Naona, kuna 'Anonymous' fulani kagusia hii swala ya yalionipata nikiwa jeshini JKT. Watu wengi wamenitumia e-mail kuulizia details. Nimeamua kuibandika tena. Ni posti ya kutoka April 2006. Lakini mjue enzi za JKT, wasichana wengi walinyanyaswa kijinsia, mimi nilikuwa na bahati maana nafahamu wasichana waliokuwa gang raped. Dada fulani, alimkubali afande, alivyomaliza kaita wenzake kwa kusema, "Njooni, Mboga hii hapa!" Yule dada hakuweza kutembea vizuri kama wmezi baada ya hapo!
*****************************************************************************
Nilipokuwa Jeshi ya Kujenga Taifa (JKT) karibu nibakwe na afande Fulani (jina nahifadhi). Lazima niseme kuwa katika kipindi hicho wanaume wengi waliona makambi ya JKT kama ‘buffet’ ya wasichana. Si maafande wa jeshi tu, bali hata viongozi wa serikali walikuwa wanapitia makambi ya JKT kula tani yao!
Mimi nilikuwa Masange JKT, Tabora. Wakati huo huyo jamaa alikuwa ni Kepiteni wa JKT. Nadhani alidhania kwa vile yeye ni kepiteni basi alikuwa na haki ya kutembea na yeyote aliyemtaka. Kwangu aligonga ukuta! Bila shaka alikuwa hajawahi ‘kunyimwa’ mpaka siku hiyo alipokutana na mimi.
Miaka baada ya tukio nikiwa nafanya kazi Daily News mara nyingi nilikuwa napishana naye Posta Mpya. Basi ananisemesha, na mimi namnunia halafu napita zangu kimya bila kumjibu kwa hasira. Siku moja kanisimamisha kaniambia, "Chemi, naomba msamaha, nisemahe tafadhali, kweli nilikukosea!” Aliongeza kuwa miaka mingi imepita hivyo sina sababu ya kuwa na hasira naye! Na mimi nilimjibu, “Mshenzi sana wewe!” nikaenda zangu.
Ikapita kama mwaka mwiingine. Jamaa anaendelea kunisalimia kila nikimpita njiani na mimi kwa uchungu bado nikashindwa kusema kitu. Basi nikafikiria alichoniambia Posta Mpya. Lakini niliona kama jambo hilo linamsumbua. Na nikasema kama Bwana Yesu aliweza kusamehe watu kwa madhambi yao kwa nini mimi nisimsamehe. Basi baada ya hapo ikiwa nikimwona na akinisalimia naitika na naendelea zangu na nikaona kidogo hata yeye alikuwa na raha.
Lakini bado najiuliza kama kitendo chake kilimsumbua miaka na miaka kama ilivyonisumbua mimi.Unauliza ilikuaje mpaka nikajikuta kwenye situation ya kubakwa. Au mnasema nilitaka mwenyewe. Ngoja niwaelezee ilivyokuwa.
Nilikuwa mhudumu Officer’s Mess, mpishi na msafishaji. Huyo jamaa alikuwa ni mgeni kutoka Makao Makuu ya JKT Dar es Salaam. Kwa kweli sikutaka kufanya kazi pale Mess lakini tulichaguliwa special na Matron, mimi kwa vile niijua kupika vyakula mbalimbali hasa za kizungu. Lakini uzuri wa hiyo kazi ni kuwa uanambulia mabaki ya vyakula (leftovers), na mara nyingine kulikuwa hakuna.
Basi huyo Afande alikaa kambini wiki kadhaa. Katika kumhudumia tukawa tunaongea na mimi nikawa namheshimu kama kaka vile. Wala sikusikia mapenzi yoyote kwake. Basi jioni fulani, kanialika chumbani kwake kunywa soda na biskuti na kwa Maongezi zaidi. Sasa kama ulienda jeshi unajua njaa kali unayokuwa nayo. Nikaenda, kanikaribisha vizuri, nilipewa soda na tukawa tunaongea. Basi nikaona mwenzangu anabadilika ghafla! Mara ananikumbatia kwa nguvu, na kunibusu na mengine. Nikajaribu kuaga lakini jamaa hakuniachia. Baada ya ku-plead naye aniachie, kaniachia. Kaomba msamaha na kaniomba niendelee kukaa nimalize hizo soda alizoninulia.
