Wednesday, August 29, 2007

Wapenzi na Wivu


Mara nyingi tunasikia habari ya mtu kumpiga mpenzi wake kwa ajili ya wivu. Mwanamke kasalimiwa na mwanaume mwingine, kibao! Mwanamke anapiga simu nyumbani kumwulizia mtu, mke anampiga na sufuria na mengine. Lakini wakati mwingine wivu unazidi mpaka watu wanafanya maajabu.

Nimesikitika sana kusikia habari ya jamaa kujinyonga Gesti huko Tandika eti kwa vile mpenzi wake wa miaka 19 alikuwa na wapenzi wengi. Kitu gani kilimwingia marehemu Said Libonge mpaka kaamua kumchoma mpenzi wake kisu na yeye mwenyewe kujinyonga. Ni wivu au ugonjwa wa akili?

Mimi sikuwepo bali nimesoma tu hiyo habari ya kusikitisha. Na huyo dada lazima atajiuliza mara mbili tatu kabla ya kuingia gesti na mwanaume au kuwa na mpenzi mwingine.

Lakini nikikumbuka vituko wanavyofanya wapenzi kwa jina la wivu, nasikitika na nacheka. Haya tuchukue kesi ya mama fulani aliyemkuta mume wake yuko kwenye shughuli ndani ya gari eneo ya Mbuyuni Dar es Salaam miaka ya tisini. Yule mama alidai kuwa alifungua mlango wa gari kamkuta mume wake yuko juu ya howara wake anapampu na alidai kuwa mambo yao yalikolea kiasi kuwa alikuwa anampiga mume wake aliyekuwa ameshusha suruali matakoni na hakusikia kitu. Kwanza mtu wa kawaida angebakia anashangaa mdomo wazi, au angekimbia kwa aibu. Lakini hapa huyo mama na wivu zake kaweza kufungua mlango wa gari na kuanza kumpiga mtu shughulini.
Haya nakumbuka kisa cha mama mwingine miaka ya themanini. Mume wake alienda na howara wake kwenye gesti Manzese. Yule mama alijua yuko chumba gani. Kitanda kilikuwa chini ya dirisha. Basi yule mama alikesha pale kwenye dirisha na walipoanza mambo yao, yule mama kafungua dirisha na kuwamwagia chupa ya tindi kali. Kwa vile walikuwa uchi wote waliungua vibaya! Wivu jamani!

Nilivyokuwa nasoma Tabora Girls kuna dada fulani aliuliwa na mume wake. Sitamsahau yule dada. Alikuwa anakaa National Housing na mume wake, ndoa yao bado changa. Dada mwenyewe alikuwa mzuri kweli kweli. Mume wake alikuwa ni mwanajeshi mwenye cheo cha Kepiteni. Alikuwa mwembamba mwenye kipara. Kuna wenzangu walimuwa wanamvizia yule baba. Basi kuna siku yule baba alishikwa na wivu, kamfunga kamba mke wake na kumtia matambara mdomoni mwake kusudi asiweze kupiga kelele. Wanasema kuwa yule baba alimpiga raundi ya kwanza, kampiga raundi ya pili, kampiga raundi ya tatu mpaka yule dada kafa. Eti kapusuliwa bandama! Kisa cha kumpiga mke wake mpaka kafa kilikuwa eti alimwona anaongea na mwanume mwingine. Yule baba alihukumiwa kifo.

Niendelee? Kuna visa vingi, vya watu kuua au kuumiza wapenzi wao kwa jina la wivu.

Mimi mwenyewe nimeshikwa na wivu mara kadhaa lakini siyo kiasi cha kuua au kumwumiza mtu! Niwasimulimie kisa kimoja. Kuna jamaa nilikuwa nampenda sana. Lakini yeye hakunijali wala nini zaidi ya kusalimiana. Basi kuna siku nilimwona anakwenda kwenye deti mjini DSM na dada fulani! DUH! Nilijikuta naona kizunguzungu, Siwezi kusema, hasira zimejaa na nikaanza kulia! Watu waliniuliza nalia nini, nikashindwa kusema! Baadaye nikasema basi Mungu hakupanga niwe naye. Yaani nikikumbuka nacheka.



