Sunday, January 13, 2008

Steven Kanumba yuko Hollywood!








Wadau mliuliza na hii ni jibu:

Mcheza sinema maarufu wa Tanzania, Steven Kanumba aka. Denzel wa Tanzania, yuko ziarani Marekani. Kwa sasa yuko Hollywood. Amenitumia picha za safari yake na nazi-share na wadau.
Ametembelea Warner Brothers na Universal Studios.
* Steven Kanumba allitutuembelea kwenye seti ya sinema ya Bongoland II tulivyokuwa tunashuti Magomeni. Alitambulishwa kwa crew wetu kama Denzel Washington wa Tanzania. Naona hiyo nickname ni sawa maana amecheza kama lead kwenye sinema/video kadhaa, sijui kama yupo aliyemfikia.

57 comments:

  1. YOU WILL NEVER EVER COMPARE YOURSELF WITH DEZEL WASHINGTON.KANUMBA ACHA MAMBO YA AKA.KANUMBA ANALAZIMISHA KUIGIZA HANA KIPAJI.NAOMBA ULIACHE JINA LA DEZEL PLEASE.

    ReplyDelete
  2. Mh,Kanumba kawa "Denzel wa Tanzani" tangu lini?First time I hear the "nickname".Anyway,all the best for him,hoping he isn't in Hollywood kushangaa shangaa but rather to enhance his promising career.

    ReplyDelete
  3. Naomba kuuliza,hivi kufika Hollywood katika kutembea tu na wala usionane na mtu yeyote bali uishie kupiga picha kwenye mabango(kwa nje)kama mtalii mwingine yeyote tu ni sifa au ni nini hasa?Maana naona watanzania tunataka kupeana sifa zisizo na kichwa wala miguu.Katembelea Hollywood,kama vile mimi au wewe tunavyotembelea au hata kuishi(mimi naishi hapa hapa Hollywood),then what?Ameonana na nani,amejifunza nini,amepata deal yeyote?That is what I would like to hear.Otherwise,such photos nadhani ni better be kept for his own family and friends.

    ReplyDelete
  4. anajitahidi lakini mwili unamzidi. sijui ndio chips mayai za bongo? afanye mazoezi ndio umuite jina hilo la denzil sio sasa

    ReplyDelete
  5. Asante Da chemi, ila akirudi itabidi afanye mazoezi kidogo ataharibika sasa hivi! unless amenenepa kwa ajili ya movie. huo ni mwezi tu au aane hukuhuku kama bado yupo. Marekani ukifika lazima kwanza unenepe maana hakuna anyekushauri habari ya vyakula vinavyo futua mwili. mpige interview basi tujue amejifunza nini so far. Swali lingine ukitaka kuwa extra unafanyaje? na mpaka uwe mji gani? kuna criteria wanaitumia?

    ReplyDelete
  6. dooh kaazi kwelikweli sasa hana mlinzi wala mwenyeji wakumtembeza ana mpiga picha wake tu.

    ReplyDelete
  7. Anonymous wa 7:44AM, ameuliza swali kuhusu kuwa 'extra' katika sinema.

    Inategemea uko wake, lakini kama uko Atlanta, New York, Boston, Los Angeles, Miami na Chicago ndo nafasi zinakuwa nyingi zaidi.

    Uchukue acting lessons. Halafu upige headshot kwa professional pohtographer. Utengeneze acting resume, yaani itakuwa na malezo kyako, una urefu/uzito gani, unaongea lugha gani, una kipaji gani. Halafu zitume kwa casting agencies kwenye mji wako/ au mji karibu na unapokaa. Kama uko union, unapata nafasi zaidi katika kuwa extra.

    Wakati mwingine kunakuwa na Open Casting Call, yaani mtu yeyote anaruhusiwa kwenda. Hapo ndo unaweza kwenda na picha uliyopiga nyumbani. Lakini kwa vile watu wengi wanaenda nafasi ya kuchaguliwa inakuwa ndogo.

    ReplyDelete
  8. nyie wabongo acheni wivu kwa kanumba kazi kusifia ya watu wengine ya home kwenu mnayatusi mimi nilitegemea wabongo wote tungemsifu kanumba na kujivunia kwa hatua aliyofika maana haijawai tokea ktk historia ya film bongo badala yake mnaleta chuki na wivu binafsi..pumbavu zenu nyie watumwa wa nchi za watu igizeni nyie basi tuwaone..hongera kanumba wala usikate tamaa hao wanaosema wanaishi hollywood mbona hawajawai kupiga picha hata moja tukaiona? kazi kuwafuta mavi vikongwe wa kizungu alafu wanajitapa wako hollywood.

    ReplyDelete
  9. WEWE MTOA MAONI WA KWANZA HAPO JUU KWANI DENZEL UNAMUONA MUNGU?AACHE KUTUMIA JINA LA DENZEL AMEKUOA?AU DENZEL ANAKUJUA WEWE?PUMBAVUUUUUUUUUUU MKUBWA WEWE PENDA VYA KWENU,BILA SHAKA SI MTAZAMAJI WA FILM ZA KANUMBA UNGEKUA UNATIZAMA UNGEKUBALI JAMAA LINA KIPAJI..HONGERA KANUMBA WATANZANIA WENZAKO TULIOWAZALENDO TUNAKUUNGA MKONO ENDELEA HIVYO USISIKILIZE MANENO YA WATU WA CHUKI BINAFSI.

    ReplyDelete
  10. AM PROUD OF U STEVE KANUMBA.CONGRATULATION BUT REMEMBER PALIPO NA MAFANIKIO HAPAKOSI FITINA NDIO MANA UNAONA WENGINE ROHO ZINAWAUMA....WEE SONGA MBELE TU

    ReplyDelete
  11. wewe mtoa maoni namba tatu kwanza kabisa nakupongeza kwa kuwa limbukeni namba one tena mwehu,usidanganye watu kuwa unaishi hollywood,hollywood unapajua wewe au unauza unga hapo maana kama si msanii basi unajiuza hapo kama umefika hollywood hata hao mastaa wenyewe hawaishi hapo huwa wanakuja kwa ajili ya film production tu na kwa watu wote tunaoishi marekani tunaelewa sasahivi hollywood kuna tatizo la mgomo wa writters hivyo hakuna star mkubwa yoyote anayewezapoteza mda kukaa sehemu ya anasa kama hapo bila kufanya kazi ndo maana wote wamerudi kwao wewe ulitaka apige picha na nani?acha uongo kama unaishi hollywood lazima utakua wajua gharama na ugumu wa kuingia hapo na sidhani kama ulishawai kulipa pesa uingie hapo maana maisha ya wabongo huku twajuana wenyewe,tunachokuomba da chemi muhoji kanumba tujue hayo mafanikio aliyopata ili nasi tujivunie..hongera kanumba.

    ReplyDelete
  12. congrats kanumba now you re a king of movie in East Africa hata wakikuita denzel ni sawa tu wenye wivu wajinyonge

    ReplyDelete
  13. Hongera sana kanumba hakika unaitoa kimasomaso bongo.

    ReplyDelete
  14. great stuff my broh hongera sana....i like your movie so much esp..dar2 lagos

    ReplyDelete
  15. You are a greatest supar star in tanzania congratulation my dear

    ReplyDelete
  16. i love u kanumba

    ReplyDelete
  17. JAMANI MPAKA MTU KAFIKA HAPO UNIVERSAL STUDIOS,HOLLYWOOD,WARNER BROTHER BADO TU HAMUAMINI NYIE KWELI SHWAINI TATIZO LENU WABONGO ELIMU NDOGO..SOMENI MSIKIMBIE UMANDE.

    ReplyDelete
  18. bahati ya mtu usiilalie mlango wazi na riziki ya mtu mtoaji ni mungu hata ukisema vipi mungu kashampa kanumba panda juu ukazibe

    ReplyDelete
  19. mimi nampenda kanumba

    ReplyDelete
  20. NATAMANI SIKU MOJA NIJE NIKUMBATIWE NA HUYU KAKA KWA JINSI NINAVYOMZIMA NITAZILAI SIKU HIYO

    ReplyDelete
  21. HATA MIMI NAMPENDA KANUMBA

    ReplyDelete
  22. I tell you my friend Mr Kanumba!...acting is a hard business!...and it is even harder to try to be like someone else because no matter how hard you try to be, you will never be like him (Mr Washington)!...there is only one Denzel Washington!

    Ok, don't make fool of yourself! Being at Hollywood doesn't mean anything to you!..it's just another place away from DAR! Don't try to make a name for yourself by posting those pics to fool people back home.

    My advice to you is that continue to work hard and be yourself! To work as an actor in Hollywood is a difficult dream only few in a million accomplished it.

    ReplyDelete
  23. Hi Chemi! Jana nimepata dvd ya Fake Pastors. Kusema kweli acting ya hawa jamaa leaves a lot to be desired. Nadhani hata Wa Nigeria wametupita. Inafaa wapatiwe training zaidi kabla ya kutoa filamu zingine zaidi.

    ReplyDelete
  24. Uwii!! huku manassas kulivyo slow kutakuwa na dili kweli? Sijakata tamaa bado kinacho ni sukuma huwa nakasirika sana wanapokosea kiswahili in some movies or songs ambazo naamini wame rely sana kwa watani zetu wa jadi kwa assistance wakati manguli wa kiswahili wenyewe tupo. Thanks I will give it a try as I want to make a difference sio lazima kuwa extra tu hata kusaidia when it comes to the language

    ReplyDelete
  25. Steven we admire you very much! I am a Nigerian fan!

    ReplyDelete
  26. Na mini nimeiona Fake Pastors. Ni kweli Tanzania tuko nyuma sana..TENA SANA. Halafu shida kubwa ni hii...tunajufunza kutoka kwa wa-Nigeria ambao sinema zao ni below standards. Yaani a 'poor rated..third world production' Story ni c average na acting kuwahurumia ni D-. Yaani mambo ya 'kibongo-kibongo'...kiingereza cha kibongo, set-up over-exagerated, muziki kelele tupu...shida kabisa!

    Kanumba is chasing his dream so please get off his ass and let's see what you have to offer!

    ReplyDelete
  27. Anonymous wa 7:12AM, na mimi nachukia sana nikisikia watu wanaongea lugha ya ajabu kwenye sinema halafu wanasema eti ni kiswahili. Kuna sinema moja niliangalia majuzi jamaa alisema, "buji buji buji" eti ni Swahili! Studios wanajua kuwa watu wanaotazama hawatajua kuwa siyo sahihi. Hata ile sinema ya The Color Purple iliharibiwa mwisho wale watoto watatu walikuwa wanaongea lugha tofauti. Yule Tashi (alichezwa na Mkenya) alikuwa anaongea Kiswahili,alisema, "Nafurahi sana kukuona mama nimesikia habari zako!"
    Kwanza ni heshima hivyo?
    Kwa zaidi ya miaka 10 nimeandika barua kwenye studios za kulalamika kuhusu authenticism za Afrika katika sinema. Naona siku hizi wanajitahidi kidogo wanatafuta language experts. Yupo mzungu moja Michigan(aliwahi kukaa Bongo) ambaye studios wanamtumia sana kupata ushauri.

