza kupata huduma duni. Lakini watakutibu. Halafu dawa ni juu yako. Bahati nzuri napata bima kutoka kazini kwangu. Japo kuna co-pay lakini huduma inakuwa nzuri.

    ReplyDelete
  3. Pole sana da chemi naomba mungu akusaidie upone haraka

    ReplyDelete
  4. huo utaratibu ni mzuri.asante kwa jibu.get well soon!

    ReplyDelete
  5. Chemi,
    Pole na mungu akusaidie upone haraka.Nina tatizo moja tu kuhusu uandishi wako.Hauandiki kama mtu aliyewahi kufanya kazi kwenye taasisi ya habari kubwa kama DailyNews kwa miaka mingi namna hiyo.

    Pili ingawa blog ni kitu huru,cha mtu binafsi nadhani sio vibaya pia kama utawaacha wasomaji wako wakijifunza jambo.Kwa mfano kuumia kwako kungekuwa kumeenda na masuala ya bima kama alivyogusia Zemarcopolo,ungeweza kugusia mambo kama ya huduma ya EMT na ufanisi wake.Maoni tu

    ReplyDelete
  6. Kwa anonymous wa 8:15, asante kwa maoni yako. Hii ni blog hivyo naandika staili ya 'blogging' siyo staili ya kuandika kwenye gazeti. Kwa maana hiyo siwezi kusema kuwa ni Journalism. Of course kama ingekuwa article imeandikwa kwa ajili ya gazeti lazima ingebidi nifuatilie 'aspects' za EMT, Police Response, Insurance etc. Kwa hiyo naomba uchukulie maandishi hapa kama 'blog' na siyo gazeti.

    ReplyDelete
  7. Natuma pole zangu kwako, ila nimefurahia kitu kimoja ulichoandika Kuhusu Bima, mie nadhani hicho ni kitu muhimu sana ingawa wengi wetu huwa tunakipuuza. Tena, ugua pole!

    ReplyDelete
  8. Pole sana dada Chemi. Asante Mungu hujavunjika na unaendelea vizuri. Umenikumbusha ile story ya yule "subway hero" iliyotokea NY hivi karibuni.

    ReplyDelete
  9. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  10. Chemi,

    Habari za siku nyingi sana tangu enzi zile.

    Pole sana kwa aksidenti uliyopata na tushukuru Mungu kuwa hukuumia sana na umeshatengamaa. Hiyo ni sehemu ya maisha. Kuna wengine wanapoteza kabisa viungo vyao.

    ReplyDelete
  11. Chemi,
    Pole kwa shida hiyo ilokupata.
    Ushauri wangu: Hebu jaribu pia kujiangalia katika suala la uzito wa mwili, huwa linachangia kuzidisha maafa mtu anapoanguka. Pengine ungekuwa mwembamba ungeamka tu na kuendelea na shughuli zako. Ni ushauri tu, samahani, nothing personal!

    ReplyDelete
  12. Kwa anonymous wa 10:31AM, labda hukunielewa vizuri. Nilishindwa kuamka shauri ya maummivu kwenye mguu na goti siyo shauri ya unene. NIlidhani mguu umevunjika. Hizo ngazi zimetengenezwa na mawe. Nilipata 'trauma' kwenye mguu ndo maana nilishindwa kuinuka.

    ReplyDelete