Wednesday, November 21, 2007
Happy Thanksgiving
Kesho ni sikukuu ya Thanksgiving yaani siku ya kushukuru hapa Marekani. Ni sikukuu kubwa hapa Marekanai karibu kila kitu kinafungwa kusudi watu waweze kwenda kusherekea na familia zao.
Asili ya Thanksgiving ni kutoka mwaka 1620, wale wazungu wa kwanza walivyotoka uingereza kuja Marekani. Walitua hapa Massachusetts shemu ambako sasa tunapaita Plymouth. Walifika zaidi ya watu mia mbili lakini wengi wao walikufa shauri ya njaa na ugonjwa. Waliponea watu 51 tu! Watu wa asili wa pale, wahindi wekundu, waliwasaidia na kuwaonyesha jinsi ya kulima vyakula kama mahindi na kula bata mzinga (turkey).
Zaidi ya wale watu 51 kuponea kifo, Thanksgiving ni siku ya kushukuru na kukumbuka familia.
Kesho kutakuwa na maandamano za kusherekea na za kuipinga. Kuna watu amabao wamechukia maana wale wahindi wekundu waliowaokoa wale wazungu waliangamizwa! Na ilikuwa mwanzo wa ukoloni Marekani na kuangamizwa kwa wahindi wekundu pote Marekani.
WaBongo wengi hapa wanasherekea sehemu mbalimbali kwa party na ma dinner.
Nawatakia Thanksgiving njema.
http://www.objectivistcenter.org/cth--1593-The_Productive_Meaning_of_Thanksgiving.aspx
http://countenance.wordpress.com/2006/11/22/the-true-meaning-of-thanksgiving/
http://www.boston.com/ae/food/dishing/2006/11/the_real_meanin.html
Dada Chemi I also wish you and your family a Happy Thanksgiving! Thank you for your nice posts.
ReplyDeleteHappy Thanksgiving!Nakutakia kila la kheri katika kuinjoi siku! Wakiinjoi , injoi !La sivyo, kasheshe!:-)
ReplyDeletehappy thanks giving wapenzi wote wa da-chemi na chemi mwenyewe!!
ReplyDelete