Mnasemaje kuhusu wapenzi na wivu?

9 comments:

  1. Wivu ni kitu kibaya sana regadless upendo wako ni mkubwa kiasi gani. Cha muhimu ni kujitayarisha kukabiliana na matokeo ya mapenzi kisaikolojia hapo ndio utaokoka. Kinyume na hapo jasho litakutoka utajikuta segerea bure.Vile vile mapenzi ni uamuzina hiari ya mtu kutoka moyoni. Wenzetu wazungu moyo unapokengeuka anakuwa muwazi na kusema sasa hivi upendo unapungua na nimependa mtu mwingine hata katika ndoa. Sisi waafrika ni deni ukipendwa wewe unataka uwe wewe tu na si vingenevyo. Tukumbuke kuwa upendo ni hiari na involuntary mtu anapo amua kuwa na mahusiano na mtu anakuwa amedhamiria kwa hiyo ukate panga ulie haitabadili chochote. Thoery yangu kwa wanandoa ni mpaka mtu unaamua kuvua nguo unakuwa na kili zako timamu na shetani wako wala hakuna ksingizio ch kutegwa ama vinginevyo. Mwenye ndoa una kila sababu ya kumhoji mwana ndoa wako na si yule wa upande mwingine Hivyo basi uliza sababu za msingi kistaarabu zilizopelekea mwenzio kuhamisha upendo. Kama kuna uwezo wa kurekebisha mambo rekebisha haiwezekani anza taratibu.Wasimbe nao hali kadhalika. Ila kwa wenye wivu wa kijinga ndio sina msalie mtu nao kabisa kwa sababu kama nilivyo sema mwanzo binadamu anakuwa na mahusiano na watu mbali mbali kabla ya kujilock na mahusiano hayo yanweza kuwa ya kawaida kabisa yenye upendo wa dhati lakini si mapenzi ya kimwili kwa hiyo ni bora uwe muwazi umuonyeshe rafiki zako na uelezee aina ya uhusiano wako kabla shari haijawa kamili

    ReplyDelete
  2. Huyo kaka uliyekuwa unamtaka hadi ukalia watu wakakauuliza unalilia nini Chemi ndiyo mimi hapa ninayekuandikia.

    Sasa unasemaje Chemi nakusikiliza kwa makini.....Sema basi Chemi..

    ReplyDelete
  3. sasa bila ya wivu kutakuwa na mapenzi kweli? hata wewe chemi najua kuwa una wivu ndo upendo na bila wivu hakuna mapenzi ni kupotezeana muda tu. hata hivyo siungi mkono kuuwa kupiga kujinyonga au kuharibu mali sababu ya wivu.

    ReplyDelete
  4. yiChanzo kikubwa kwa maoni yangu ni tofauti ya kipato kati ya watu wawili wapendanao.
    Kama mmoja ana kazi na mwingine hana, au mmoja kaachishwa au kufukuzwa kazi kunakuwa na chembe za 'inferiority complex' na hivyo mmoja asiye na kazi au mwenye mapato kidogo anamfikiria mwenye nazo kuwa hampendi au hamwonyeshi upendo wa kweli au anamdharau.
    Suala hapa sio kulala na mtu au kuzungumza na mtu, bali ni inferiority complex iliyojijenga ndani ya mtu. Kama wote mna majukumu ya kuwaleteeni kipato ni nadra sana wivu kuonekana.
    Mbaya zaidi ni pale mmoja anapokuwa hana ajira au shughuli ya kujiongezea kipato (au wote hawana ajira)!

