Nilitoa hapa kwenye blogu kwa ya kwanza, January 3, 2006.
Baada ya kuandika kuhusu matako makubwa, na kusoma feedback yenu, nimeona niongee kuhusu mashindano ya urembo. Asante kaka Ndesanjo kwa kunichokoza!
Hivi karibuni Miss Tanzania 2005, Bi Nancy Sumary alienda kwenye mashindano ya Miss World na kafanikiwa kutwaa taji la Miss Africa. Kwa kweli lazima nimpongeze maana toka mashindano ya Miss Tanzania ifufuliwe miaka ya 90, hakuna Mtanzania aliyefanikiwa kuingia katika raundi za fainali na hata kutwaa taji lolote.
Kwa kweli Tanzania imepata sifa kubwa katika dunia ya mashindano ya U-Miss. Pia Tanzania imepata sifa kuwa ina wanawake wazuri, lakini nauliza ni uzuri wa aina gani? Maana sioni kama ni uzuri unayafuata maadili ya kiafrika bali ni uzuri wa kizungu!Nikitazama picha na kanda za video za Miss Ilala, Miss Kinondoni, Miss Utalii, na mashindano mbalimbali za u-Miss huko Tanzania nashangaa nachoona. Kwa kweli naona wasichana weusi wakijaribu kuiga wazungu!
Wengine wanapaka make-ups usoni ambazo zimetengezwa kwa ajili ya wazungu wakati make-up za weusi zipo. Yaani ni vichekesho mpaka wengine wanaonekana vituko. Najua hapo niatambiwa nawaonea wivu lakini si kweli na naomba mnisikilize kabla ya kunipa hukumu.
Kwanza tutazame hao wanaopelekwa na nchi zao katika mashindano hayo. Ukiangalia walio kwenye Miss World na Miss Universe, washindi wote wana hulka (characteristics) za kizungu. Tutazame waafrika wanaoenda, cheki nywele zao, zinafanana na wazungu, yaani zimenyoka kabisa. Na kama tunavyojua, sisi wenye asili ya Afrika nywele zetu ni za kipilipili. Hawa wanaweka dawa au weave! Wanaficha nywele zao za asili, sijui wanazionea haya.
Je, wanaona haya kusuka nywele zao au kuonyesha mtindo wa nywele enye asili ya Afrika?Haya, tutazame shepu zao, wote ni wembamba, hakuna mnene, hata hips za maana hawana. Na kama ana matako ni kiasi, sio ile boxi, wowowo, yokohama inayopendwa Africa. Yaani wanafanya mazeoezi eti kusudi wapunguze matako yao.
Na hao weusi kutoka Marekani na Ulaya wanafanya liposuction na surgery kupunguza matako yao asili, eti iwe ya kizungu fleti. Huko Afrika tunasema mtu mwembamba ana shida, hana raha, mgonjwa, lakini mzungu anasema ni uzuri. Na sisi tunaiga! Basi unakuta akina dada hata Tanzania, “Oh nafanya diet!” Kheh! Kisa anataka kufanana na mtu amliyemwona kwenye gazeti.
Hawajui kuwa hizo picha zinafanyiwa editing na air brushing. Kwa hiyo dada zetu wanashinda njaa kusudi wawe wembamba! Hawajui kuwa hao wanaofanikiwa kwenda kwenye u-Miss, wanajitapisha, na kujinyima chakula kusudi wasinenepe, na ukweli hawana raha.
Haya tuangalie wanavyotembea na kuongea…wanaongea na kutembea kizungu! Jamani na hata macho hawasahau, maana wanatia contact lenses zenye rangi ya bluu na kijani kusudi wawe na macho ya kizungu! Doh! Matokeo ni kuwa hao siyo watu tena bali na madoli.
Na kuhusu rangi ya ngozi, ni lazima niulize, je, umewahi kuona mshindi mweusi tii? Hao weusi wanaofanikiwa wengi ni weupe. Basi hao dada zetu wanajichibua na madawa ya ajabu. Ubaya ni kuwa usoni wanaonekana weupe lakini miili yao bado rangi yao ya asili. Mwisho wanakuwa na rangi mbili. Halafu wengine baadaye wanajikuta wana kansa ya ngozi shauri ya dawa hizo za kujichibua.Ubaya ni kuwa kama nchi ya kiafrika inataka kushinda mashindano kama Miss World, Miss Universe ni lazima mtu wao awe Mdoli wa kizungu.