    Pia nachukia kuona waSouth Africa wanacheza kama waGanda, hiyo kwetu sisi haiji kabisa, maana looks za waSouth Africa ni tofauti kabisa na looks za waGanda.

    Na siku hizi naona sinema nyingi wanajitahidi kupiga sinema location kama Kenya, na Mozambique. Zingine wanapiga Hawaii halafu wanasema eti ni Afrika! Na nimewahi kusema, Tanzania tufungue milango waje kutengeneza sinema maana dola zitaingia. Hela za kulipia locations, chakula, malazi, extras usafiri. Tanzania tusizubai! Na hivyo huko Kenya kumetokea vurugu basi siku hizi wanatazama Tanzania kama next frontier, lakini tuko ready kuwapokea?

    ReplyDelete
  28. Dada Chemi,

    Wheather some think he is a great actor, he is NOT, maybe he will later.

    If one make a proper analysis of all his works, he has a long way to go. Not in the language (I mean Kiswahili alone forgeting other languages he knows)

    Watanzania wenzangu, tusifikiri kuwa kwa sababu sisi hatufanyi uchambuzi yakinifu wa video/filamu zetu, na wengine hawazichambui.

    Sasa hivi kuna makala zimeandikwa kuhusu video za Tanzania na ubora wake, karibu zitajaa maktaba. Ukizisoma utashangaa jinsi watu wanakamata nondo kwa kuonyesha umbumbumbu wetu kwa dunia. Sisi tunabaki kupiga kelele ka wapiga debe badala ya kuandika na kutetea hoja kitaalamu.

    Some of his works have been analysed (even without a translator), they were rated poor in terms of

    1. Story line- they don't have any motive
    2. Body movement/diction/ emotions/gestures (hazielezi chochote)
    3. Camera appealing/photogenic (bado hajatulia mbele ya kamera)
    4. Creative acting skills (anatakiwa kujichunguza vipaji7hisia za ndani ili azijenge)
    5. Costume and make up (haziwiani na mlolongo wa hadithi)

    Kiufundi improvement should be on
    1. Sound (bado haina kiwango7kelele ni nyingi sana)
    2. Lighting (with no purpose)
    3. Camera use (creative/impossible shots should be designed)

    Ni mengi mengine nimesahau baada ya kusoma hizo ripoti

    Kitu kilichopewa alama/sifa ni mazingira/scenery, ingawa bado kuna mapungufu yanayotokana na uongozaji na matumizi ya vifaa

    What I can say, he can be an actor but not "KANUMBA THE GREAT" as he has dubbed hemself. Achilia mbali hao wakongwe wengine wa fani.

    Ushauri
    Afuate maelekezo ya washauri/wataalamu ambao kila kukicha wanajitahidi kumwelekeza wapi arekebishe ingawa yeye anaona kama tayari anajua kila kitu

    Watanzania, kuigiza kwenye filamu haukuwa utamaduni wetu. Tumekopa. Basi tujifunze kwa tuliowakopa, halafu tuweke manjonjo yetu ya kiasili

    Tanzania kuna wasanii wengi wazuri zaidi yake ila hawajimwambafy kama yeye.

    Najua kuna timu imekaa mkao wa kupinga hoja za kushauri uDenzel wa Kanumba. Mara zote kocha huwa hachezi, kwa hiyo usiulize waliochambua kazi za Kanumba wameigiza filamu gani

    Hivi sina kazi naanza kulumbana na THE GREAT...mmhh

    ReplyDelete
  29. Mimi nakubaliana na Dada Chemi kuwa Kanumba anasthaili kuitwa Denzel, kwa wingi wa sinema alizofanya. Je, kuna mwingine anayemfikia Tanzania kucheza kama mhusika mkuu? Huenda hakuna ubora ya kazi lakini uwingi upo!

    ReplyDelete
  30. Kanumba kafika Hollywood! Waliokuwa wanamwonea wivu walie tu! Kijana ana moyo kweli na sinema. Kweli yeye ni Denzel Washington wa Tanzania! Go Kanumba Go!

    ReplyDelete
  31. Nakuona Kanumba the Great umetua Hollywood. Sasa mbona hatuoni website ya John Wayne International Movie Awards. Pia umepata award gani?

    ReplyDelete
  32. Wakati Kanumba ameanza kuigiza michezo kwenye TV alikuwa mdogo na watu hawakutegemea kama angefika hapo. Kusema kuwa Kanumba ana maringo labda yaanze sasa baada ya kufika huko kwa wanaojua kuringa (US) maana huko watu wakifika hubadili kila kitu kuanzia lugha, namna ya kuongea na mengineyo, kwa kuwa walimu wapo naye labda ataiga (si tunawaona huku mitaani wanaotoka Marekani!) Na kuhusu ubaya au uzuri wa sinema alizocheza zinategemea story, muongoazaji, na bajeti ya sinema, hata huko kulikoendelea ziko sinema zilizo flop na zikawa rated vibaya. Na kuhusu sinema Bongo tangu kufa kwa ile taasisi ya sinema ya serikali iliyokuwa inasimamia filamu (kumbuka fimbo ya mnyonge, harusi ya mariam na nyinginezo) fani hii nayo ikafa. Sasa ndio imefufuka, na ndio kwanza tunajikongoja, mwanzo mgumu, na hatuwezi kuwafikia Nigeria, India au Europe na US sasa hivi we have a long way to go. Na tutafika huko tu iwapo tutapeana moyo na si kukatishana tamaa. Sioni ajabu mtu kuwa na aspirations za kutaka kuwa kama fulani kwani nayo ni malengo aliyojiwekea.

