Monday, June 09, 2008

Ugomvi kati ya Spike Lee na Clint Eastwood yazidi!

Wanajeshi wakipandisha bendera ya Marekani Iwo Jima, JapanSpike Lee na Clint Eastwood kwenye party mwaka juzi

Spike Lee ni muongoza sinema ma mcheza sinema maarufu wa Hollywood pia ni mmarekani mweusi. Clint Eastwood naye ni mcheza sinema na muongoza sinema maarufu wa Hollywood wa kizungu.

Clint Eastwood ametengeneza sinema mbili kuhusu vita kuu vya pili vya dunia (WWII) , 'Flags of Our Fathers' na 'Letters from Iwo Jimo'. Katika sinema hzo mbili, Eastwood hatumii waigazaji weusi, anatumia wazungu tu. Sasa Spike Lee amaechachamaa, anasema kuwa Eastwood hajatambua mchango wa wanajeshi weusi walioshiriki katika hiyo vita.

Eastwood anasema eti weusi hawakushiriki katika kupandisha bendera. Pia Eastwood alimwambia Spike Lee kupitia vyombo vya habari kuwa "afunge domo lake"

Spike Lee anadai kuwa weusi walikuwepo. Na sasa kaleta ushahidi. Mzee Thomas McPhatter (mweusi), ambaye alikuwa Sergeant wa jeshi wakati huo, anasema kuwa ni yeye ambaye aliwapa bomba ambayo wanajeshi wa kizungu walitumia kutundika bendera. Anasema ni hiyo bomba ambayo walitumia kuipandisha bendera hiyo.

Pia Spike Lee anasema kuwa atakusanya kikundi cha wanajeshi weusi waliokuwa huko Iwo Jima, na atamwomba Clint Eastwood awambie kuwa si kweli walishikiri katika hiyo vita. Makubwa!

Spike Lee ametenegeneza sinema, 'Miracle at St. Anna' ambayo inahusu mchango wa wanajeshi weusi huko Iwo Jima na ktika WWII.
Yaani historia ya Marekani. Wazungu ni wepesi sana kusahau au kutokutambua michango ya weusi katika kujenga nchi hii. Tuanzie utumwa! Weusi ndo walijenga hii nchi. Pia ni wavumbuzi, weusi wamevumbua taa za trafiki, plasma (damu ya transfusion), lifti (elevator), upasuaji wa moyo, subway na mambo mengine mengi. Lakini utajua kweli bila kuchambua na kutafuta ukweli?

Kwa habari zaidi someni:

1 comment:

  1. Spike Lee sema usiogope sema! Ubaguzi umezidi Marekani!

    ReplyDelete