Kama mjinga nikamwamini, nikakaa nakunywa hizo soda. Tukaendelea na Maongezi, kukaa kidogo huyo kanirukia, najaribu kusimama huyo, kanivuta na kuniangusha kitandani! Mimi saa hizo nikawa naogopa kabisa nia yake!Kaniambia eti, “ukipiga makelele najua nitasema nini! Nyamaza! Huna sababu ya kunikatalia!” LOH! Kanizaba kibao! Nikamwuliza kwa nini anaifanyia hivyo, na mimi nilikuwa namwona kama kaka yangu!Hapo sasa ikaniingia. Nabakwa! Loh!
Nilimpiga mangumi na mateke lakini jamaa alikuwa na nguvu huyo kachana chupi yangu! Baada ya hapo, jamaa kashika miguu yangu huko anafoka kwa sauti kama vile anatoa amri “panua miguu! PANUA MIGUU!” Huko katoa ume wake uliyosimama kwenye suruali! Basi kuona sipanui jamaa kaongeza makofi na kafanikiwa kupanua miguu yangu! Kuona kafanikiwa kupanua huyo kajaribu kupenya. Ilipogusa kwangu nilipiga kelele cha kufa! Nikasema, “Nakuufaaaa!”
Heh! Ghafla jamaa kaniachia kaniambia niende. Alisema, “Nimeigusa na ume wangu, unatosha!” Nenda zako! Na ukimwambia mtu najua nitasema nini!”Loh nilikimbia bwenini na giza lile la Masange huko nalia. Wenzangu wananiuliza vipi, nikashindwa niseme nini! Kwanza niliona haya! Fikiria, niliona haya (shame)!Kesho yake nikaenda dispensary na kujiandikisha mgonjwa. Sikwenda kazini Officer's Mess bali nililala bwenini.
Siku iliyofuatia huyo Afande mshenzi kapita bwenini kwetu kaulizia hali yangu, na mimi huko natetemeka kwa woga nikashindwa niseme nini. Alininunulia Orange squash na biskuti na kuzileta bwenini. Sitasahau alivyonitazama! Ilikuwa kama vile anapanga jinsi gani atanipata. Baada ya hapo alimwopoa msichana mwingine na huyo alimkubali kabisa. Akawa analala kabisa huko Officer’s Mess. Hakuna anayemsumbua wakijua ni bibi wa Afisa. Basi, siku za yule jamaa kukaa kambini zikaisha, na yule binti alienda naye Tabora mjini kwa siku kadhaa. Halafu jamaa karudi zake DSM. Yule binti karudi zake kambini! Kumbe alienda bila pass. Alidhania kwa vile yuko na mkubwa hana haja ya pass. Na yule Afande ndo kaondoka kimoja! Maafande waliobakia wacha wamtese huyo binti alivyorudi kambini! Walimtesa kwa Extra drill na mengine mpaka ikabidi Military Police waombe wakuu wamsamehe la sivyo atakufa. Raha yake iliishia kwa suluba! Sijui yule binti alidhania jamaa atamwoa! Kwa nini alimkubali yule mshenzi.
Anyway, kila mtu na vyake. Alivyotoka kwenye suluba tulimwuguza! Siku haizkupita na mimi nilitolewa kazi Officer’s Mess na kupelekwa kwenye kikosi cha Ujenzi na lazima nisema hapo nilifurahi sana. Basi miaka ilipita. Mimi nilikuwa mwandishi wa habari Daily News, tena nilijenga jina. Sasa nikawa napishana na yule jamaa huko kapandishwa cheo na yuko JWTZ. Jamaa anajaribu kunisalimia na mimi napita zangu kimya, namnunia kabisa.
