Monday, May 07, 2007

Ajali ya Ndege ya Kenya Airways














Photos from:
Usiku wa kuamkia jumamosi May 5, 2007, ndege ya Kenya Airways ilianguka huko Cameroon, mara tu baada ya kutake-off kwenye uwanja wa ndege ya mji mkuu wa nchi hiyo Douala. Lakini ilichukua masaa 40 kuona ndege ilianguka wapi. Ajabu zaidi, huko Cameroon sijui hawakujua ndege imeanguka. Watu walienda kwenye airport Nairobi na ndege haikuonekana! Ilikuwa itue Nairobi saa 12 asubuhi. Kwneye hiyo ndege kulikuwa na abiria 115 kutoka nchi 23 na mmoja alikuwa MTanzania.

Hapa kazini kwangu wazungu wanasema, ehe mnaona huko Africa ni Bush/Jungle mpaka wanashindwa kujua ndege imanguka wapi. Japo comments inchukiza lakini ni kweli kwa nini ilichukuwa muda wote huo kuona mabaki ya hiyo ndege. Na kama mtu aliponea, huenda alikufa akingojea waokozi! Africa ina sifa mbaya sana kwenye suala ya usafiri wa ndege.

Hata hivyo, nimesisitiza kwa hao wazungu kuwa Kenya Airways ni airline nzuri hawatumii zile ndege za kirusi za zamani, bali wanatumia ndege za kisasa. Hata hiyo ndege iuliyoanguka ilikuwa mpya maana ilikuwa na miezi sita tu.

Na tusisahau kuwa miaka sita iliyopita ndege ya Kenya Airways, ilianguka huko Abidjan, Ivory Coast. Katika ajali hiyo watu kumi kati ya 169, waliponea.

Kwenye hii ajali nchi za France, South Africa, Kenya na Marekani walituma watu kwenda kusaidia kutafuta mabaki ya hiyo ndege. Jamani, Cameroon enyewe imeshindwa kuona ndege iliyoanguka kilomita 20 kutoka mji mkuu wao. DOH!

Na kwa sababu ya joto, maiti na mabaki ya abiria waliokuwemo kwenye hiyo ndege zimeanza kuoza. Wanasema kuwa hata wakipata maiti ambayo ni nzima, wakinyanyua inadondoka vipande!

MUNGU AWALAZE MAHALI PEMA MBINGHUNI. AMEN/AMIN.

Kwa wanaotafuta habari zaidi:

Kenya Airways advised relatives seeking information to call +271 12071100, which is an international line, and 3200353, 3200354, 3274349.
Stories zinazohusiana na hii ajali:

http://allafrica.com/stories/200705070649.html
Majina ya Crew ya Ndege hiyo:
• Wamwea Francis Mbatia - Captain • Wanyoike Andrew Kiuru - First Officer • Kiiru Phylis Njeri - Flight Purser • Njoroge Allan Njenga - Flight Attendant • Nyakweba Lydia Mocheche - Flight Attendant • Ong’ondo Elizabeth Achieng - Flight Attendant • Wakhu Shantaben Niriza - Flight Attendant • Kadurenge Cyprian Mande - Flight Attendant • Kisilu William Muia - Flight Engineer

5 comments:

  1. Wee Chemi una kasumba ya majina ya Kiingereza, ina maana hujui kuwa France ni Ufaransa?
    Halafu unashangaza mno kustaabu kwa nini ndege hiyo haikuonekana - sijui ni tatizo la shule au nini? Wewe unajua Kameruni ina misitu ya aina gani? Unafahamu mabwawa yenye uoto wa mimea yalivyo? Unajua kwamba ndege hiyo ilianguka usiku? Unajua kwamba haikulipuka kiasi cha moto au moshi kuonekana mbali? Unajua kwamba Uwanja wa Ndege ule uko pembezoni mwa mji na kwamba mwendo wa ndege wa dakika 13 unatosha kuifikisha kwenye msitu mnene? Unafahamu kwamba ndege hupatikana mapema iwapo kirusha mawasiliano chake hakikuharibika ambacho huweza kukaa saa 48? Umeonesha ungumbaru kuiponda Kameruni. Waambie hao Wazungu wako kwenye nursing home kwamba hata ile ndege iliyoanguka Septemba 11 kule PA nayo ilipotolea msituni.

    ReplyDelete
  2. Kwa anonymous wa 8:23PM, hiyo ndege Flight 93, iliyoanguka Pennsylavania ilionekana mara moja.

    Mambo yote uliyoelezea kuhusu kuanguka kwa hiyo ndege nilijua. Na nikweli nimewaponda waCameroon, maana najua ndege ingeanguka Tanzania tungeiona baada ya muda mfupi si baada ya masaa 40. Ni aibu!

    Lakini Boeing wamesema kuwa hiyo ndege ilikuwa na alert system ambayo ilitakiwa ifanye kazi siku mbili. Lakini iliacha baada ya dakika. Tutasikia uchunguzi unasemaje.

    ReplyDelete
  3. Nimekutolea mfano wa ndege ya Pennsylvania ili upate cha kuwajibu wazungu wako kwamba hata hapa kuna misitu, siyo suala la kuonekana mapema, elewa mama. Iwapo ndege ingeanguka kwenye misitu mikubwa kwenye nchi yeyote kazi ya kuipata ingekuwa ngumu. Tanzania hatuna misitu kama ya Kameruni. Jiografia mama hiyo.

    ReplyDelete
  4. Kweli sijui kama mmesha ona heavy forest, basi Cameroon, the two Congos...Central Afrika,..hiyo misitu ipo, Tanzania tuna savana not forests.

    Maoni yangu hata kama hiyo ndege wangeiona haraka there was no hope ya kukuta walio hai it seems every thing went so fast! Only God knows why/when and how things happened.

    Mungu awepe nguvu families zinazo husika kwa hili pigo kubwa!

    One's destination is in God's hands!

    ReplyDelete
  5. waridi,

    Sijakataa kuwa Cameroon kuna misitu/jungle.

    Kwa kweli suala la kutoana hiyo ndege pia lazima isumbue hao ndege manufacturers BOEING! Yaani hakuna emitter wala beacon iliyoweza kutoa ishara ndgee ilianguka wapi! Ndege eneyewe iko labelled ULTRA-MODERN!

    Lakini tusisahau, hata meli ya Titanic ilizama wakati walisema ni ULTRA-Modern kwa wakati huo 1912.

    ReplyDelete