    Wako wasanii walionza kabla yake lakini yeye amejitahidi kuthubutu kutoka nje ya mipaka ya Tanzania, kuweza kucheza filamu na Wanigeria si jambo dogo. AMETHUBUTU! Kinachotukwamisha wengi ni woga wa kuthubutu angalia wanasoka wetu target yao ni timu ya taifa ya Tanzania, basi akishafika hapo karidhika anaogopa kuthubutu kushindana na wengine.

    Watanzania wenzangu tusifunjane moyo iwapo mmoja wetu ameamua kuthubutu nasi itapasa tuangalie wapi tunaweza kuweka ushindani kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu. Wakati nchi nyingine wako busy kutafuta opportunities na kuzitumia wao na jamaa zao sio tuko busy kupigana madongo na kubaniana, mtu hata kama kitu anajua yeye hawezi kufanya lakini yuko mtz anaweza hawezi kumwambia, kweli tutafika? Nakupongeza Da Chemi kwa moyo wako wa kuwaonyesha wengine opportunities kama huyo uliyemshauri namna ya kuwa extra.

    ReplyDelete
  33. Anonymous wa 11:17AM, asante kwa maoni.

    Mimi nina ujuzi na uzoefu katika fani ya sinema hapa Marekani na natoa ushauri kwa watu wanaotaka kuingia na wako tayari kusikiliza. Kuna waBongo na waKenya ambao nimewapa ushauri na wengine wamefanikiwa. Kuna faida gani ya kumwonea mwenzako wivu? Si bora afanikiwe labda siku moja huyo uliyemsaidia anaweza kukusaidia. WaNigeria na watu wa West Africa ndo wamekuwa na mafanikio zaidi Hollywood kwa nini na sisi kutoka East Africa tusifanikiwe sasa?

    Nachukia sana tabia ya waBongo na watu weusi kwa ujumla kupenda kuonea wivu wenzao. Akimwona anapanda ngazi hufanya juu chini kumvuta chini tena wawe sawa. Hebu mwone Obama na maneno mabaya amabyo weusi wanamwaga juu yake huko South Carolina.

    ReplyDelete
  34. mimi nadhani tumpongeze kanumba kuwa angalau amefika kwenye chimbuko la actors wengi wa kimataifa. However aelewe kwamba kufika tu hollywood hakutamsaidia chochote. Kama amekuja tu kama mtalii basi wenzetu mlioko huko wenye influence kama dada chemi msaidieni kijana angalau aonane na actors mbalimbali kwa lengo la kujifunza kitu fulani toka kwao. ikiwezekana aangalie uwezekano wa ku -further his career; nina maana atumie nafasi hiyo kutafuta shule kwani atafanikiwa zaidi kama atakuwa ni mtaalamu kwenye fani hiyo. keep it up kanumba ! where there is a will there is a way !!

    ReplyDelete
  35. Chemi! I don't know you personally but I respect you just like anyone else.

    In your last comments, I think you have mixed up things!

    I think something you have forgotten is "if you are in public domain then you have to accept criticism"...otherwise if you think you can't handle it (criticism) you have to find another life under the shell of the snail!...so, I'm afraid, whether you are "man of the god" or "politician" like Obama, you can't get away with it!

    Back to Mr Kanumba! Chemi,as a longtime and experienced journalist (I heard you are in USA!) you got all rights to tell the people around the world the truth about this chap!...is it true, Mr Kanumba is working in Hollywood right now as it has been publicized? or is just another visitor chasing unnecessary headlines in Hollywood buildings?

    Waiting to hear from you.

    ReplyDelete
  36. Naungana na Chemi kuhusu maoni yake aliyotoa. Sioni ubaya wowote kwa Kanumba kama ameenda huko Hollywood kutalii kwani huko kutalii kwake kunaweza kum-inspire akatamani na yeye kufika hapo siku moja. Ndio maana kuna study tours ambazo watu hutoka eneo moja kwenda kuangalia wenzao wa eneo lingine wamefanya nini. Hiyo nayo ni elimu tosha haina hata ulazima wa wewe uingie ukifanye kile uliwatembelea wanakifanya, lakini unajifunza kwa kuona.

    Labda nitoe mfano mdogo tu, huwa tunawapeleka vijana wa Sekondari vyuo vikuu ili wakaone huko kuna opportunities gani na wao waje wasome kwa bidii ili angalau nao siku moja wafike huko, na ni kweli wengi wanaweka malengo kuwa lazima na mie nifike chuo kikuu baada ya kuwa inspired. So wether Kanumba is on tour or working it doesnt matter kama yeye amefika hapo na somehow amekuwa inspired to fulfil his goals that fine. Iko siku maybe naye ataona jina lake hapo kama la SS kwenye hall of fame.

    Kwa Kanumba kama unasoma hizi message, maoni mazuri yachukue uyafanyie kazi na mabaya pia yafanyie kazi kwani yote yana mwongozo ukiyaangalia in a positive way. Usife moyo huu ni mwanzo tu utakuna na mengi zaidi ya haya follow your dreams & work hard to achive them na elimu haina mwisho, jifunze na ujifunze na ujifunze hata maisha pia ni sehemu ya elimu.