    ReplyDelete
  5. Duh unajua dada Chem, wivu ni psychological phenomenon ambayo kwa kiasi fulani huwa inatokana na moral commitment katika mahusiano ya mapenzi. Hivyo, kila mtu ana wivu tofauti ni namna ya kuu-control kwa maana hiyo kitu cha msingi ni kwa mtu kujielewa mwenyewe wivu wako uko wapi. Kama wewe ulivyolia lia ni heri lakini ungeshindwa kuji-control ungezua ugomvi na kusababisha ammbo mengine.

    Nawasilsha

    ReplyDelete
  6. Mimi naomba ushauri Dada chemi na wadau kwaujumla mimi nilimpenda sana my first boyfriend sana tu tulikuwa boyfriend and girlifriend for alomost 9 years wakati wote huo kulikuwa na migogoro sana pamoja na kumkamata aki cheat mara nyingi sana kisingizio ni mtoto wa gate kali,mwishowe niliona nihame nchi kabisa.uwa tunawasiliana kama marafiki ana girlfriend sasa hivi na mimi nina boyfriend ila cha hajambo kuhusu miminimeshindwa kumwamini mwanaume yeyoyote yule saa ingine na jihisi nikokwenye mapenzi kabisa lakini nadhani sio kweli kila relation ni nayo jaribu na end up kumchukia mtu na wala sijali kuachana nae sina ile kitu broken heart ebu ni fanye nini? na yule Ex b wangu anasema anashindwa kuoa kisa kila mwanamke hakuna anaemfaha na mimi siwezi kurudiana nae kwasababu anatabia chafu sana mbinafsi na malaya aswaaaa ila nadhani kama isingekuwa hivyo nadhani maisha yangu ya upendo yangu yangekuwa mazuri sana na sio kwamba si kujaribu nilijaribu mara nyingi sana mwishowe nika give up

    ReplyDelete
  7. Dada yangu hutabiriki kabisa!! Jana injili motomoto leo HOWARA, SHUGHULINI...aisee!!! Any way ni funzo kabambe kwa wenye wivu.

    ReplyDelete
  8. Anon uliyeomba ushauri, kwanza si kweli kuwa huyo jamaa ameshindwa kuoa kwa kuwa hapati mwanamke wa kumfaa. NO! Ni kutokana na tabia yake. He is not ready inside.

    Kuhusu wewe, LEARN TO LET IT GO!! Jisemee kila subuhi kuwa umemuacha huyoooo. Kama una picha zake chukua uzichane!! Usijilazimishe. Move from your confort zone and discover a new world. Watu wengi hivyo hivyo wamedanganywa na vistori mshenzi vya hollywood sijui true love sijui nini wakaishia kuambukizwa virusi. Do not follow your heart, follow your mind!!

    ReplyDelete
  9. Chemi nafurahia sana makala zako. Si hii peke yake bali nyingi sana ulizoandika ktk blog hii. Ya kwanza ambayo ilinisisimua sana ilikuwa ile ya Matako Makubwa ikifuatiwa na ile ya maisha ya JKT Masange (ambapo mimi pia nilipitia kama miaka 6 baada yako).

    Yaani unaonyesha ukomavu wako katika 'open-ness of mind and freedom of expression!'

    Kuna vitu ambavyo watu wengi wanaona haya kuvisema wazi, lakini ktk giza wanavisema au kuvifanya. Lakini wewe umeonyesha ukomavu wako ... na sasa wengi wetu tunaweza kuona na kujifunza.

    Nadhani wapo wengi pia ambao mambo kama haya yamewagusa kimaisha na walikuwa wanapata shida kimawazo. Na kwa bahati nzuri sasa wataona kuwa kumbe hili sio tatizo lililowapata wao pekee bali ni kwa mwanadamu yeyote linaweza kumpata au limeshamsibu!

    I really find your blog very entertainig and a place to socialize with everybody, because you have shown the way!!!

    Thank You Chemi.

    ReplyDelete