Nilimwona mshenzi, mnyama, na kila kitu kibaya ndo ilikuwa yeye! Angefanikiwa kuingiza na kunimwagia uchafu wake ningejiona mchafu mpaka leo! Miaka kama 20 imepita sasa na bado nina uchungu naye.Jamani nyie wanaume nawaambia kubaka kinaathari zake kwa wanawake. Unataka raha ya dakika na unamwachia mwenzio na uchungu wa maisha! Wengine mpaka wanakuwa wagonjwa wa akili.
Kwa nini nimeamua kuzungumzia kubakwa kwangu hapa, ni kwa sababu naona wasichana wengi wanabakwa, halafu wanaamua kunyamaza kimya. Kisa wakienda polisi na hospitali wanahofia kuambiwa ni Malaya au walitaka wenyewe! Hata mwamanke mwenzako anaweza kukufokea kuwa ulitaka mwenyewe. Tanzania, wanaume walikuwa na usemi wao kuhusu wanawake na ngono. Walisema eti ukimwomba mwanamke halafu akijibu ndiyo, manake ndiyo atafanya. Akisema labda, manake atafanya, akisema hapana, manake hapana. Lakini jamani tendo si inakuwa tamu kama wote mmekubali? Na kama angefanikiwa kuingiza si angeniumiza sana!
Wengine wanasema ningemshitaki. Je, ningemshitaki ingekuaje? Kwanza jeshini mimi ningepewa Extra Drill mpaka niumie au kufungwa jela ya jeshi iliyojaa maji na mbu kusudi niteswe. Kumbuka ilikuwa Tanzania na yule alikuwa ni Kepiteni wakati huo na mimi nilikuwa Private. Hakuna ambaye angekuwa tayari kunisikia zaidi ya wenzangu maPrivate, na yeye alijua hivyo. SHENZI TAIPU!
pole sana dada Chemi, yaani wanawake wote duniani wangekuwa na ujasiri wa namna hiyo basi wasingenyanyasika na tena wangeogopwa. lakini wengi huwa wepesi wa kuogopa na kumsabilia mwanamme kwa kile anachokitaka.
ReplyDeletemungu alokuvua hilo atakuvua na jengine (ameen)
Chemi, ni kweli wewe ni mwandishi na pengine ni vizuri kuwa muwazi lakini kuna wakati hakuna haja ya kuandika mambo kama haya maana kuna wanao amini na wengine hawata amini kama kweli hukubakwa (maana point huyu jamaa aliyofikia kutoingiza mmmh question mark)
ReplyDeleteAnyway usijali ni maoni yangu one does not have to tell the world her/his private adventures good or bad. Naandika hivi kwasababu nimeona impact yake wakati ulipo weka habari ya waziri wa Liberia kuna mtu katumia hii issue somehow kushusha dignity yako all the same kipenda roho.....
Anonymous was 6:31AM, asante kwa maoni yako. Nilvyoandika ni ukweli na ndo ilivyokuwa. Jamaa hakuingiza, namshukuru Mungu, labda yule Afande alivyojua kuwa kweli sitaki, maana nadhani alikuwa amezoea kupewa kwa ajili ya cheo chake. Kuhusu watu na maoni yao, watasema mengi, si unajua sisi waswahili tulivyo, umbea hauishi.
ReplyDeleteNa Anonymous was 4:39am asante pia. Sisi wanawake tunafudishwa kuwa wapole na ku-treat wanaume kama vile wako juu yetu. Lakini nasema hapana, kuna usawa. Napenda ule usemi wa kizungu na wa Women's Lib, "ANYTHING YOU CAN DO I CAN DO BETTER!"
We Chemi ulikuwa Kuruta au Service(wo)man SIO Private!!!!
ReplyDeletePole sana mwana-'serengeti' kwa kuponea chupuchupu kubakwa! Unajua kwa umbile kama lako msichana ukivaa bukta yenye kubana mapajani+ T-shirt iliyoshika matiti vizuri, mwanaume yeyote ni lazima asisimkwe! Ila wenye busara hujizuia ashiki au hamu zao zisionekane wazi!!! Kwa hiyo huyo ofisa alikosa busara za kujizuia (siwezi kumlaumu kwa kukutamani ila namlaumu kwa kushindwa kuji-control.. na hilo ni kosa!)
