Saturday, April 26, 2008

Miaka 44 ya Muungano

Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, akichanganya udongo wa Tanganyika na Zanzibar kama ishara ya muungano rasmi, April 26, 1964. Siku hiyo Tanzania ilizaliwa.

*****************************************
Wadau nawauliza hivi - huo udongo uko wapi?

Mnahabari kuwa jina la Tanzania ilipatikana katika mashindano. Watu waliombwa wapeleka majina ya nchi mpya. Tanganyika + Zanzibar. Karibu tuitwe TANGIBAR!

Leo namwomba Mungu kuwa tuendelee kujivunia uTanzania wetu. Tuendelee kukaa kwa amani na utulivu na tuendelee kuwa mfano na nyota barani Afrika. AMEN

5 comments:

  1. AMEN! Muungano Idumu! Amani Tanzania Idumu! Utanzania Udumu!

    ReplyDelete
  2. CHEMI NILIKUWA NAUSHAURI WA BURE UNAJUA TUNA MABLOGGER WENGI SIO WOTE WANAJARIBU KUTAFUTA NYUZI ZAO SASA HII YAKO INA BORE MAANA WEWE UNACOPY ZOTEEEEEEE KUTOKA UKO TULIZOZIONA KWA MICHUZI HAKI JR UONI KAMA KUNA WATU WENGINE WALIOKO NYUMBANI PIA WANGEPENDA KUJIFUNZA MAMBO YA NJE OR ELSE BASI WEKA INTERNATIONAL NEWS LAKINI KWA MTINDO HUU SIELEWEI KWANINI UKO COPY AND PASTE WAKATI WATU TUMESHA SOMA UKO KWINGINE ALL IN ALL I ALWAYS ADMIRE YOU NA HII SIO SABABU YA MIMI KUTOACHA KUKUTEMBEA HAPA KWAKO
    MDAU WAKO WA NGUVU

    ReplyDelete
  3. Hakuna mtu anayejua huo udongo uliochangaywa siku hiyo uko wapi.

    ReplyDelete
  4. kweli old is gold,hivyo vitenge walivyovaa hao watu 2 waliobeba chungu ndo vimetoka sasa tena ni vizuri balaa.

    ReplyDelete
  5. Kwa nini Karume hakushiriki na kuchanganya udongo na raisi mwenzie? What is main advantage about this union? What's the benefit?

    ReplyDelete