Saturday, May 10, 2008

Mchuano ni mkali Tuzo za Vinara!


ONE GAME PRESS RELEASE:

Na Mwandishi Wetu

Ikiwa ni wiki moja tangu jopo la majaji lianze kazi ya kuzipitia filamu zilizowasilishwa na watayarishaji wa filamu nchini ili kuwania tuzo za filamu za Vinara (Vinara Film Award), imeelezwa kuwa kumekuwa na mchuano mkali miongoni mwa filamu hizo.

Taarifa hiyo iliyotolewa na mratibu wa tuzo hizo zinazotolewa na One Game Promotion, Khadija Khalili (pichani), imetanabaisha kwamba mchuano huo umetokana na sehemu kubwa ya filamu hizo kuwa na kiwango cha juu cha ubora.

"Kazi ya kupitia filamu zilizowasilishwa inaendelea vizuri, hivyo tuna imani kuwa kazi itamalizika kwa wakati uliopangwa... Isitoshe, mchuano umekuwa mkali sana tofauti na tulivyodhani, filamu na wasanii vinakabana koo kwa viwango vya ubora," akasema.

Akaeleza, jopo hilo lilimtumia taarifa ya maendeleo ya kazi hiyo iliyoonesha mchuano kuwa mkali miongoni mwa filamu zilizowasilishwa kuwania tuzo hizo zitakazotolewa kwa mara ya kwanza nchini, huku kazi hiyo ikiendelea vizuri.

Aidha, majaji hao wanatarajiwa kumaliza kazi hiyo Mei 17 mwaka huu na kutoa fursa ya kutangazwa majina matano kwa tuzo zipatazo kumi na tisa zitakazowaniwa huku tuzo ya heshima ikipangwa kutolewa kwa msanii aliyetoa mchango mkubwa katika sanaa hiyo. ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Ndovu Special Malt ikishirikiana na Shirika la


Onesho la utolewaji wa tuzo hizo litakalofanyika Mei 30 mwaka huu, limedhaminiwa na KampuniUtangazaji la Taifa (TBC) na Global Publishers.


Wiki chache zilizopita, mratibu huyo alisema kuwa, zaidi ya filamu sabini za Kitanzania zimewasilishwa na watengenezaji wa filamu nchini kuwania tuzo hizo kwa mwaka wa 2007/08.

No comments:

Post a Comment