Kule O/Mess ni mbali kidogo na pamejitenga ila sajent's mess pako njiani kuelekea kisimani na ni karibu na ofisi ya CO na mwembe mawazo.
Ilikuwa OP. gani hiyo, mie nilikuwa masange op. kambarage, (Chale Coy)tulikula viazi sana vya kalunde wakati wa kufyatua & kuchoma matofali, magogo ya kuchoma tumbaku na mashamba mahindi ya embakasi, zimbabwe + ujenzi wa nyumba za maafande! Kuokota kuni porini, na kilimo cha bustani hizo ni baadhi ya kazi za masange.
Nakumbuka kulikuwa na kisima cha wasichana na wavulana kwa ajili ya kuoga mchana!
Niliwahi kutoroka kwenda Dar kwa ajili ya ku-process application za vyuo vya juu, niliporudi ilikuwa kasheshe!!!!!!
Kwa Anonymous wa 3:13am, asante kwa maoni yako. Umenikumbusha mbali. Nilikuwa kwenye Opresheni Nguvu Kazi. Na asante kwa kunisahisha. Nilikuwa Servicewoman. Tabora Girls ndo nilikuwa naitwa Private. Nilikuwa A Company halafu baada ya kutolewa Officer's Mess nilienda Headquarters Company mpaka nilimaliza.
ReplyDeleteMasange kulikuwa na visima vingi, lakini mbali na mabweni. Kuoga huko wakati mwingine ilikuwa lazima. Kuna siku niliwahi kuanguka ndani ya kisima, na kushindwa kutoka. Niliokolewa na Afande fulani (No strings attached).
Ulisikia mkasa wa akina Mwangupile? Nilimtafuta nikiwa Dar, Novemba lakini sikumpata. Nitasimulia kuhusu hiyo ajali hivi karibuni.
Chemi, unalaumu wadada wanabakwa na hawasemi, wewe mbona hukusema ulipokuwa mdogo, umesubiri umekua, na umesemea kwa blog, na bado mhusika umehifadhi jina, huna ujumbe wa ujasiri wa kuwabeza wanaobakwa.
ReplyDeleteAnonymous wa 11:27AM, asante kwa maoni yako. Si kweli kuwa nilinyamaza. Kuna watu niliwaambia, lakini kumbuka enzi hizo nisingeweza kwenda polisi. Na maMP wangenipa suluba na kilema cha maisha. Ndo maana nilisema yule jamaa alitumia cheo chake kuonea wasichana.
ReplyDeleteHata hivyo watu watanyamaza wakijua watambiwa walitaka wenyewe na kuitwa malaya. Hebu ona maoni hapa na kwenye original posti, watu wanasema nilijipeleka hivyo shauri zangu.
Nami nasema wasichana wafundishwe Self Defense ili waweze kukabiliana na wanaume washenzi kama huyo!
Chemi, mie ndo anoni wa 11:27AM, nilidondoka hapa baada ya kuletwa na link ya Michuzi, si unajua kule tuna analyse mambo haraka haraka na kutoa comment chap chap kunogesha umma. Nimetoa coment hapa, umeijibu wewe mwenyewe rasmi. Kwa Michuzi, huwa anajibu burning issues pekee, unaweza elewa tonnes za maoni kule. Ok, I respect you, I respect your work and your opinion, sikuwa nimejua ni mwanamke wa shoka haswa. Greetings and wish you a happy life (kwa familia yako pia). Nimefatilia uandishi wako, ni mzuri actually kusema ukweli. Once again, believ in your opinions, na Molla akujaalie. LOVE.
ReplyDeleteAnonymous wa 11:27AM/2:26, nasema asante tena. Naona itabidi niandike piece nyingine. Ujue nilikuwa na hasira sana na wanaume baada ya hiyo tukio. Wanaume ndo walikuwa wakubwa wa vyombo vya habari na sehemu nyingi wakati huu na kazi kulindana. Wanawake tulikandamizwa sana, na mimi niliyedhiriki kusema nilipata shida sana, na hata kupigwa shauri ya kutaka haki zangu kama mwanamke na kama bindamu. Bora mambo yamebadilika siku hizi.