Mfano, miaka mingi Nigeria walikuwa wanapeleka mrembo wao ambaye alikuwa mrembo Nigeria lakini mbaya kwa wazungu. Mwaka 2001, waliamua kumpeleka Mdoli wa kizungu, yaani dada fulani, mwembamba, futi sita na kashinda. Na tazama kesi ya aliyeshinda Miss Universe 1996, Miss Venezuela, Bi Alicia Machado…baada ya kashinda, alinenepa kweli! Yaani aliongezeka kama kilo 20! Basi majaji wakasema watamvua taji lake kama hatapungua! Dada wa watu alilia na kusema kachoka kashinda njaa!
Na tuanganlie hatima ya hao wanaoabudu hiyo standard ya kizungu na kuwa wembamba. Wanapambana na magonjwa kama Osteoperosis, yaani ugonjwa wa mifupa kuvunjika kwa urahisi, utapialmlo, na magonjwa wa akili. Ndiyo, mtu ambaye kila saa anawaza kujikondesha na kuwa hatapendwa kama si mwembamba ana ugonjwa wa akili.
Je, madaktari huko Tanzania wako tayari kutibu hayo magonjwa wa kisasa?Mashindano ya U-Miss yataendelea kuwepo, na dada zetu wataendelea kutaka kushindana na kufanana na madoli wa kizungu. Bahati mbaya ndo dunia ya leo. Lakini napendekeza tuwe na mashindano ya Miss Bantu, Miss Tanzania asili pia. Mashindano hayo yawe na nia ya kusifia uzuri asili wa mwanamke wa kiafrika. Tusisahau tulikotoka. Na hao wazungu wakiona tunajipenda basi wao wataanza kuheshimu maadili zetu.
UPDATE - Flaviana Matata aliwakilisha Tanzania kwenye Mashindano ya Miss Universe 2007 na kufika kwenye Top 10. Bado wanamzunguzia.
mambo yote "bantu" figure jamani !!kama alivyo da chemi mwenyewe "big boobs" and "big bum" !! da chemi ungekuwa hujaolewa mimi nimekulilia hata kwa machozi ya damu, duuu unalipa mama !!!
ReplyDeleteNi kweli kabisa chemi hakuna cha wivu wala nini!!wazungu walituharibu sana kwa kutuhuburia kuona chochote cha mtu mweusi hakifai!kudhani kwamba wanawake wa kizungu ndio wazuri wenye shepu nzuri haina maana na ndio tunavyoonyeshwa kila siku!!!mimi mwenyewe naona asilimia kubwa ya kinadada weusi sio wote wako busy na kutaka kuwa wazungu!!inashangaza sana.watu weusi na waafrica wote inabidi tuamke tujikubali kwamba vya kwetu navyo ni vizuri ndipo na weupe watatuheshimu bila hivyo watazidi kutudharau na kutucheka mpaka mwisho wa nyakati..
ReplyDeleteDa Chemi,
ReplyDeleteLazima nikupongeze pale penye kupongezwa, ila kwa mdau wetu Obama ulichemsha. Ok tuondoke kwenye obama tuje kwenye issue hii.
Kwa kweli Da Chemi mimi binafsi nikoconcern sana na hii trend inavyokwenda ya kuiga mambo ya watu, bila kuwa na ubunifu wetu wenyewe watanzania, na hicho kinanisikitisha.
Wakati mwengine nafikiria hivi sisi watanzania tunayosense ya imagination na ubunifu kwa ujumla kama tunavyoona kwenye nchi nyingine.Mwana blog Metty-reflections amejaribu kuyaongea sana maswala haya ijapokua amekua lay way to the right to the issue kiasi ya kwamba anainsult watanzania wengi kwenye tone na uandishi wake juu ya mentality za Watanzania kwa ujumla.
Lakini kuna mambo na baadhi ya issue sisi watanzania tunafuata mkumbo blindly bila ya kuwa na fikra na upeo wa mbali wa kile tunachokifuata.
Je hii inatupelekea kwamba sisi watanzania tunajitambua kama ni watanzania wenye hulka na tamaduni zetu, au tuko katika wimbi la cultural and social globalisation, ya Mzungu ni yetu, ya Mmarekani mweusi ni yetu, na ya Mtanzania ??? ni yetu. Sitaki kuwa philosophical lakini tuangalie sana Watanzania tunapokwenda na mitindo ya kuiga bila kutambua kile tunachokiiga.
Ni hayo tu kwa leo nawakilisha.
By Mchangiaji