    ReplyDelete
  37. JAPO UMEICHUNIA COMMENT YANGU NILIOACHA JANA KUHUSIANA NA PARA HII "Nachukia sana tabia ya waBongo na watu weusi kwa ujumla kupenda kuonea wivu wenzao. Akimwona anapanda ngazi hufanya juu chini kumvuta chini tena wawe sawa..." BADO NAAMINI NILICHO-COMMENT KILIKUWA SAHIHI.ANAYEKWEPA KUKOSOLEWA ANAWEZAJE KUWA MSHAURI MZURI?

    ReplyDelete
  38. Anonymous wa 4:05PM asante kwa maoni. Ukweli siwezi kumshauri Kanumba akaonane na actors wengine kama nia yake ni kutafuta kazi za acting. Lazima uelewe kuwa nao wanatafuta kazi pia. Ila naweza kumshauri akaonane na agents, producers, directors etc. Hao actors wanaweza kumsaidia tu ku-share experience.

    Anonymous wa 8:39AM ulitaka nikujibuje?

    ReplyDelete
  39. Da'Chemi amesema ukweli. Watu weusi hatupendani habu soma comments hapo juu! Watu wanamkashifu Kanumba ile mbaya kwa vile wao hawajafika alipofika yeye. Tuna wivu sana.

    Mimi namsapoti Kanumba na nategemea kuona akina Kanumba wengi maana vijana watafuata nyayo zake!

    ReplyDelete
  40. Chemi huyo anayesema kuwa ulimchunia kuhusu ushauri wake na alichosema ni sahihi. Ana uhakika ni sahihi? Pengine ni sahihi kwa malengo na mtazamo wake lakini si lazima tukisemacho na kuwashauri wenzetu kiwe sahihi. Lazima tufike mahali tuone kuwa mawayo yangu yanaweza kuwa sahihi kwangu lakini yasiwe sahihi kwa mtu mwingine. Unapompa mtu ushauri si lazime aufate naye anahaki ya kuuchuja kuona kwa mtazamo wake kipi mchele na kipi pumba.

    Mie sijawahi kuwa sahihi tangu nizaliwe na siwezi kung'ang'ania kuwa nikisemacho mimi ni sahihi kwa sababu binadamu tuko tofauti. Tunatofautiana mawazo, fikra, mapendekezo, vitu tunavyovipendelea, utashi na mengineyo. Usahihi wa 100% ni wa muumba peke yake, wengine wote tuliobaki hatuna sifa hiyo. Hivyo basi mheshimiwa waweza ona kwa mtazamo wako uko sahihi lakini kwa mtazamo wa wengine hauko sahihi kama ambavyo unavyoona mitazamo ya wenzio sio sahihi. Kizungumkuti eeh! Ndivyo maisha yalivyo na ndivyo inavyobidi tuishi kwa kukubaliana au kutokubaliana kistaarabu lakini bila kugombana!!!

    ReplyDelete
  41. We anony wa 11:18 utakuwa na matatizo kama hujawahi kuwa sahihi tangu uzaliwe.Na sikubaliani nawe kwani usingekuwa sahihi (ie unakosea ktk kila unachofanya) usingeweza hata kuandika hicho ulichoandika,maana badala ya A ungeandika X (unless what you meant to say was you have not always been right,which is common as almost every human being does).

    Haya,Denzel Washington wa Bongo ameanza kujimwagia ujiko.Da Chemi,tusaidie japo kupata picha za tukio hili.Nanukuu kutoka Globalpublisherstz.com "
    Kanumba amwaga chozi
    risasi mchanganyiko
    ....Kanumba aliwasiliana na mwandishi wetu kwa njia ya barua pepe alisema kuwa, amefurahi sana na hakuamini macho yake alipotembea juu ya red carpet (kapeti jekundu) kupokea tuzo hiyo.

    “Kaka nina furaha sana usiku huu wa leo, nimepewa tuzo nyingine kama Best Tanzania Achievement Actor yaani muigizaji mwenye mafanikio kutoka Tanzania iliyotolewa na Kampuni ya Universal Hollywood, nimetembea juu ya kapeti jekundu huku machozi yakinitoka, kusema kweli siamini kilichotokea,” alisema Kanumba.
    Alisema mara baada ya kumaliza zoezi la kupokea tuzo, waliandaliwa sherehe ya nguvu kwenye Ukumbi wa Aqua Lounge, Los Angeles ambapo ilihudhuriwa na mastaa kibao wa Hollywood.

    Msanii huyo alisema kuwa, kwa muda mfupi aliokaa huko amejifunza mengi na ameweza kujichanganya na baadhi ya mastaa wanaoigiza sinema za kutisha duniani kama anavyoonekani akiwa amepozi nao kwenye picha ya ukurasa wa mbele.
    Hii ni tuzo ya pili kwa msanii huyo kutunikiwa kutoka Marekani ambapo ya kwanza ni ya Johnwyne International Award.
    Kanumba yuko nchini Marekani kwa takriban miezi mitatu sasa kwa mwaliko wa Kampuni ya Johnwyne ya Hollywood..."

    Nimejaribu ku-google ku-authenticate stori hiyo lakini sijaambulia kitu.Da Chemi,kazi kwako.

