Tuesday, June 05, 2007

Ukiumwa malaria Marekani!


Umewahi kuugua malaria Marekani? Usiombe maana ugonjwa ambao unatibika Bongo, inaweza kukuua hapa. Bora uje na dawa kutoka Bongo kabisa.

Hapa USA hawaelewi kabisa malaria ni ugonjwa wa aina gani. Nawambia huwezi kuipata kupitia kwenye hewa. Nikawaambia kuwa Afrika, m ugonjwa wa malaria ni common vile ugonjwa wa mafua hapa. Watu wengi tu wanapata. Nawaambia inaambukizwa na mbu, tena anopheles mosquito. Hapa Marekani hamna. Kuna siku niliwaambia watu weusi na wazungu wa hapa kuwa niliuugua malaria sana nikiwa Tanzania, wakanitazama kwa mshangao na woga. Utadhani walikuwa wanamtazama Frankenstein yule monster wa kwenye masinema!

Nafahamu wazungu kama wanne ambao wamekufa nao hapa. Kisa madaktari hawakujua wanaumwa nini. Wali safiri nchi zenye malaria na kuugua baada ya kurudi. Pia mara nyingi madatari wa Marekani hawa uzoefu na huo ugonjwa ambao Tanzania ni kama kuugua mafua hapa.

Kuna MBongo kanisimulia kuhusu alivyokuja tu kutoka Bongo miaka ya 80, New York. Anasema alianza kujisikia vibaya na akaenda clinic. Kamwambia daktari kuwa anadhani ana malaria, maana katoka Tanzania hivi karibuni. Heh! Kosa kubwa. Kajaza fomu kwenda CDC (Center for Disease Control). Anasema manesi walikuwa wanamwogopa. Wakawa wanauliza kama wanaweza kuambukizwa. Anasema daktari hakuwahi kutibu malaria na ilibidi angalie kwenye kitabu na kumwandikia prescription ya quinine! Damu ilipimwa na ilichukua siku tatu kupata majibu. Haikuisha hapo, anasema alivyofika nyumbani katembelewa na health officer wa serikali. Wakamwuliza maswali mia kidogo mpaka kaogopa kuwa atarudiishwa Tanzania.

Bahati nzuri haikuwa na malaria wakaacha kumsumbua.

Lakini hivi karibuni kuna jamaa alienda Tanzania, karudi na malaria. Akashindwa kwenda kazini , alichukua siku mbili off na kupiga simu kuwa amerudi kutoka safari lakini anaumwa. Alivyoenda kazini, bosi kamwuliza alikuwa anaumwa nini, jamaa kamwambia, alikuwa na malaria. Heh! Utadhani jamaa alimwambia anaumwa Ebola virus. Jamaa alifukuzwa kazi. Nikamwambia bora ungemwambia unflu au UKIMWI, kulikoni umwambie kuwa una malaria.

Na kuna dada fulani naye aliuugua, tena alipata attack ya kusikia baridi na kutetemeka akiwa kazini. Kazi aliyokuwa anafanya ni ya kuangalia wazee. Huyo alikuwa na bahati walimpa paid leave ya wiki tatu! Lakini aliniambia kuwa alijuta kwa nini aliwaambia maana watu walikuwa kama wanamwogopa.

Naona siku hizi mambo kidogo afadhali, maana kuna tropical disease experts wengi. Wengine walifanya practicals kwenye mahospitali za Afrika na hata Tanzania. Lakini ukimkosa mtaalamu wa kukutibu, Mungu akulinde.

Karibuni mtoe maoni yenu au story zenu za malaria Marekani.

6 comments:

  1. Hii ni kweli kabisa. watu waende na dawa zao au wamlazimishe daktari awaandikie dawa-watu wengi hawajui haki zao.

    ReplyDelete
  2. @Chemi,
    Nina rafiki alitoka Liberia. Wakati anakuja, hakujua kwamba virusi vya malaria vilikuwa mwilini. Sampuli ya damu ilitembe toka Lexington, KY mpaka CDC Atlanta. Gharama ya tiba (ukitoa sehemu ya bima) ilikuwa kama $400 hivi.

