Tuesday, February 05, 2008

Leo ni Super Tuesday! - Nani atagombea Uraisi wa Marekani!








Leo mamilioni ya waMarekani wanajitokeza kupiga kura. Wanaiita siku ya leo, Super Tuesday. Kura wanaopiga leo zitasaidia kuchagua nani atakuwa mgombea rais kwa upande wa Democrats na upande wa Republican.

Kwa upande wa Republicans waliobaki kugombania nafasi ni Mike Huckabee, John McCain, na huyo mshenzi/mnafiki alikuwa Gavana wetu hapa Massachusetts, Mitt Romney.

Kwa upande wa wa Democrats waliobakia ni Hillary Clinton, na Barack Obama. Kuna mashindano makali sana kati ya hawa wawili. Wote wana wafuasi wengi. Huenda leo hatutajua nani kapita upande wa Democrats na itabidi tusibiri hadi siku ya Convention (mkutano mkuu wao), itakayofanyika mwezi wa nane huko Colorado.
Nadhani kuna chensi kubwa kuwa Democrats watanyakua White House safari hii. Watu wamechoka utawala wa Bush. Wanasema ameharibu nchi na hadi yake, pia kaanzisha vita isiyo na maana huko Iraq. Pia hali ya maisha kwa Marekani umekuwa mbaya, watu wanfukuzwa katika majumba yao, bei ya mafuta umepanda, hata bei ya chakula umepanda mno!
Bush aliwaahidi waMarekani kuwa kama atakuwa Rais bei ya mafuta utashuka. Wakati huyo ni kama $1.80 a gallon. Leo ni $3.10! Wajinga ni nani! Hao waliompigia kura Bush kwa hasira wanaweza kupiga kura zao kwa Democrats! Warudishe hadi ya nchi ilivyokuwa enzi za Rais Clinton!

May the Best Man/Woman win!

1 comment: