Tuesday, May 27, 2008

Watoto wadogo walazimishwa kufanya ngono ili wapate Chakula!


Jamani! Unaweza kulia baada ya kusikia habari hizi! Kumbe huko Haiti, Sudan, Ivory Coast na nchi zingine watoto wadogo wenye miaka sita wamelazimishwa kufanya ngono na kupiga picha za uchi kusudi wapate chakula kutoka kwa wafanyakazi wa vyama vinavyotoa misaada.
Wanasema kuwawalinda amani (Peacekeepers), na watoa misaada wa vikundi mbalimbali wamo kwenye orodha ya wanaonyanyasa watoto wadogo. Wanasema kuwa mara nyingi uhalifu kama huo unatokea kwenye makambi ya wakimbizi. Huduma mpaka kwa ngono! Habari zinasema wamelazimisha hata watoto wenye miaka sita kufanya ngono!
Huko Haiti binti wa miaka kumi na tano alisema kuwa alikuwa antembea na rafiki zake. Wakakutana na kundi la wafanyakazi wa chama kimoja cha misaada. Walitoa bolo zao kwenye suruali na kuwaambia wazinyonye ili wapate hela. Yule binti alikataa lakini rafiki zake walikubali na kupewa vihela na pipi.

Ubaya zaidi ni kuwa ingawa wenyeji wanajua inatokea nini, hawasemi kitu. Wanaogopa kuwa kama wakilalamika misaada itaacha kuja.

Lakini hebu mjiulize. Ni watu gani wanaofanya kazi kwenye hizi kundi? Mara nyingi ni watu waliokosa kazi kwao! Je, wanapimwa akili kabla ya kupewa kazi muhimu kama kwenda kugawa chakula au kulinda amani.

Lazima nisifu ripoti waliotoa Save the Children. Wamefanya kazi nzuri mno ya kuumbua hao washenzi!
Kwa habari zaidi someni:



2 comments:

  1. Dunia imeisha,umaskini ulaaniwe kwa jina la Yesu,yani jamani mtu anafanya jambo ambalo ni hatari kwa maisha for the sake of kuishi.
    yani umaskini ni chanzo cha matatizo mengi hapa duniani,tuupinge kwa kujibidisha kwa kufanya kazi na sio kubweteka na kusababisha maisha ya familia zetu kuwa ya unyanyasaji na magumu.
    Ms Bennett

    ReplyDelete
  2. Binadamu wamegeuka na kuwa sawa na wanyama.Mtoto wa miaka 6 wewe mwanaume unachokitaka kwake mbona laana tu.kwa kweli hii dunia inakoelekea panatisha ata shetani akiangalia yanayotendeka sometimes anatoa chozi kwani ni beyond of his/her expectation.Mungu atusaidie sana.
    zaka

    ReplyDelete