Monday, October 01, 2007

Mapacha wabaka na kuua Tabora!

Hivi wanaume wanakuwa na nyege za ajabu kiasi gani mpaka kumbaka mtoto mdogo asiyejua kitu kuhusu ngono. Kwenye ippmedia.com nimesoma habari ya hao mapacha vichaa waliobaka mtoto wa darasa la kwanza ambaye bila shaka, hakuwa na matiti kifuani na sehemu zake nyeti bado za kitoto.

Kama tunavyojua nyeti za wanaume waliokuwa ni kubwa na kwa mtoto mdogo hazifai kabisa. Na kwa kawaida mwanaume aliyekuwa hawezi kumtamani mtoto mdogo hivyo.

Bila shaka hao mapacha walimchana huyo mtoto uko chini na kuharibu kizazi chake na viungo vingine. Huenda alipata 'internal injuries' pia. Yaani walishindwa kumpata mwanamke wa umri wao? Hakuna malaya huko walipokuwa? Kwa nini aliamua kufanya 'gang rape' kwa huyo mtoto? Yaani hao mapacha wanafanya kupigwa mawe hadharani hadi kufa!

Mungu alaze roho ya huyo mtoto mahali pema mbinguni. AMEN.

Naomba na hao mapacha wafungwe gerezani maisha!

****************************************************************************
From ippmedia.com

Mwanafunzi afa kwa kubakwa na mapacha 2007-10-01

Na Lucas Raphael, PST Tabora

Mwanafunzi wa darasa la kwanza wa Shule ya Msingi Mkoani ya mjini Tabora, amekufa baada ya kubakwa na wavulana mapacha wenye umri wa miaka 17. Kufuatia mauaji hayo, watuhumiwa (majina yanahifadhiwa kwa ajili ya umri mdogo), walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Tabora.

Mapacha hao walipandishwa kizimbani Ijumaa iliyopita kujibu tuhuma za kubaka na kuua mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Bi.Roda Ndimilanga. Mwendesha Mashitaka wa Polisi Bw.Wilibad Kaiza alidai mbele ya Hakimu Bi.Ndimilanga kuwa washitakiwa kwa pamoja walimbaka mtoto huyo na kupelekea kifo chake.

Aliendelea kuileza mahakama hiyo kuwa washitakiwa hao walitenda kosa hilo Agosti 28, mwaka huu, majira ya mchana, katika Mtaa wa Kwihara katika Manispaa ya?Tabora. Kaiza aliendalea kudai kuwa watuhumiwa hao walimsababishia mtoto huyo (jina limehifadhiwa) maumivu makali sehumu za siri na kupelekea kifo chake.

Watuhumiwa hao walifikishwa kwa mara ya pili katika mahakama hiyo, ambapo mara ya kwanza ilikuwa Agosti 30, mwaka huu, kwa tuhuma za kumbaka mtoto huyo. Hata hivyo, watuhumiwa hao walifikishwa mara ya pili mahakamani kwa tuhuma zakubaka na kusababisha kifo cha mtoto huyo.

Washitakiwa hawakutakiwa kujibu chochote hadi watapofikishwa katika mahakama kuu? kwa kuwa kesi hiyo imeangukia katika kesi za mauaji na hivyo kesi hiyo imepangwa kusikilizwa Oktoba 11 mwaka huu.

8 comments:

  1. DADA chemi kiswahili kinavyokutoka mpaka mwili unasisimka,mwezi wa toba huu,punguza makali

    ReplyDelete
  2. Hii habari ni ya kusikitisha sana tena sana. Tunaamini sheria zilizopo zitatumika kuwaadhibu wahusika. Lakini dada Chemi hayo maswali uliyouliza hapo unamuuliza nani? Hawa jamaa sidhani kama wananafasi hata ya kuyaona.

    Mungu ailaze pema peponi roho ya malaika huyu asiyena hatia yoyote.

