Monday, June 16, 2008

Seti la - The Surrogates huko Taunton, MA

Extras wakingojea kuitwa kwenye set. Kabla ya kwenda tulipanga foleni na kukaguliwa costume/nguo zetu na mwongoza sinema, Jonathan Mostow. Ilinikumbusha enzi za Tabora Girls, na JKT. Kama nywele nguo au viatu havikumfaa unatolewa na kupelekwa wardrobe/make-up. Hatukuruhusiwa kuvaa make-up. Kulikuwa na watu wenye makrimu za kufuta make-up kwenye uso za watu ukikamatwa umevaa. Pia ukionekana msafi, mtu alikuwa anapita na kutupaka make-up ya uchafu. Moja wa majengo kwenye set.

Moja wa kondoo waliotumika kwenye shoot.
Huyo nguruwe naye ni mwigizaji.


Wazazi wa watoto waliokuwa extra waliangalia shoot. Ona nyaya za umeme. Ilibidi watumie magenerata kwa vile hakuna umeme hapo.



Hao kuku nao ni waigizaji! ASPCA (Chama cha Kulind ahaki za wanyama) walikuwepo kuhakikisha usalama wa wanyama wote kwenye seti.




Siku hiyo kulikuwa na extras 300! Hapa tumemaliza siku na tunangojea check-out....kupata receipts zetu.



Wadau, kwanza samahani kwa kuchelewa kuposti hii habari ya seti. Nilikuwa na matatizo ya komputya.


Hii ni costume niliyovaa siku ya kwanza kwenye set ya The Surrogates. Nilikuwa mpita njia na nilimpita Bruce Willis kama mara kumi na tano. Alikuwa anatembea na kushangaa mji wetu wa Dreads. Siku ya pili sikupiga picha ndo ilikuwa scene ya kuchoma moto maiti.

Kibao kinatueleza sehemu ya kusubiri mpaka kuitwa kwenda kwenye seti. Kampuni ambayo inatengeneza hii sinema ni Walt Disney. Walikodi mabasi ya kutupeleka huko, na haikuwa mbali.

Seti enyewe ilikuwa Paul Devers School, ambayo zamani ilikuwa shule maalum kwa ajili ya watoto wenye magonjwa ya akili. Kuna majengo kibao. Ni kama ghost town, maana majengo yote ni abandoned. Walituweka nje kwenye mahema, kwa vile walisema majengo hayako salama kwa vile zina asbestos ndani.

9 comments:

  1. Umesema kampuni inayotengeneza sinema ni Walt Disney? Oh la laaa, Da Chemi hongera! Hongera sana!
    Asante kwa kutupa maendeleo ya kazi ya sinema hiyo.
    Pamoja daima!

    ReplyDelete
  2. wewe dada vipi badala ya kuwekea mambo ya jamii hunatuwekea mambo ya maisha yako nani anataka kujua mambo yako

    ReplyDelete
  3. Hongera Dada Chemi. Kuna siku tutasikia una role kubwa katika sinema hizo za Hollywood. Wala usivunjike moyo.

    ReplyDelete
  4. Hi Subi,

    Ndiyo ni sinema ya Walt Disney productions. Wana bajeti kali maana hizo special effects si hela ndogo.

    Ila ubaya wame-import actors wengi kutoka Los Angeles badala ya kutumia actors wa hapa New England. Actors wachache ambao nawafahamu wamepata nafasi ya ku-act kama principal (Yaani unaongea).

    ReplyDelete
  5. Umependeza kweli Chemi!!!!

    ReplyDelete
  6. Mdau wa 8:43, asante kwa comment, ila kwenye sinema hii hakuna kupendeza sisi Dreads tulitakiwa kuonekana wabaya wabaya.

    ReplyDelete
  7. hujui kuigiza fanya kazi ingine hiyo waachie akina kanumba tu wenye fani zao.upuzi

    ReplyDelete
  8. unajifagilia ktk blog yako.huna lolote.

    ReplyDelete
  9. Ndo maana sisi waswahili htauendelee! Wivu na chuki tukiona mtu kaendelea. Ni wabongo wangapi waliowahi kuwa katika sinema za Hollywood? Wachache sana. Da Chemi mi nakupongeza na hasa kwa ku-share info na kutupa moyo kuwa inawekezana.

    We anony wa 8:14am na 8:15am ni mtu moja na nikikupata nitakuchapa kiboko ushike adabu.

    ReplyDelete