ReplyDeleteNasema tena, asante kwa mchango wako na maoni yako.
Che Mponda umenikuna! Nashukuru sana kwa ujasiri wa kutoa facts za yaliyokusibu, Naamini Mungu amekupa ili kutoa fundisho au changamoto kwa wadada waliokumbwa au kunusurika na janga kama hilo. Mimi naamini kabisa kwamba huyo Afande hakufanikiwa kukuingilia kama ulivyosema vinginevyo najua ungekuwa muwazi na kutuambia after all we are talking about past. Wasioamini shauri yao kikubwa ni fundisho tunalolipata katika tukio kama lile. Bibie hujachelewa sana kutoa hii story , ni muda muafaka maana kuna kundi kubwa sana la wasichana linahitaji bado kujifunza. Nikupe pole kwanza kwa mkasa na pia Hongera kwa kazi nzuri ya kujilinda. Umenifurahisha kwa maoni yako kwamba ni vizuri wasichana wafundishwe self defence waweze kukabiliana na wanaume wasioweza kujizuia .Kitendo cha kumsamehe huyo Afande ni cha kiungwana kabisa, Jamani tujifunze kusamehe tukiombwa kufanya hivyo haijalishi ni kosa gani (This is my opinion).
ReplyDeleteNapendekeza utoe nafasi pia ya wakinadada waliokumbwa na mkasa kama wako kuandika yaliyowapata na mazingira ya tukio ili kutoa elimu zaidi kwa wengine ili kuepuka /kuwa makini zaidi wanapoona dalili au mazingira nayoashiria kubaka.
Mimi binafsi nilishawahi kunusurika katika matukio mawili ya ubakaji tena na watu ambao ninawaheshimu sana na walikuwa kama walezi wangu.
Nipo tayari kutoa hizo facts na naamini zitakuwa na mchango mkubwa kwa wasichana wengi walio kwenye hatari hiyo.
Nikirudi kwenye enzi ya JKT kwa kweli story za huko zilikuwa kabambe ukianzisha different topics nafikiri wengi watakuwa na mchango mkubwa katika mambo mbalimbali ukiachilia mbali hilo la ubakaji, kuna mazuri mengi ambayo tulijifunza enzi hizo na kwa kweli sijutii kupitia JKT!
Chemi wadada wa kichagga lazima utumie nguvu sasa...
ReplyDeleteAnonymous wa 6:14PM, asante sana kwa mchango wako. kwa kweli kama kungekuwa na National Referandum kuhusu mambo yaliotokea JKT yangesemwa mengi. Tena kuna watu waliokuwa viongozi wa taifa waliohusika pia. Kuna stories nyingi sana na najua kuwa kuna watu wameamua kusahau au kutongelea kabisa.
ReplyDeleteKuna msichana tuliyekuwa naye pale Masange aliharibiwa kizazi huko JKT! Kuna wengine walipata minba za maafande. Acha tu. Najua watu watasema kuwa JKT hakuna tena na tuisahau, lakini jamani watu walipata shida.
Kweli Chemi umekutana na mengi, na wanawake kama wewe wengi hukata tamaa yaani kutomwitaji mwanamme kwani wanaona karibu wote ni wakatili. Ila sina uhakika na hili labda una familia.
ReplyDeleteKwa kweli bora JKT ilikufa kwani maambukizi ya ukimwi toka kwa maafande tena uchwara yangelitumaliza kwani wenyewe walikuwa wanashindana nani katembea na service-woman wengi. Lakini nafikiri mfano wako uwe fundisho kwa wanawake wengine kwani nao walikuwa wanachangia hasa kujirahisisha kwa maafande ili wapewe favor.
