Tuesday, March 04, 2008
Sinema - The Ghosts of Girlfriends Past
Jana nilikuwa 'extra' katika sinema, 'The Ghosts of Girlfriends Past'. Mtaa wa Downtown Crossing, Boston uligueuzwa mtaa wa Manhattan, New York. Tulishuti, mtaa wa Temple Place. Kwa wanaojua Boston, Temple Place ni mtaa ule ambao mabasi ya Silver Line kwenda Roxbury yaana anzia. Ukipinda kona unaona jengo la Macy's. Walikodi polisi wa kuzuia trafiki kila wakipiga take.
Role yangu - nilikuwa naenda kuhudhuria mkutano fulani. Tulipewa cues na namba za kuanza action. Sasa kwenye rehearsals, nilikuwa sifiki kwenye mlango wa ofisi kabla kamera imefika mlangoni. Kamera ilkuwa kwenye dolly (ni kama reli). Halafu ubaya nilikuwa nimevaa viatu vyenye visigino virefu (high heels) halafu tulionywa tusianguke kwenye hiyo doli! Loh! Hazards of the Trade!
Kwenye hiyo scene, nilikuwa mweusi peke yangu, sasa second director alitaka kunitoa kwenye scene, director kamwambia kuna ananitaka kwenye hiyo scene. Basi walichofanya ni kumtoa mwanaume wa kizungu ambaye alikuwa ananitangulia. Basi hapo niliweza kuwahi kufika kwenye mlango kabla ya kamera. Tulipiga teki kama kumi na tano. Nangojea kuona kama nitaonekana hata kama ni kwa sekunde moja.
Ghosts of Girlfriends Past inahusu jamaa anayeenda kwenye aruis ya kaka yake, halafu akiwa huko anatembelewa na mizimu ya wasichana ambao amewahi kutembea nao. Navyoona ni kama ile hadithi ya 'A Christmas Carol', inayomhusu yule mchoyo Mzee Scrooge.
Stelingi wake ni Matther McCounaughey, Jennifer Garner na Michael Douglas. Hatukuwaona jana.
No comments:
Post a Comment