Saturday, July 12, 2008

Bongoland II Review - Beda Msimbe

Nimeona hii review ya sinema, Bongoland II huko Lukwengule Entertainment. Imeandikwa na mwandishi wa habari maarufu Beda Msimbe. Aliiona leo kwenye Tamasha la filamu huko Zanzibar.

*********************************************************

Bongoland ll full uzushi full kupendeza

Ndio kwanza natoka kuangalia filamu iliyotengenezwa na watanzania ya Bongolandll katika ukumbi wa sinema wa wazi ndani ya Ngome Kongwe. Nyumba ilikuwa imeshiba, nataka kusema kwamba sinema hii ilipata mapokezimakubwa kwani ilishangiliwa na vile vijembe viliandaliwa kama vinavyostahili,maeneo ya manzese yalionyesha utofauti mkubwa wa maisha ndani ya Bongo ukilinganisha na mahali kazi zinapofanyika, dauni tauni.

Naam kama kuna wakati nilijisikia raha ni pale ambapo nilimuona dada Chemi akiwana waigizaji wazoefu sana nchini kama mama Mjata wakifanya vitu vyenye uhakika.Nilimaliza kuona filamu iliyojaa utata mkubwa wa maisha Bongoland ll nikiwa najisikia kuwapa Hi watanzania ambao wameonyesha tofauti kubwa ya maisha, akili,uwezo na kupozi maswali ambayo yanamgusa mtazamaji.

Ama hakika kazi ya Mtanzania huyu Josiah Kibira anayeishi huko Ughaibuni, Marekani ina maana kubwa na changamoto kwa waandazi wengine wa filamu nchini.Picha ya Bongoland 11 ambayo ni mwendelezo wa picha nyingine iliyoandaliwa naMtanzania huyo Bongoland ni ukakasi wa mapenzi, machungu, uzushi nauwongo,uzembe na kutojali maisha.

Ni filamu iliyoonyeshwa nchini kwa Mara ya kwanza ikiwa pia miongoni mwa filamuza kitanzania chache zilizofikishwa ZIFF kwa ajili ya kushindanishwa. Ikiwa inatumia dakika 109 inazungumzia umaskini kwa namna nyingi.

Umaskini uliomo ndani ya filamu hii ni wa mawazo, akili na swali kama kweli sisi ni mafukara linatawala kila mahali.hivi kama watu hawataki kazi watakuwaje mafukara?

Juma baada ya kurejea nchini akajikuta anatapeliwa, anadanganywa na pia anapata habari nyignine si nzuri, anapambana na bosi wake ambaye ana vibanda na vijumba basi mambo juu ya mambo.Naam ilikuwa filamu ya kuona kwani inasema wazi na ghasia zote sisi tu maskini wa mawazo.

No comments:

Post a Comment