Friday, May 23, 2008

Balali Aliagwa Jumanne!

Kutoka Ippmedia.com

Balali Aagwa

2008-05-23 22

Na Mwandishi Dar, Mashirika

Aliyekuwa Gavana wa Tanzania, Dokta Daud Balali aliyefariki Ijumaa iliyopita huko nchini Marekani, hatimaye ameagwa rasmi na ndugu na wapendwa wake, kabla ya mwili wake kupelekwa kwenye makazi yake mapya atakapopata pumziko la milele.

Taarifa za mtandao zilizothibitishwa na baadhi ya jamaa wa gavana huyo waishio Marekani zinadai kwamba, familia ya yake iliyo huko majuu na watu wa karibu, waliaga mwili wake Jumanne wiki hii. Kwa mujibu wa taarifa hizo, Jumanne ndiyo ilikuwa fursa pekee ya watu maalum waliopewa kibali kuona mwili wa Dk. Balali.

Imedaiwa kuwa leo, hakutakuwa na uwezekano wowote wa waombolezaji kuonyeshwa mwili wa marehemu. Kwa mujibu wa taarifa hizo, misa ya kumuombea marehemu ilitarajia kufanyika leo kuanzia saa 4:00 asubuhi (kwa saa za huko) katika kanisa la St. Stephen Martyr lilililo Pennsylvania Ave, NW Washingiton DC.

Ilielezwa kuwa mazishi yatafanyika katika makaburi ya ``Lango la Mbinguni\'\' yaliyopo eneo la Silver Spring, mjini Washington leo mchana. (kwa saa za kule). Taarifa zaidi zinadai kuwa shughuli hiyo nzima ni marufuku kwa wazamiaji ambao hawajaalikwa na kwamba ni maalum kwa ndugu, jamaa, na marafiki wa karibu.

Habari za mtandao zinasema bado haijajulikana kwa uhakika kama mwili wa marehemu utazikwa ardhini kama ilivyo desturi ya Kiafrika au utateketezwa kwa moto kwani makaburi hayo yanatoa huduma hiyo pia.

Kama ulikuwa ni wosia wake kuteketezwa, basi kwa kanuni za Kanisa Katoliki shughuli hiyo, itafanyika mara tu baada ya ibada. Kwa kanuni za Kanisa Katoliki mwili uliolazwa kwa njia ya kuteketezwa kwa moto mabaki yake (majivu) hawapewi familia, kusambazwa au kugawanywa katika mafungu madogo madogo na badala yake ni lazima viwekwe ardhini au kwenye sehemu maalum inayotumika kwa maziko ya namna hiyo.

Dk. Ballali ambaye amefariki akiwa amezungukwa na wingu kubwa la kashfa dhidi yake na dhidi ya taasisi aliyoingoza inasemakana aliacha wosia uliotaka atakapofariki basi azikwe Marekani.

Taarifa zaidi zimedai kuwa ibada ya mazishi inatarajiwa kuhudhuriwa na watu mbalimbali wakiongozwa na Balozi wa Tanzani nchini Marekani Bw. Ombeni Sefue, watumishi wa idara mbalimbali alizowahi kuzitumikia ikiwemo IMF, ndugu zake ambao waliwasili siku chache zilizopita, na baadhi ya Watanzania kadhaa waishio maeneo ya Washington DC.

Balali alizaliwa mwaka 1942 huko Iringa. Baada ya Elimu ya msingi na sekondari alipata shahada ya kwanza katika Uchumi mwaka 1965 toka Chuo Kikuu cha Howard nchini Marekani na kupata shahada ya pili toka Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Marekani miaka miwili baadaye.

Alijiunga na Benki Kuu ya Tanzania mwaka 1967 na kupanda ngazi taratibu hadi kufikia cheo cha Ukurugenzi wa Utafiti mwaka 1973. Baada ya hapo ndipo alipoanza kazi katika shirika la Fedha Duniani, IMF hadi mwaka 1997 alipoitwa nyumbani na Rais Mkapa na kuteuliwa kuwa mshauri wa Rais mambo ya Uchumi. Mwaka 1998 aliteuliwa na Rais kuwa Gavana mpya wa Benki Kuu

Ballali ameacha mke na familia.

SOURCE: Alasiri

3 comments:

  1. I thought walisema jamaa ataagwa leo yaani may 23.Yaani wanazidi kuongeza mazingaombwe.

    Pumbuj4

    ReplyDelete
  2. The guy will be buried/cremated, i don't know what to believe controversial till the day he goes to the grave/oven.

    Weird! Weird!.. and I thought why not sent back to Tanzania for funeral.

    and whats so secret about death, burial or cremated for that matter. The man is DEAD, dead and fallen, I have respect for the family, but they are creating an air of controversial and suspects ?

    Has he stashed a lot of millions in US ? The family worries that would be unearthed ?

    Why buried a GOVERNOR of a country, a man who imposed a sign on our currency, and not receiving the dignity of a burial on his own land ? and instead on a foreign land. I just don't get it.

    ReplyDelete
  3. Mimi nilipiga simu kwenye Devol Funeral Home kuulizia habari za Mzee Balali. Walisema kuwa alifariki nyumbani kwake huko Georgetown, D.C. Pia niliambiwa kuwa ndugu waliaga mwili wake jumanne na jana ingekuwa misa tu bila mwili.

    ReplyDelete