    ReplyDelete
  3. Taarifa hii ni ya kusikitisha sana tena sana. Lakini dada Chemi hayo maswali yako unamuuliza nani hasa? Inaelekea una-jazba wewe!
    Maana hawa jamaa sidhani kama wana nafasi wa hata kuyaona.

    Mungu ailaze pema peponi roho ya malaika huyu asiye na hatiya wala asiyejua lolote. Na pole kwa wazazi.

    ReplyDelete
  4. Inasikitisha sana.Maana kwa jinsi nilivyosoma habari yenyewe.Naona watoto(chini ya miaka 18) wammembaka mtoto mwenzao mwenye miaka 10.

    Yaani ni suala la kuumiza kichwa na wadau inabidi tujiulize nini chanzo.Je ni utandawazi?Maana nakumbuka zamani wengine tulipata muda wa kuongea na babu huko kwetu usukumani mida ya jioni wakati tukiota moto'SHIKOMBE'.

    Leo hii mmomonyoka wa maadili unazidi kuitafuna jamii yetu.Baba yupo busy kazini na mama.Wakirudi wapo bzuy kublog na kutazama news kwenye Runinga.

    Watoto wanajilea wenyewe.Kila kukicha mwalimu wao na mlezi ni tv na redio,ambazo kwa asilimi kubwa kila wakati nyimbo sio zile tena za kina Patrick Balisidya(dunia ya mashaka) au Marijani Rajabu(ulimwengu uwanja wa fujo).

    Leo hii asilimia kubwa ya nyimbo zetu ni maloveeeeee weee kwa kwenda mbele utafikiri ndio yameanza leo.Kila anayetoa 'singo'uko mbali mpezi,nakumiss,njoo unishike,mgongo mgongo,naomba nivunje kikombe chako etc.

    Lazima tujiulize mchango wetu ni upi katika hili kama jamii ili kunusuru watoto kama hao.

    Lets play our part,kuwasaidia watoto kama hao wasiendelee kubakwa.

    Mwenyezi mungu amlaze roho yake mahali pema peponi amina.

    ReplyDelete
  5. Mambo ya kutia hasira mnoo lakini kama ni vichaaaa na kicha chao ni cha kuwaona watoto watu wazima hapo kazi lakini usitie shaka mpenzi wangu dada chemi nakupa hii blog usome utulize moyo chini karibu http://hadithizachiku.blogspot.com/

    ReplyDelete
  6. Mbona ume-generalize kuwa wanaume wote wanafanya ngono au kutamani watoto wadogo.
    Nilishawahi kumsikia mtu mmoja redioni akisema kuwa 'all generalizations are false', naamini alisema kweli!!

    Umetumia neno malaya sijui ulimaanisha wanawake?

    Hivi Chemi tukikutana huko Boston nikikuomba 'mapenzi' utanipa?

    ReplyDelete
  7. enzi zetu wengine (au niseme mimi binafsi!!) wakati wa tukiwa na miaka 17 tulikuwa hatajawahi kufanya mapenzi, sasa hawa vijana inaonyesha wameshaaanza na wamepitiliza kwa kumpiga mande mtoto mdogo. duu!!makubwa haya

    ReplyDelete
  8. Lakini pia Chemi usikurupuke na hasira sana maana ukikurupuka basi utakachofanya ni kulipiza kisasi na wala siyo kumwadhibu muhalifu. Kumbuka "two wrongs won't make it right".
    Kwa mfano; umeuliza "jee kwani huko kwao hakuna malaya?" Sasa kweli wewe Chemi kama mwanamke unakubali kuwepo kwa malaya?

    Pili, unataka watu kenge maji hawa mapacha wapigwe mawe mpaka wafe, jee ni kweli hii ndo adhabu inayofaa kwa mtoto wa miaka 17 kwa kosa la ubakaji?

    Mimi ningeshauri mbwa hawa mapacha wapigwe sindano za ajabu ili nyeti zao zisifanye kazi tena mpaka siku ya kiyama. Funza kama hao mapacha wana nyege za ajabu sana wanaweza wakamfanya vibaya hata mama yao mzazi kisha wakasingizia ulevi.

    ReplyDelete