Friday, July 11, 2008

Hakuna Sumu! - Skandali ya 'Uchawi' Bungeni


Sijiui kama wabunge watakaa wakiamini kuwa wako salama sasa. Mkemia mkuu wa serikali anasema kuwa ule unga uliyomwagwa bungeni haukuwa na sumu. Lakini kwa wanaojua uchawi, huo sumu hauwezi kuonekana kabisa kwa binadamu wa kawaida. Kwa hiyo bado tutasikia mbunge fulani atakaa sehemu fulani huko Bungeni na baada ya muda kidogo atasema kuwa anajiskia kachoka kichwa kinamwuma nk.. Hii siyo mwisho wa skandali ya uchawi/juju Bungeni.


***************************************************************************


Unga uliomwagwa Bungeni hauna lolote-Mkemia

2008-07-11

Na Jackson Kalindimya, Dodoma

Hakuna ushahidi wowote uliopatikana wa mtu kuona au picha za mitambo ya kamera maalum-CCTV unaothibitisha kumwagwa sumu ndani ya ukumbi wa Bunge kama ilivyodaiwa.

Taarifa iliyotolewa jana mjini hapa na Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma, Naibu Kamishia wa Polisi, Bw. Omari Mganga, ilisema kuwa baada ya sampuli kukusanywa na kutumwa kwa Wakala wa Mkemia Mkuu wa Serikali ambaye baada ya uchunguzi wake hakuweza kuona sumu yoyote ile inayotambulika.

``Kwa maana hiyo basi hakuna ushahidi wowote ule, uliopatiakana wa ama mtu kuona au poicha za mitambo ya CCTV au wa kisayansi unaothibitisha kufanyika vitendo kama hivyo`` ilisema taarifa hiyo.

Wakati wa kikao cha Mkutano wa kumi na mbili cha Bunge la Tanzania lilipoanza mkoani Dodoma, kulitokea minong\'ono au uvumi kuwa kuna Mbunge mmoja na Afisa Mmoja walionekana ndani ya Ukumbi wa Bunge wakizunguka kwenye viti vya waheshimiwa Wabunge huku wakinyunyizia vitu/unga uliohisiwa ulikuwa kwa ajili ya kudhuru binadamu au imani za kishirikina.

Kamanda Mganga alisema, katika taarifa yake kuwa, baada ya kuenea kwa uvumi hadi kwenye vyombo vya habari, uchunguzi ulifanyika kwa kukusanya ushahidi mbalimbali. ``Watu mbalimbali walihojiwa na hakuna hata mmoja aliyeweza kuthibitisha kuwa aliona watu wa aina hiyo wakifanya hayo yaliyokuwa yakiongelewa,`` ilifafanuliwa.

Alisema, uchunguzi pia ulifanywa na wataalamu wa kampuni ya SSTL GROUP wakisaidia na Maafisa wa Usalama wa Taifa na Polisi kwa kupitia picha zinazochukuliwa na mitambo ya CCTV ndani ya ukumbi wa Bunge, milango ya kuingilia na kuzunguka eneo lote la Bunge waliona kuwa hakuna kamera zilizozimwa tangu mwaka 2006 na katika kumbukumbu hizo za picha hakuna iliyuoonyesha mtu/watu wakifanya vitendo vilivyokuwa vinavumishwa.

Alisema pia sampuli mbalimbali zilichukuliwa kutoka katika ukumbi wa Bunge pamoja na vumbi lililopatikana kutoka ndani ya mashine ya kusafishia ndani ya ukumbi wa Bunge (hoover) ambao kama kungekuwa na kitu kilichokuwa kimenyunyuziwa ndani ya ukumbi huo tangu tarehe 9/6/2008 na kuendelea ingesaidia kwa kiwango kikubwa.

5 comments:

  1. Da Chemi hivi hujasikia na Zitto Kabwe kaugua baada ya kutoka Bungeni. Naye alikaa kiti chenye unga ambayo binadamu hawezi kuona.

    ReplyDelete
  2. Mganga kawapofua macho ndo maana hawakuona kitu! Mnacheza!

    ReplyDelete
  3. Ni kweli tunatakiwa awepo pia mpiga ndumba mkuu wa serekali kuweza kuona vitu kama hivi.

    ReplyDelete
  4. Anayeamini kuwa hakuna uchawi Bungeni ni punguani. Upo sana huko!

    ReplyDelete
  5. hiki kitu ni kweli kwanini wasimchague sheik Yahya kuwa mchawi mkuu wa serikali?wasijifanye serikali haitambui uchawi wakati uchawi hauonekani na mtu asiekuwa mtaalam wa hayo mambo.

    ReplyDelete