Thursday, February 21, 2008

Update - Jambo Forums


JAMBO FORUMS


Jioni ya leo (February 20, 2008) kwenye kipindi cha BBC mara baada ya Mwanakijiji kuhojiwa, alifuatia Msemaji wa Jeshi la Polisi ambaye alijaribu kuelezea ni kwa nini vijana wawili wanashikiliwa na Polisi kwa sababu ya kuhusika na mtandao wa Jambo Forums. Katika madai ya jeshi hilo ni kuwa mtandao huo siyo tu ni wa uchochezi bali pia unamawazo ya kigaidi au uvunjaji mwingine wa sheria.

Tafadhali ingia kwenye "Pics and Docs" kwenye "Press Releases" na kujisomea tamko hilo pamoja na makala iliyowatambulisha watu wengi kwenye Jambo Forums iliyotolewa karibu mwaka mmoja uliopita na kuwekwa hapa bila ya kufanyiwa uhariri wowote au mabadiliko.
Wakati huo huo tunaitisha michango ya wana JF katika kuwasaidia ndugu zetu. Wengine tumetoa muda wetu, watu wawili tu wamechangia fedha kidogo na wengine wanaendelea kutoa michango ya "maneno ya kizalendo" na mshikamano.

Tunahitaji michango ya kuhakikisha siyo tu JF inarudi bali inarudi ikiwa na nguvu zaidi lakini pia kusaidia juhudi za ndugu zetu nyumbani. Endapo vijana hawa watafunguliwa mashtaka tunahitaji kuwa na "Legal Defence Fund".

Michango inaweza kuingizwa kupitia tovuti hii au kwa kuwasilina na klhnews@klhnews.com This e-mail address is being protected from spam bots, you need JavaScript enabled to view it .
Mwisho tunaomba kuwahakikishia kuwa Jambo Forums iko salama kabisa na kila kitu kilichokuwapo bado kipo na muda si mrefu itarudi hewani.

Ndugu yetu "Invisible" anaendelea kufanya vitu vyake bila kubughudhiwa na matukio yanayoendelea.

1 comment:

  1. Tehehehe! Watu wanaogopa kuwa Pindarized wakicomment juu ya Jambo Forum.

    ReplyDelete