    ReplyDelete
  42. bwana kanumba mimi sikufahamu lakini nimesikia tuumke\wamaba umecheza kenye video nyingi (ofcourse za ubora wa chini ) za hapa nyumbani .ninasema kanaumba hongera siyo kwa sababu eti umekwenda kutalii hollywood au japo kuona tuu taasisi ya utengenezaji sinema ya marekani ,na ya dunia pia ninakupongeza kwa sababau kufuatilia maoni ya wengi waliozifahamu kazi zako ni wazi kwamba umejitahidi kuliko wengine hapa nyumbani.kanumba usikate tamaa ndio bado una mapaungufu ya kiutaalamuktk uchezaji wako sinema
    lakini kama utaendela na fani yako na kukubali kubadilika yaani kujifunza utafika mafanikio makubwa sana kuliko hata unavyofikiria .mimi nakupa heshma kwa sababau walau umjitoa muhanga na kunza shughuli za uchezaji sinema je ni wangapi ambao huishia kusema tuu miaka yoote na wasifanya hata kazi moja tuu ya mfano na sisi tuzione kama vile kazi zako tunazoziona?
    haters ni wengi sana ktk society ya watanzania popote pale walipo
    lakini brother usikate tamaa tena weka pamaba sikioni
    endelea ku-endeleza fani yako acting hasa hapa marekani ni fani moja yenye ukatishaji tamaa wa hali ya juu lakini cha kujiuliza kanumba akina djimoni hansuh,vandame,schwaznegar,jacki chan,antonio benderas,thandie newton, hao na wengine wengi tuu amabao si wazawa wa marekani wamewezaje? wao ni binadamu kama wewe na ni wasnii kama wewe mwanangu kaza buti ,utafika siku moja.japo kuwa ni vema ukafahamu kuwa hollywood ni pagumu mno lakini wanaotaka kuwa wanakuwa bila kujali ni wapi asili yao.ebu angalia historia ya maisha ya hao niliowataja hapo juu halafu utafakari hadithi zao kwa kweli zinafurahisha sana na zina tia moyo

    anachosema chemi ni ushauri mzuri tena japokuwa mimi binafsi simfahamu lakini inaonekana ni msanii wa mtazamo endelevu wa nje ya box yaani ule wa kiglobal kila aina ya mtu kanumba anasehemu yake hoolywood hata kwenye film industry ya nyumbani pia hivyo usikate tamaa wewe kaza buti
    mtafute chemi kama wewe ni mchezaji(actor) nina uhakika anaupeo mkubwa sana kiufundi not necessarily kitaaluma ktk mambo ya uchezaji i can guarantee hilo atakupa ushauri mzuri kiufndi na endelevu

    cha msingi
    usijione kwmba unajua wewe kuwa open minded kubali kwamba hujui ili usaidiwe lakini sio na kila mtu

    sinema takataka (nigeria)
    kanaumba nakupa ushauri wa bure kama unataka kujifubza na kuendela achana na video mbofu za nolly wood kwa maoni yangu hazitakujenga kiundelevu bali zitakujenga kurudi nyuma na kuanguka kiusanii kama unatafuta mentua au sehemu ya kujifunza kwa afrika mimi nashauri angalia sana kwa wasouth afrika !
    lakini daima jifunze kutoka hoolywood productions. holly wood ni pinacle ya sanaa za utengenezaji sinema duniani

    rahisi
    njia moja wapo rahisi ya kujifunza acting ,ukiachia njia kadhaa zingine amabazo ni conventional, ni kuangalia sinema nyingi sana za hollywood,tena repeatedly
    unapongalia kuwa na malengo ni kitu gani hasa unachunguza ikiwezekana nunua vitabu vyenye scripts za sinema hizo kisha uangalie shot by shot scene kwa scene repeatedly if possible ni jinsi gani mchezaji alivyoweza kujivika na kumtoa character anayemwigiza na akakubalika kwa kiwango kwamba watazamaji kama mimi na wewe tunaona hii ni kweli na kwamba siyo suala la kuigiza!
    pia ktk hili fanya majaribio ya kuangalia sinema moja ikiwa na sauti kisha angalia hiyo hiyo ikiwa bila sauti hii itakusaidia kuona ni jisi gani acting inavyomake sense hata kama sauti hakuna ukiachilia mbali suala la editing na factor zingine zinzofanikisha sinema

    misifa ya uongo /kiunafiki
    watanzania kwa maoni yangu tunatabia na utamaduni wa unafiki wa kusifia jambo na hali jambo lile kihalisi halina ubora wowote ule eti kwa kuhofia kwamba si kiungwana kumwambia mtu ubaya au mapungufu yake ,hivyo weni wa watanzania huamua kusifia jambo hata kama jambao lile lina mapungufu yenye athari kubwa sana kwa jamii na yenye kustahili ya kusemwa hadharani tukifikiri kwa kufanya hivyo eti tunakupa moyo ,
    huu ni utamaduni wetu ulioota mizizi na itatuchukua muda sana kuutupilia mbali kwani hauna maana
    mfano mdogo tuu mtu akifa kwa kawaida sisi watanzania hupendelea kusema mazuri tuu na misifa kibao ya unafiki ya marehemu na japo mioyoni tunayajua maozo yake ambayo labda yangesemwa wazi either jamii inayomzunguka,ndugu na wengine basi tutapata nafasi ya kujirekebisha au kutatua tatizo la aina hiyo la marehemu
    nina maana kwamba humu kwenye blog kuna watu wengi tuu wametoa ukosoaji ,don get me wrong ,sizungumzii haters! no! ukosoaji ,kanumba usome ukosoaji huo kwa furaha tena shangilia ,hivyo ndio wanakuimarisha na epuka sana sifa zetu sisi watanzania tunazo kupa