Anonymous wa 7:16AM, asante kwa maoni yako. Ni kweli kulikuwa na maafande waiokuwa wanashindana na hao walikuwa maofisa. Kuna siku kuna dada moja alijirahisisha kwa afande fulani, basi kazi yake tulipewa kumfanyia. Kulima miraba mirefu. Mimi nililamika. Heh! Huyo afande si aliniita kuniuliza kama ni kweli nililalamika. Nikasema, ni kweli nililalmika. Wacha nipewe adhabu!
ReplyDeleteKuhusu maafande kuudedi na mdudu, nasikia wengi walishaaga dunia shauri hiyo.
Chemi acha story,afande alikua ameshakojoa na akaona akuteme utambae na issue zako.Inaonekana ulikua bomba sana kwa kushika tu mapajani inatosha kukojoa.
ReplyDeleteKwa anonymous wa 3:19PM, huyo Afande alikuwa bado hajafikia stage hiyo labda baadaye alijifurahisa mwenyewe...mimi nilishakimbia! Mbio niliyotoka nayo pale ningeweza kushinda na mkimbiaji Michael Johnson! Kwa kweli angenichafua ingekuwa mbaya, maana nisingemsamehe kabisa! Akae na uchafu wake! Nataka kutapika nikikumbuka...Loh!
ReplyDeleteLile halikuwa jeshi ilikuwa ni "Forced labour".Ni kitu kimoja kilicholitia aibu taifa kama sehemu ya uvunjaji mkubwa wa haki za binadamu ambapo Binadamu alilazimishwa kujiunga na jeshi bila hiari na kutumikishwa kama punda bila ujira wowote akiishi katika mazingira duni ya kutisha.
ReplyDeleteNi kitu ambacho hakiwezi rudiwa tena.Si tu usamehe huyo askari bali pia isamehe serikali na nchi iliyobuni hapo zamani vitu vya kutesa watu kama hivyo.
Dada Chemi Pole sana.I feel like crying.It is a sad, true story
ambayo imewatokea wengi.Pole dada Chemi.Pole sana dadangu.I feel your pains.
Koloboi@yahoo.com
Dear Anonynous wa 5:55AM, asante sana kwa mchango wako. Umesema kweli yale makambi yalikuwa ni 'Forced Labour' camps. Nililima sana, na nilijenga majumba na tulilima tumbaku na nani alinufaika? Nilijifunza mengi jeshini, lakini kwa kweli yalikuwa ni makambi ya suluba.
ReplyDeleteUkifikiria, maafande wengi walikuwa wamishia darasa la saba. Hivyo 'wasomi' walikuwa wanaonewa kwa vile maafande walikuwa na wivu. Pia walizuia matumizi ya kiingereza kwa service people kwa vile waliona kuwa wanatukanwa na hawelewi wanasema nini.
Ulisikia ile joke ya afande mshamba:
Kuruta: Afande, leo siwezi kula kwa vile sina 'appetite';.
Afande: Mwombe Juma akuazime yakwake!
HIvi Chemi una familia au bado?
ReplyDeleteAnonymous wa 8:16AM, kama unauliza kama nimeolewa jibu ni ndio.
ReplyDeletethe next question umeolewa lini
ReplyDeletena je huyo mumeo anakutunza vizuri maana naona umebadilika...kama hakutunzi basi tuko radhi kukuchukua nduguzo
http://videozamatusi.blogspot.com/
Na wewe Matusi maswali mengi kweli. Nimecheki hiyo blogu yako, karibu nipofuke!
ReplyDeleteUnapoongelewa suala la ndoa kila mtu anakuwa makini awe mlokole au kafiri kwani biolojia haina hayo. watu wanaposema tendo la ndoa wanamaanisha kuingiliana kimwili a.k.a kufayana, mikasi, kukazana, kupigana miti, kurushana roho, kupungana na lile ambalo ni hash zaidi ambalo nakumbuka nikiwa mtoto ukitamka mbele ya wakubwa unachapwa viboko kuwa umetukana ni KUTOMBANA. Ila nina swali je na mashoga ambao siku hizi nao wanaoana tuite vipi tendo kulana migongo, yuite pia tendo la ndoa?, jibu hapana. Tendo la ndoa ni mwanaume kumuingilia mwanamke, na hii ni kwa sababu ukisema kutomba au kutombwa inadhalilisha jinsia moja ya kike na kukwaza ya kiume, kutombana pia lina utusi, basi kuondoa utusi ndio tunasema tendo la ndoa, kwani dhumuni kubwa la kuoana ni kufanya hilo tena. Sasa basi kama tendo hilo linafanywa na wasio katika ndoa, bado maana inakuwa ile ile wanafanya tendo la ndoa.
