Monday, October 29, 2007

Boston Red Sox washinda Baseball World Series tena!



Boston Red Sox wameshinda World Series kwa mara ya pili katika miaka minne. Kabla ya mwaka 2004 walikuwa hawajapata ushindi kwa miaka 86. Watu walikuwa wanasema eti ni laana za Babe Ruth aka. Curse of the Bambino.
Babe Ruth aliwahi kucheza kwenye timu ya Red Sox lakini mwaka 1918 aliuzwa ghafla kwa timu ya New York Yankees. Watu walidai alilaani timu ya Red Sox na huenda ni kweli aliwalaani maana hawakupata ushindi wa World Series kwa miaka 86. Kila mwaka ilikuwa vichekesho maana watu walikuwa na vituko mpaka wachawi wakawa wanaenda Fenway Park kutambika!
Haya wameshinda tena. Nawapongeza ila naomba wa punguze bei ya tiketi za game zao Fenway kusudi watu wa kawaida waweze kwenda kushabiki. Tiketi za Red Sox ni za ghali kuliko timu zote za Baseball Marekani.
Nashinwdwa kuelewa kwa nini wakishinda lazima wajichafuana kwa kumwagiana chupa za champagne? Pia kwa nini ni lazima washibiki wapindue magari na kufanya uhalifu? Kuna maajabu.
ATTENTION RED SOX YOUR TICKETS ARE TOO EXPENSIVE AND YOU ONLY CATER FOR THE YUPPIES! NEXT TIME IT WON'T BE CURSE OF THE BAMBINO BUT CURSE OF THE AVERAGE MAN!

4 comments:

  1. Dada Chemi,
    Inaitwa "world series" ni nchi gani zingine zinashiriki?

    ReplyDelete
  2. In my opinion basebal is the most boaring sport. Jamani mimi sijui ni kitu gani kinawafanya watu waupende huu mchezo ! Halafu kingine kinachoniboa katika huu mchezo ni tabia ya wachezaji wakiwa katika dug out kutema tema mate !

    ReplyDelete
  3. Anonymous wa 9:52am, sijui kwa nini wanaita World Series. Wanaoshindana ni timu walioshinda National League na timu walioshinda American League na wote ni timu za Marekani.

    Anoymous wa 3:46PM. Usiangalie baseball ukiwa unakula maana wanatema mate ni balaa! Kwenye Red Sox huyo meneja wao Terry Francona anaongeza kwa kutema malugi.

    ReplyDelete
  4. Hawa ni wenda wazimu, hivi kwao World maana yake USA? Watashindanaje wa Marekani pekee hala waite World Series. Ndio maana Wamarekani kwa jiografia ni mbumbumbu kwa sababu wanalazimishwa kuamini dunia ni Marekani tu.

    ReplyDelete