    Denzel
    nakushauri binafsi uache kujiita eti wewe ni denzel wa tanzania huu ni utamaduni mwingine mkongwe wa kujinga ,kishenzi na wa kiunyonge usio wa maendeleo na wenye upeo finyu
    tumia jina lako na achna na mambo ya kijinga ya kujiita the great ingawa endelea moyoni mwako kuamni kuwa siku moja watu sisi tutakuita the great kutokana na kazi yako iliyokuwa nzuri
    hujiulizi kwa nini denzel mwenyewe ahjawahi kujiita sidny poitier wa atlanta ,au chicago nk au kwa nini hakujiita morgan freeman wa mahala fulani wakati alipokuwa anahangaika bado hajakuwa star
    Au mbona hata chemi asijiite queen latifah wa chicago.... nk
    kiprofeshenali nakushauri acha kasumba hiyo
    tumia jina lako

    lugha
    kanumba hao wenye kucheka lugha wasikutishe bwana kama wewe unakipaji lugha hua haionekani je unajua siri anayofanyiwa antonio benderas ili aweze kuzungumza kimarekani ktk sinema?
    na wengine wengi tuu wasiojua english ya kimarekani vyema
    JE UMESOMA HABRI ZA DIRECTOR ALIYEDIRECT SINEMA YA WILL SMITH
    INAYOITWA PURSUIT OF HAPPINESS?
    SOMA NDUGU YANGU hapao itakusaidia kukupa moyo kwamba lugha haifui dafu mbele ya kipaji ,japokuwa sio wakati wote
    kanumba kaza buti unjitahidi ,bado unanjia ndefu sana na kwa ujumla industry nzima hapa nyumbani
    hakuna aliye mkamilifu asilimia 100 soote tunaanzia mahali fulani
    maoni yangu ni kwamba unjitahidi no doubt.

    Raceznobar

    ReplyDelete
  43. Huyo anayekandia sinema za kinaigeria nani? Sinema za kinaijeria mbona ni nzuri sana? Ingawa sio zote! Kwa upande wangu mie naona pia si vibaya kwa kanumba kujifunza kupitia sinema za wanaijeria. Wametutangulia... hilo tulikubali!

    ReplyDelete
  44. Mmmh, Mimi sina matatizo na kanumba kwa kipaji chake kwani nilianza kumwona tangu akiimbia ile choir ya kanisani mpaka alipotimuliwa baada ya kuonekana anakwenda na mambo ya kidunia. Nashukuru hakukata tamaa akaendeleza kipaji mpaka hapo alipofikia.
    Tatizo langu kubwa ni huo UDanzel Washington aliojipa! Bado najiuliza hivi jina lake linamatatizo gani kwa nini asijiite KANUMBA WA TANZANIA? Kuliko kumtangazia biashara msanii mwenzake. Najua sana kuwa anapenda awe kama Danzel, lakini si kwa kutumia jina lake. Seven Kanumba hilo ni jina lako na unatakiwa ulitangaze lijulikane.
    Mimi naamini unakipaji cha msingi ni kuwa serious na fani ufikie malengo yako.
    Nimeona Senema zako nyingi nimeona unajitahidi sana wewe kama msanii na si kama mwandishi, mpiga picha, au mwingine yeyeto aliye nyuma ya kamera.
    Keep it up! accept challenges and find mitigation strategies to overcome.

    ReplyDelete
  45. Kwa kweli nimekubali wabongo hatupendi maendeleo ya mtu.Jamani huwezi kulinganisha Tanzania na Marekani katika uwanja wa maendeleo.Tanzania ni nchi masikini lakini inajitahidi inavyoweza.Inapotokea yeyote anajitahidi kufikia hatua flani,tukubali kajitahidi katika nafasi hiyo.
    Namanisha Kanumba hawezi kulinganishwa na wazoefu wakubwa wa kuigiza ambao wako katika nchi zilizoendelea.Lakini kwa hapa hapa Bongo Kanumba yuko juu na ndani ya afrika anapiga kazi wazee.Anajitahidi sana kuigiza, kinachotakiwa tuwape support na kuwaunga mkono.Tunaweza tukiwezeshwa sasa tuwawezeshe hawa wasanii wetu.
    Lakini tukizidi kukatishana tamaa hatutafika mbali.
    Ushauri:
    Wasanii wa kibongo tumieni majina ya kibongo tuitangaze nchi yetu.You should be pround of your country and not otherwise.Mbona wazungu hawatumii majina ya kwetu, bali sisi tunawaiga kila kitu.Acheni hizo jamani.
    Nyumbani ni nyumbani lazima tupapende na kupatukuza
    BIG UP KANUMBA NA WASANII WENGINE,KAZENI UZI MTASONGA MBELE
    siboditz@yahoo.com

    ReplyDelete
  46. Kanumba anatufanya watoto wadogo. Hakuna John Wayne International Award! Pia hajapata award majuzi huko Hollywood eti kutoka Universal Studios! Kama kapata ni nani waliopata kutoka nchi zingine? Kanumba msanii kweli!

