Monday, August 06, 2007

Mjue Msanii Chipukizi wa Bongo - Liz Michael

Liz in her costume for Bongoland II scene.
Cameraman Sam Fischer akipozi na Liz Michael baada ya audition yake.


Nilisema siku nyingi kuwa Bongo kuna watu wenye vipaji vikubwa katika mambo ya uigizaji. Na kweli, tulivyokuwa kwenye shoot ya Bongoland II huko Dar, tuliona wengi wenye vipaji. Hata vijana wadogo wamebarikiwa.

Nilikutana na msichana Liz Michael Kimemeta, mwenye miaka 12 tu. Kama uko Bongo huenda umemwona akihosti vipindi vya watoto. Katika sinema ya Bongoland II anaigiza kama mtoto muuza chapati. Alijua lines zake mara moja na kushangaza watu. Nilimwuliza kama mzazi wake alimsukuma katika mambo ya uigizaji na filamu, alisema hapana na alitokea kupenda mwenyewe.

Pia Liz aliweza kuongea kiingereza kizuri sana (alisema alianza kujifunza kiingereza mwaka jana tualipo hama shule) na kuelezea crew kuhusu ndoto yake ya kuifka Marekani na kuigiza katika sinema huko. Akiendelea na moyo wake huenda atafanikiwa.

6 comments:

  1. Da Chemi afadhali umeongelea swala la kiingereza. Ndiyo ugomvi wangu mkubwa na wasanii wa bongo. Kama hujui kiingereza ongea kiswahili watu watafsiriwe.

    Kuna michezo ya kuigiza ya Tanzania inakinaisha kwa kweli wakishaanza pumba za kizungu. Naita pumba maana hawana lazima ya kuzungumza lugha wasioijua!!! Kama ni kujifunza wajifunze kwanza na sentensi zao zihaririwe. Mchwiiiiiii

    ReplyDelete
  2. Anonymous wa 10:51 am, asante kwa maoni yako. Kweli kiingereza bado ni shida kwa watu wengi Tanzania na hii inatokana na historia yetu. (Kuongea English ni Kasumba!)

    Huyo binti aliniambia kuwa anasoma shule ya English Medium sasa toka mwaka jana na ndo anajifunza English huko, na kwa kweli aliongea kiingereza kizuri mpaka nilishangaa. Na ilikuwa rahisi yeye kuelewana na wazungu tuliyokuwa nayo.

    Kuhusu English kwenye michezo Bongo, nakubaliana na wewe. Kama hawawezi kuongea Proper English basi ni bora watumie kiswahili.

    ReplyDelete
  3. Che ponda lazima huy ni ndugu yako unampa publicity.Atakua big headed she wont do well maana ni mtoto tu.

    ReplyDelete
  4. Anonymous wa 12:31am, huyo mtoto nimemjua kwenye film shoot. Na tayari yuko kwenye TV Tanzania aki host vipindi vya watoto, hivyo kama ni big headed, basi tayari kwisha kuwa big headed.

    Lakini ujue nilikutana na watu grown-ups waliokuwa big headed kweli kweli kwa vile wametoka kwenye TV play. DUH!

    ReplyDelete
  5. da chemi naungana nawe kwa kweli huyu mtoto anajitaidi sana atafika mbali yani anaigiza vizuri sana na bila woga nimeona michezo mbali mbali alioigiza shiz iz young and the best

    ReplyDelete
  6. Da Chemi sisi bwana ze englishi ni problem kwani siku moja nilishangaa mtu gradueiti mmoja kutoka mlimani akijikanyaga kwenye tensi. Kwa kweli nilishangaa sana. Lakini ndo hali halisi. Kuna wakati wazalendo walidai kubadilisha masomo kwa lugha ya Taifa sasa sijui lengo lao lilikuwa ni nini. Ukizingatia uchumi wetu ni tegemezi. Hata mheshimiwa prezidaa mwenyewe kuna wakati amekuwa akichemsha, jaribu kuangalia konvazesheni zake awapo nje ya nchi.

    ReplyDelete