Tuesday, November 20, 2007

Majambazi wavamia UDASA Club!

Duh!

*************************************************************************
From ippmedia.com

Majambazi yapora pesa Chuo Kikuu Mlimani

2007-11-20
Na Mwanaidi Swedi, Jijini

Watu wawili wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wamevamia bar ya UDASA iliyopo Chuo Kikuu Dar es Salaam kampasi ya Mlimani na kufanikiwa kupora simu za wateja, pesa na vitu vingine kadhaa .

Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Jamal Rwambow, amesema tukio hilo limetokea jana mishale ya saa 5:20 usiku. Kamanda Rwambow amesema Polisi walipata taarifa kutoka kwa Meneja wa bar hiyo, Bw.Titto Raymond, 29, akidai kuwa jana akiwa kazini walifika watu wawili wakiwa na silaha na kuvamia bar ya Udasa na kukomba pesa zote za mauzo ya siku hiyo, simu za baadhi ya wateja na Vocha mbalimbali za simu.

Akasema Kamanda Rwambow kuwa inaonyesha watu hao walifika kwenye baa hiyo mapema na kujinganya miongoni mwa wateja waliokuwa wakijipatia kinywaji. Amesema ghafla watu hao wakaibuka na kuvamia kaunta ya bar hiyo wakiwa na silaha na kuwaamuru wateja wote kulala chini. Amesema baada ya wateja kutii amri ya kulala chini, wakawaamuru mhudumu wa kaunta awape pesa zote.

Amesema majambazi hao walipoona wahudumu wakisuasua kuwapa fedha, wakaamua kuvunja kaunta na kufanikiwa kuchukua pesa zote za mauzo kiasi cha shilingi milioni moja na vocha za simu zenye thamani ya shilingi 430,000. Akasema baada ya hapo walianza kuwapekua wateja waliokuwa wamelala chini na kuwapora simu zao hususani zile walizokuwa wakiziona kuwa ni za bei mbaya.

Amesema Kamanda Rwambow kuwa baadhi ya wateja waliokubwa na mkasa huo, wamesema kuwa watu hao walielezwa kuwa mmoja kati yao alikuwa mrefu mnene anakovu la kukatwa shavu la kulia ba mwingine alielezwa kuwa ni mrefu maji ya kunde. Kamanda amesema kuwa Polisi wanaendelea na msako kuwasaka majambazi hao. Aidha, Kamanda Rwambow ametoa wito kwa wananchi watakaowaona watu wa aina hiyo kutoa taarifa katika vyombo vya dola kwani ni watu hatari.

SOURCE: Alasiri

1 comment:

  1. Huu uhandishi siuelewi kabisa eti "watu wawili wanaodhaniwa kuwa ni majambazi".....baadae mhanidishi huyo huyo anasewma...Walipora simu na pesa.. kama walipora kwanini wadhamiwe kuwa ni majambazi?..mimi nafikiri kitendo cha kupora kinafufanya uwe ni jambazi na sio tena kudhaniwa?

    Concord

    ReplyDelete