ReplyDeleteNa mzee wa MATUSI blog yako poa sana naifagilia kwani tendo hili ni sanaa, usipojua kulicheza utakimbiwa, ila du sanaa hii inataka wehu ili uweze kuimudu, maana yale mambo si ya kitoto ni mambo ya mtu kukimbia akaacha chupi..., rigwaride rimemshinda
Pole Chemi, ujasiri wako utasaidia wasichana na wanawake wengi waliokumbwa na janga hilo la kubakwa. Mara nyingi watu wakipatwa na majanga hujiwekea wenyewe kwa hiyo umma haufaidiki. Kwa kushiriki hapa unajisaidia mwenyewe pamoja na dada zetu. Asante sana.
ReplyDeleteMsafiri Musa
Hongera kwa kwa kuonyesha ujasiri,na kusaidia jamii,mimi naitwa LUGEYE ADOLPH MWANASELE,nilikuwa op miaka 40,ni hivi karibuni tu,mwaka 2002-2008,mimi pia ni mhanga wa tatizo kama lako ila mimi sikutaka kubakwa kama wewe ila nilifukuzwa jeshini pale katika kambi ya STONE QUARRY KUNDUCHI JKT kwa sababu kama ulizozitaja wewe kuwa Afande kutumia cheo chake kunyanyasa watu hasa sie ambao hatutoki familia za maafande,yule afande alikuwa anaitwa afande BAZICHA alikuwa na nyota 2 tu,akishirikiana na kibaraka wake afande MAHELA yeye alikuwa ni staff sajenti,kitu alichoamua kunifanyia mazingira ya kukatishiwa mkataba wangu ni baada ya mimi kua nakataa sera zake za unyonyaji hasa pale alipokuwa anataka sisi service man tukamfulie nguo zake mpaka mashuka yake,na wakati huo utaratibu haupo jeshini inatakiwa anitume kazi za kijeshi hapo kambinilakini sao kwenda nyumbani kwake kumfulia nguo,sasa mimi nilipokuwa nawaeleza vijana wenzangu kuwa mnaonewa yeye akaamua kuweka chuki na mimi akaniundia zengwe kwa CO wakaamua kunisitshia mkataba wangu mm peke yangu,na wakati tulikuwa tumebakisha miezi 2 tu tuajiriwe kweli wenzangu waliajiriwa kasoro mimi tu,ila namshukuru Mungu baada ya kurudi nyumbani nikapata mfadhili wa kunilipia ada ya chuo kwa sasa nasomea ACCOUNTANCY CBE, kitu ambacho napenda kuwashauri Serikali yangu sikivu ni kwamba kuanzia mwaka kesho nimesikia wanafunzi wanaomaliza form six wanaenda jeshini kwa mujibu wa sheria,serikali iwe makini sana na hao watoto wa watu dhidiya maafande wenye tamaa ya ngono,na tukizingatia 75%ya maafande ni waathirika wa HIV,naogopa badala ya kupata tulichokitarajia vijana wakakamavu tukajikuta tunatengeneza Taifa la waathirika wa ukimwi na kama tunavyojua watoto wa siku hizi wanaaanza hayo mambo ya ngono mapema!tuwe makini sana hata ukiangalia zamani waliokuwa wanamaliza form six walikua kidogo ni vijana wakubwa wameshakomaa kiakili lakini watoto wa siku hizi wanamaliza form six bado vitoto kabisa naomba serikali iandae mazingira mazuri kwa hao vijana wanaotegemewa kuingia jeshini mwaka kesho.
ReplyDelete