Tuesday, May 20, 2008

Michezo ya UMISSETA


Wadau, nani amewahi kushiriki michezo ya UMISSETA. Mimi niliwahi kushiriki kwenye mchezo wa Volleyball nikwa Tabora Girls. Sasa wanasema huenda michezo isifanyike mwaka huu!

****************************************************
UMISSETA sijui kama itafanyika -TMK

2008-05-20

By Abdul Mitumba, Temeke

Walimu wakuu wa Shule za Sekondari Manispaa ya Temeke, wameonyesha wasiwasi wao juu ya kukwama kwa michezo ya Shule za Sekondari nchini, UMISSETA, kutokana na tofauti ya mihula kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza na sita.

Tofauti hiyo inasababisha hata likizo za wanafunzi hao kutofautiana, hali inayotishia kutopatikana kwa wakati mmoja hasa ikizingatiwa michezo hiyo inapaswa kufanyika bila kuathiri masomo. Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Michezo na Utamaduni kwa Shule za Sekondari ya manispaa hiyo, Meja Martine Mkisi, ameonyesha hofu hiyo na kuonya endapo serikali isipolipa uzito suala hilo, UMISSETA itakwama.

``Kila mtu anayefuatilia masomo kwa wanafunzi wa sekondari anaelewa mihula kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi nne na wale wa kidato cha tano na sita inatofautiana, haitakuwa rahisi kwa wanafunzi hawa kuwaweka pamoja,`` amesema.

Amesema shule zilizomo katika manispaa hiyo zilipanga kuanza michuano ya UMISSETA wakati wa sherehe za Pasaka, lakini kutokana na ufinyu wa muda haikuwezekana. Mwenyekiti huyo ambaye pia ni mkuu wa Shule ya Sekondari Jitegemee inayomilikiwa na Jeshi la Kujenga Taifa, JKT, amesema endapo serikali imedhamiria kurejesha michuano hoyo ni lazima ifanye mabadiliko ya wakati ndipo itachezwa.

Novemba mwaka jana, Rais Kikwete alizindua rasmi michezo mashuleni kule mkoani Pwani na kuagiza utekelezaji wake uanze mwaka huu.

SOURCE: Alasiri

No comments:

Post a Comment