Thursday, October 04, 2007

Steven Spielberg amkomesha Kijana aliyefichua siri ya sinema yake!

Steven Spielberg

Actor/Dancer Tyler Nelson

DOH! Steven Spielberg na George Lucas wana mabilioni ya dola. Lakini walimshitaki kijana wa miaka 24, aliyekuwa extra kwenye sinema yao mpya. Sasa maskini ya mungu huyo Tyler Nelson, atakuwa maskini kupindukia na itabidi aishi kwenye boxi chini ya daraja! Kisa kamwudhi Spielberg. Tyler alikuwa anaigiza kama askari wa kiRusi. Pia anacheza densi.
Spielberg anatengeneza sinema inaitwa, Indiana Jones and the Kingdom of the Crystal Skull . Wafuasi wa sinema za Indiana Jones wanaingojea kwa hamu. Itatoka 2008. Sasa huyo kijana Tyler Nelson, alihojiwa na gazeti la huko kwao, Edmund Oklahoma na kusema alichoona akiwa kwenye seti.

Mkono wa Spielberg ulivyo mrefu na enye vitisho sasa hata hiyo article huwezi kuisoma! Ni hivi kila mtu aliyecahguliwa kuigiza na kufanya kazi kwenye hiyo sinema ilibidi wasaini, "NON-DISCLOSURE Agreement" Yaani wasiseme walichoona. Lakini inaelekea Tyler aliingiwa na Kiwewe na kashindwa kuvumilia maana kuigiza katika sinema ya Hollywood ilikuwa kitu kikubwa mno maishani mwake.

Uko Hollywood kuna watu ambao wanaogopwa na hasa ni hao wenye majina makubwa makubwa. Ukiwa kwenye seti zao ni lazima ufuate masharti waliyoweka. Wakisema "Ukitoka hapa hakuna kusema ulichoona!" ni lazima ufuate waliosema. Navyoona kumshitaki mtu mdogo kama Tyler wanataka iwe fundisho kwa watu wadogo wengine.

Kinchonichukiza ni kuwa Spielberg kasema eti huyo kijana "hata fanya kazi Hollywood tena"
Yaani walishindwa kukata scenes zake au kudai arudishe malipo aliyopata.

Lakini mikosi na hiyo sinema inaendela. Leo wametangaza kuwa vifa akama computer na props zimeibiwa kutoka kwenye set.

Kwa habari zaidi someni:

http://www.express.co.uk/posts/view/20541/Actor-s-big-mouth-loses-him-his-break-in-Indiana-Jones-IV

http://www.femalefirst.co.uk/entertainment/Steven+Spielberg-41473.html

http://news.scotsman.com/entertainment.cfm?id=1583572007

http://www.digitalspy.co.uk/movies/a76961/indiana-jones-lawsuit-is-settled.html

3 comments:

  1. chemi napenda kusoma blog yako kwa sababu moja; iko informative.

    katika maelezo yako unakuwa straight forward au tuseme precise kiasi kwamba hata kwetu tulioko UK na kwingineko inakuwa raha kufuatilia matukio ya US.

    by the way, interest yako katika film industry inanifanya niwe shabiki wako bila hata kukufahamu.kazi kunjufu...!

    ReplyDelete
  2. "non-disclosure agreement" sio mchezo bwana. Huyo Kijana atapata adhabu anayostahili. Labda naye inabidi apate mwanasheria mzuri ili kusaidia kupunguza makali.

    ReplyDelete
  3. 'Indiana Jones' Lawsuit Settled

    Oct 3

    SANTA MONICA, Calif. (AP) - The producers of the new "Indiana Jones" movie have settled a lawsuit against an actor accused of breaching a confidentiality agreement by revealing the film's plot in a newspaper interview.
    A Superior Court order was filed Tuesday finding that Tyler Nelson knowingly violated the agreement that he signed when he was cast to appear in a scene of "Indiana Jones and the Kingdom of the Crystal Skull," said Lucasfilm Ltd. publicist Lynne Hale.

    The agreement barred everyone involved in the film from publicly discussing it.

    Terms of the settlement were not disclosed. An after-hours call to Nelson's talent agency was not immediately returned.

    The fourth installment of the adventure series was directed by Steven Spielberg and stars Harrison Ford.

    Tyler revealed plot details during an interview last month with his hometown newspaper, Oklahoma's Edmond Sun, Daily Variety reported. That story has been removed from the newspaper's Web site.

    "We ask every cast and crew member to sign a confidentiality agreement because we want to protect the movie's thrills and surprises for audiences," said Lynn Bartsch, Lucasfilm's director of business affairs.

    A spokesman for Spielberg said he didn't know whether Nelson's scenes would be cut from the movie.

    The new Indy adventure, which also stars Cate Blanchett and Shia LaBeouf, will be in theaters next May.

    ReplyDelete