Saturday, May 05, 2007

Ndege ya Kenya Airways imeanguka huko Cameroon!




Ndugu wa abiria huko Kenyatta Aiport Nairobi.



Kuna habari kuwa ndege ya Kenya Airways enye abiria 115, imeanguka huko Cameroon. Ilikuwa inatoka Ivory Coast (Cote d'Ivoire) kwenda Nairobi lakini ilipitia Cameroon kuchukua abiria wengine. Mungu awalaze marehemu wote mahali pema mbinguni. AMEN/AMIN.

****************************

NAIROBI, Kenya (AP) -- Kenya Airways has lost contact with a commercial airliner carrying more than 100 passengers that took off from Cameroon early Saturday, the airline said.

"The last message was received in Douala after takeoff and thereafter the tower was unable to contact the plane," Kenya Airways CEO Titus Naikuni said Saturday.

The Boeing 737-800 was carrying 106 passengers, eight crew members and a flight engineer, he said. The plane is capable of carrying 189 passengers.

"We have no details about what has happened to the aircraft," Naikuni said.The flight departed Douala at 12:05 a.m. and was to arrive in Nairobi at 6:15 a.m. The flight originated in Ivory Coast but stopped in Cameroon to pick up more passengers, the airline said.

The airline opened a crisis management center near the airport. Relatives of those on the plane were instructed to go to a downtown airport, where they would be provided information as it became available.

The last crash of an international Kenya Airways flight was on Jan. 30, 2000, when Flight 431 was taking off from Abidjian, Ivory Coast, on its way to Nairobi. Investigators blamed a faulty alarm and pilot error for that crash, which killed 169 people.

6 comments:

  1. dada che habari gani sasa hapao kwenye hiyo habari unanichekesha unaposema mungu awalaze mahali pema mbinguni hivi ni kweli kwamba mtu akifa anaenda mbinguni kama ni kweli watu wakifa wanaenda mbinguni ni wapi huko umeipata hiyo fact nasema hivyo sababu nafahamu mtu akifa amekufa tu na anakuwa konshas of nothing sasa sijui huko mbinguni wankuwa ktk state gani mortal au immortal?
    lakaini nakuunga mkono tuowaombee hao ndugu wa marehemu ili mungu awape kareji na strength ktk wakati huu mgumu

    ReplyDelete
  2. anonoymous wa 5:23AM, sijui hata nisemeje maana watu wana imani tofauti. Hapa kuna watu wanasema ukifa ndo basi tena, unaoza na kuwa vumbi. Wanasema hakuna cha motoni wala mbinguni. Wengine wanasema ukifa kama ulikuwa mtu mwema utaenda mbinguni, au kama wewe ni mbaya utaenda motoni.

    Ila nachojua ni kuwa hakuna mtu aliyekufa na karudi duniani kuelezea Kifo kilikuaje.

    Lakini maskini, hao watu waliopanda kwenye ndege jana usiku wakijua kuwa leo watakuwa Nairobi au wata transfer Nairobi kwenda sehemu zingine. Inasikitisha.

    ReplyDelete
  3. kwa mujibu wa dini yetu ya Kiislam, mtu anakuja duniani kama kupitia njia tu. namaanisha kuwa kuna pepo kwa watenda mema na moto kwa watendao maasi. na kama mtu akifa kafa tu basi kusingekuwa na faida ya kuwa na dini.

    ReplyDelete
  4. msinichekeshe mnanikumbusha mbali hapa Tanzania kuna magazeti ya kiswahili hapa Tanzania kama vile "Uhuru,Mtanzania,Nipashe,n.k" Sasa mtu utakuta kabandika picha ya marehemu aliyekufa miaka iliyopita,halafu utakuta anaandika hivi chini ya picha ya marehemu wake " Leo ni miaka kadhaa toka ulipotutotoka unakumbukwa sana na ndugu zako fulani na fulani"

    Sasa swali je hayo magazeti yanasomwa na hao marehemu huko waliko?

    Haya maneno nafikiri mara ingine ni uigaji mambo usio na kichwa wala miguu.

    ReplyDelete
  5. huyo anony anayedai kwamba dini yako inasema kwamba ukifa unaenda peponi kama ulikuwa mwema na motoni kama ulikuwa mbaya mdhambi nasema hivi kama hiyo nfio dini yako inavyosema basi haya amini hivyo isipokuwa najaribu kufikiria mungu kama baba yetu sijui anapata nini au inampendezaje yeye kama ametuumba na kutupa maisha halafu eti anatu tormrnt kwenye moto wa milele
    najifunza kwamba mungu ni upendo na ndio maana alituumba tukapewa maisha pili najaribu kufikiria kwa mfanao wewe ungelikuwa baba na leo hii mwnao anakukosea sijui kama ungelimchoma moto milele eti amekukosea kwa kuzingatia hili sidhani kama wewe baba mwanadamu unaupendo wa mwanao zaidi ya ule wa mungu
    sasa kama mungu anaupendo zaidi ya kiumbe chochote ni kwa nini basi atuchome moto milele eti kwa sababu tumekosa?
    kuhusu kifo ktk kitabu kitakatifu cha dini yangu kuna mifano kadhaa ya watu ambao walifufuliwa mfano doricas na lazarus lakini wote baada ya kufufliwa hakauna ushaidi kwamba walisema chochote juu ya mbinguni ,paradise au pepeoni hakuna hata mmoja wao alisema chote juu ya kuna paradise huko aupepo au hell
    pili kitabu hicho kizuri kina sema tulikuwa muvumbini tutarudi kwa kuwa huko ndo tulitoka lakini hakaikusema ukifa unaenda peponi
    pia kimesema tutakufa leo lakini tuna matumani ya maisha ya milele hapa duniani kama kama tunaimani na hiyo ni babada ya kufufuliwa
    pia hicho kitabu kimesema the meek ones shall inherit the earth
    pi kimesema mungu aliumba dunia na ulimwengu na vyoote vilivyoma ili sisi tuweze kuishi humo na siyo kwamaba alitutengenezea pepo au mbingu ili kwamba tukifa tuende hukona mwiso kama mtu ukifa eti kuna maisha babada ya hapao basi kifo hakina maana na kwamba maana ya kifo inabidi ibadilike na kwamba basi kifo does not exist
    anay way jamani tumwombe mungu hivi sasa awape nguvu na awaongoze ndugu woote wa marehemu hasa ktk wakati huu mgumu wa majonzi wa kupotelewa na their loved ones
    amen

    ReplyDelete
  6. Suala la ukifa unaenda wapi it is up to you.Hiyo ni personal affair utajijua mwenyewe.Kama utaoza,utakwenda motoni au utaenda mbinguni au hutaki kokote shauri yako I don`t mind.

    Najali maisha yangu ya sasa yajayo ukifa hayanihusu na siyo issue ya maana sana kwangu!Tena mabo yenyewe eti baada ya kufa who cares about a dead person.Utajijua mwenyewe uliyekufa.

    ReplyDelete