Wednesday, January 09, 2008

Hillary Clinton ashinda New Hampshire!


Senator Hillary Clinton ameshinda uchaguzi wa awali huko New Hampshire kwa upande wa Democrats. Senator Barack Obama, amekuwa wa pili. Matokeo yalikuwa karibu. Clinton alipata asimilia 39% ya kura, na Obama alipata asilimia 36%. Clinton sasa ni mwanamke wa kwanza kushinda uchaguzi wa awali New Hampshire.
Watu walitarajia Obama atashinda tena kwa kura nyingi. Watu wengi walishangaa kuona Bi Clinton anaongoza kutoka mwanzo. Watu wanasema huenda alivyoanza kulia juzi ulisaidia watu kuona kuwa Hillary kumbe ni binadamu kama wao. Bi Clinton aliulizwa awali kuhusu nywele zake.
Hali ya hewa New Hampshire ilikuwa nzuri na wazee wengi walitokea kumpigia kura Hillary. Vijana walioahidi kumpigia kura Obama hawakutokea. Mtangazaji moja alisema huenda walikuwa wamelewa au wamechoka kutokana na kusherekea ushindi wa Obama Iowa.
Bado uchaguzi wa awali katika states 48. Tarehe 5 mwezi Februari states 20 watakuwa na uchaguzi wa awali.
Hillary Clinton, ni mke wa Rais Clinton. Kama akishinda urais wa Marekani atakuwa mwanamke wa kwanza kuwa wa rais wa Marekani, pia atakuwa First Lady wa Kwanza kuwa Rais, na Bill Clinton atakuwa mwanaume wa kwanza kuwa First Gentleman na ambaye aliwahi kuwa rais.

Kwa habari zaidi someni:

3 comments:

  1. Hillary Clinton hatakuwa first lady wa kwanza kuwa rais. Rais wa sasa wa Argentina Cristina Fernandez de Kirchner, ni mke wa rais aliyemaliza muda wake mwaka jana, Nestor Kirchner.

    ReplyDelete
  2. Hi Kithuku,

    Asante kwa mchango wako. Actually nilikuwa nazungumzia Marekani tu. Maana hata Phillipines, Corazon Aquino alishika nafasi ya urais.

    ReplyDelete
  3. Mume wa Corazon Aquino aliitwa Benigno Servillano A. Aquino (maarufu kama Ninoy Aquino), na hakuwahi kuwa rais. Alikuwa senator na pia kiongozi wa upinzani ambaye aliuawa na utawala wa dikteta Ferdinand Marcos mwaka 1983. Hasira za kuuliwa mumewe ndizo zilizomwingiza Corazon kwenye siasa kwa nguvu na bidii kubwa hadi kufanikiwa kuwa rais wa Phillipines. Kwa hiyo Corazon Aquino hakuwahi kuwa first lady, na wafilipino walitumia maneno "first spouse" kumtaja marehemu mumewe.

    Nadhani hadi sasa first lady wa kwanza kuwa rais duniani ni huyo wa Argentina, Cristina Fernandez de Kirchner.

    ReplyDelete