    ReplyDelete
  47. jamani mbona mna leta mas-hara ktk
    kazi na vipaji vya watu
    na lazima mfahamu comparason inayo zungumza ni ipi
    kwani kuna kuji fananiza kwa aina nyingi pengine Kanumba ana jifanani na Dezel Washington ktk mwendo au kutembea , if so , that fine , nikama watoto wabongo wanavyo muigizia Joty au Ami jey kwa miondoko . lakini sio kimambo mengine

    ReplyDelete
  48. Hatimaye DENZEL WASHINGTON wa TZ aonyesha "TUZO" yake....link hii hapa
    http://abdallahmrisho.blogspot.com/2008/01/kanumba-alamba-tuzo-nyingine.html

    Kuna mtu anasema anastahili "nickname hiyo" kwa vile ameshiriki movies nyingi za Kibongo,labda hiyo ni sahihi kwa mtazamo wa anayeshauri hivyo,lakini kwa tabia hii ya ku-fix watu na tuzo feki....Watetezi wa Denzel wa Bongo mko wapi?Can someone please ask Kanumba kuilinda hadhi yake kwa kuepuka upuuzi anaoufanya huko kwenye magazeti ya udaku?Ni rahisi kudanganya kuhusu tukio la kawaida linalodaiwa kutokea Dar,lakini ni vigumu kudanganya kuhusu tukio "la Kimataifa" lililotokea mahala kama Hollywood "na kuhudhuriwa na mastaa kibao".Au Google na search engines nyingine nazo zina wivu na Kanumba?

    ReplyDelete
  49. Kanumba Mungu atakusaidia na ndoto yako ya kucheza Hollywood siku moja itatimia. Kufika Hollywood japo kutembea ni hatua kubwa sana, tena sanaaaaaaa. Wangapi wamecheza sinema hawakuweka malengo yako?

    Kaza buti kaka, wacha wanga waseme kila mtu ana malengo yake wewe kaa hollywood kimasomo au kikazi ni malengo yako, Kanumba yupo hollyhood kuangalia maswala ya sinema ni malengo yake. Huwezi kumsifia lala usingizi wote mliomponda Kanumba, better go for medical checkup as soon as possible before 13th Febr.2008

    Hakikisha malengo yako yanatimia kijana, usivunjwe moyo na yeyote yule.

    Nakutakia kila la Kheri

    ReplyDelete
  50. Kweli huu upuuzi!!!!Huyu Kanumba ambae aliulizwa idol wake nani akasema Ramsey kweli mnamuita Denzel nyie wazima ghorofani???...

    Eti kigezo kaigiza movie nyingi!!Basi muiteni Mel Blanc au hata Adoor Bhasi.Denzel hasifiki kwa kuigiza movie nyingi bali kwa kuwa muigizaji mzuri thou proven wrong in action movies....

    All i would add is no matter wat name u'll brand all critisizing the use of such a nick to Kanumba or whoever doing michezo ya kuigiza kwa kivuli cha sinema mtakuwa hamkubali ukweli tu....

    There might be a future for many in Hollywood lkn wengi wa waigizaji wenu wa bongo wanafit maigizo yao hayo hayo not otherwise...

    Haihitaji utaalam kujua mtu anapotakiwa aoneshe ameumia wakati hajaumia anatakiwa awe katika hali halisi ya maumivu,kama hujaliona hilo wahitaji jicho la tatu......

    Ntamaliza na hii kwamba Kanumba anaweza kuwa anafit kwa michezo ya kuigiza ila anazaidi ya maili 10000 kufikia milestone yake,ukichukia chukia tu kanumba hana cha kufanya nimbanie zaidi kumhurumia kwa sababu ule ndo ugali wake.Period

    ReplyDelete
  51. kwa kweli mimi binafsi nimesikitishwa sana na muelekeo wa habari hii ya kanaumba
    sababau inadalili zinazoanza kuonyesha kama vile amedanganya .kwa kweli nitasikitika sana kama haya mambo anayotuambia ni ya uongo.
    sijui ,labda ni mapema sana kusema au kuhitimisha ktk suala hili
    aibu na inasikitisha sana

    ReplyDelete
  52. Dada chemi, plse tell me about the hollywood walk of fame.

    ReplyDelete
  53. Anonymous of 11:47Pm, The Hollywood Walk of Fame is in Los Angeles, California. You actually have to be nominated to get a star there and it is for people who have worked in the film industry.

    If you are referring to the picture with my name on it, that is something I created from a website. Anyone can do that. It would be nice if one day I could have a real star there... God willing!

    ReplyDelete
  54. Mimi ni mwanaume na mpenzi mkubwa wa sinema za huyu jamaa. Nadhani ndio actor pekee ninayemfahamu kutokea Tanzania. kinachofurahisha tu ni kwamba kama mnasema jamaa anawavutia basi najua pia tuko wengi ambao tunaweza kuwavutia pia

    ReplyDelete
  55. Clearly "Talent" is something that is far fetched in this fellow's work. Having the lead role in a self written, self directed, self produced low budget (or maybe no budget) film is not exactly what people would call having talent; least to say skill.... do something else Sir... you and your fellow "Tanzanian celebrities" are going a great job at mocking the entertainment industry and the nation... word of advise.. have you thought of indulging in large scale agriculture... or rather compost manure production... coz you full of it!

    ReplyDelete
  56. Aminadab Havyarimana haminadab07@yahoo.frDecember 20, 2011 1:25 PM

    Kanumba asonge mbele! Anastahili sifa! Ni mkubwa sana, ana uezo! Turamushigikiye kandi turamukunda/ we support him and we love him!

    Wenye fitina wakubari au wakatae!

    ReplyDelete
  57. Mr.Kanumba sir,am from Kenya and I watch your movies once in a while.You are a greater actor though there is a problem with the flow of your movies.....then my brother the translation is just terrible.misspelling of words is so common and I think for non swahili speakers it's becomes difficult to really get the flow.

    ReplyDelete