    Angekuwa Bongo nadhani $1 tu ingetosha.

    ReplyDelete
  3. Nilihskuwa na experience hiyo sehemu nyingi sana duniani, kuna wakati nilikata tamaa kabisa nikiwa Japan hasa kwa vile kasi ya malaria huwa ni kali sana lakini dakitari wangu alichukua sample ya damu yangu na kuipeleka kwenye maabara kupata full blood picture. jambo lilichukua karibu siku mbili kabla sijapata dawa yoyote. Mara ya mwisho nilipoondoka Tanzania, nilikuja na dawa za maralia aina ya fansida niliyonunua kwenye famasi moja pale Dar bila kuwa na cheti cha daktari. Nilipokuwa njiani kabla ya kufika marekani nikagundua kuwa nikifanyiwa upekuzi pale airport nikakutwa na dawa hizi nitakuwa nimekwaa kisiki kikubwa sana, hivyo nikaamua kuzimeza hata kabla sijapata malaria ingawa nilikuwa nikiitegemea kwa vile niliumwa mbu sana pale Dar nikiwa kwenye vijiwe vya bia. Kwa bahati nzuri nilipofika hapa sikuugua malaria, labda ni kutokana na preemptive action ya dawa nilizomeza. Ushauri wangu ni kuwa ukija na dawa zile uhakikishe unazificha sana au uwe na cheti cha dakitari kwa vile ukishikwa na wakaguzi wa customs pale Airport unaweza kuishia lupango.

    ReplyDelete
  4. Jaduong,

    Hiyo ni kweli kabisa, nasikia sampuli zinauzwa kwenye maabara na hata vyuo vikuu wanavilipia.

    Kibri,

    Kwa kweli huenda hiyo pre-emptive measure ilikusaidia. Lakini kweli usisahau kuja na dawa ya malaria. Lakini ni kweli huenda wakadai prescription, lakini anti-malarials siyo narcotics. Lakini Customs officer ambaye hajui anaweza kusema una mandrax au sijui vidonge gani. Mwambie alambe aone uchungu wake.

    ReplyDelete
  5. Jamani tuwe makini na comments kama una uhakika we sema tu vijidudu vya malaria.

    Malaria husababishwa na single cell organisms, parasitic protozoa(kingdom: protoctista) ambao huitwa plasmodium na si virus.

    Kitaalam virus hawapo active (non-living) mpaka wawe kwenye living cells, na ndio maana virus huwezi kumuua bila kumtenganisha na living cell. virus wengi hutulizwa kama mafua n.k ila protozoa huweza kuwaua kwa kutumia dawa ikisaidiwa na antibody(protein that fight infections)kwani ni living cells.

    Kwa kuongezea ndio maana Human Immunodeficiency Virus (HIV) ambao husababisha UKIMWI(AIDS) imekuwa vigumu kuwaua au kuwatuliza kutokana na nature ya virus hawa ku replicate in living cells na kushambulia mfumo wa ulinzi wa mwili (Body Immune System)

    Sasa JADUONG METTY utakuwa umeelewa tofauti kati ya virus na non-virus. next time sema vijidudu kama huna uhakika na biological classification.

    Nashukuru

    ReplyDelete
  6. Unajua non tropical countires hawajui malaria kabisa, mi nakumbuka nilipo fika UK nikawa nasumbuliwa na tumbo kumbe ngiri bwana shauri ya baridi. Sasa cha kushangaza nikaenda NHS, jamaa wakachukua damu kidogo kupima, niliporudi next time jamaa wakawa very interested na damu yangu wakaniambia nipo OK ila hawajaona ugonjwa wowote hatari kwa afya yangu, nikamuuliza HIV vipi wakaniambia No problem nipo OK, Ila wakasema niwape sample zaidi wakafanye intensive blood check, nikajua kidogo tu, he jamaa walichukua kama robo rita ya damu. Baadae wakaanza kunihoji lini niliugua malaria n.k, kumbe yote ilikuwa janja tu lengo ni sample ya malaria kwa kuwa bongo karibu kila mtu ana vijidudu vya malaria kiasi mwilini. Anyway niligundua too late baada ya kushituliwa na jamaa.

    ReplyDelete