Wadau, hivi huyo binti ni huyo huyo Neema Mushi au ni mwingine? Shangazi yake anadai kuwa alimfia mikononi mwake. Neema mwenyewe anasema hakufa ila alikuwa anakaa Tanga.
***********************************************************
Kutoka ippmedia.com
Mtu adaiwa kufufuka
2008-07-28
Na Patrick Chambo, PST Hai
Mamia ya wananchi katika Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, wameshikwa na butwaa baada ya kumuona msichana aliyedaiwa kufariki dunia takriban miaka mitatu iliyopita akiranda randa mitaani.
Tukio hilo la aina yake, lilitokea katika kijiji cha Machame Mkuu, mkoani Kilimanjaro na msichana huyo anayedaiwa kufa na baadaye kukutwa akitembea mitaani ametajwa kuwa ni Neema Mushi, mkazi wa kijiji hicho.
Aidha, habari zilizopatikana kijijini hapo zilisema kuwa, binti huyo alisema kuwa alikuwa akiishi Tanga. Mchungaji Elimfoo Mushi wa Usharika wa Machame Mkuu, alisema ndiye aliyeendesha ibada ya kumuombea Neema ambaye mwili wake ulifikishwa kanisani hapo.
Akizungumza na PST, Neema alisema kuwa kweli hilo ni jina lake, lakini alikanusha kuwa alikufa na kuzikwa na badala yake alikuwa akiishi Tanga. Alisema eneo alilokuwa akiishi ni siri yake na kwamba akiwa huko alisikia kuwa alikufa na kuzikwa mwaka 2005. ``Mimi sijui kitu, najua nilikuwa naishi Tanga ?na wala siwaambii nilikokuwa naishi. Nimeshangaa narudi watu wanakimbia hadi nilipopelekwa polisi, wakaja ndugu zangu wakanitambua kuwa eti mimi nilikuwa marehemu,`` alisema.
Shangazi wa Neema, Bi. Liliani Mushi, alisema ndiye aliyemuuguza Neema hadi umauti unamfika na kusafirisha mwili wake hadi kijijini hapo na kuzikwa kwenye makaburi ya kanisa. ``Kweli mimi nimeokoka na sali Kanisa la Ephata, huyo mtoto alinifia mikononi huko Namanga nilikokuwa naishi naye nimeshangaa kuambiwa eti njoo umuone Neema, amekuja Machame kutoka Tanga, nilichoka, hakika huu ni muujiza wa Mungu watu wanasema kuwa eti ni msukule, mimi siamini, ninachojua alinifia tukamzika. Huyu hapa muulizeni wenyewe katoka wapi,`` alisema shangazi huyo.
Naye Mchungaji Mushi alisema, ``nasema nijuacho mimi ni kuwa huyu ndiye Neema ambaye msukule, mimi sijui,`` alisema. Polisi wilayani Hai, wamekiri kuchukua maelezo ya Neema, mwili wake uliletwa hapa kanisani na tukauzika makaburini, kwamba ni muujiza wa Mungu au wazazi, Mchungaji na ndugu wengine walioshiriki katika mazishi.
Hata hivyo, Kamanda wa Polisi wa mkoa Bw. Lucas Ng'ohoko, hakuweza kupatikana kuzungumzia sakata hilo. Aidha, ndugu na jamaa wa Neema wako kwenye harakati za kupata kibali cha polisi ili waweze kufukua kaburi hilo.
SOURCE: Nipashe
dada chemi.
ReplyDeleteNilishawahi kuhudhuria ibada katka kanisa fulani hapa Dar,nikakutana na issue kama hii ya Neema.Wao wanaita 'misukule' na katika kujieleza huyo mtu(alikuwa msichana) kabla na baada ya kuombewa alikuwa na maelezo tofauti.kwamba alikuwa akiishi manyara(kabla ya kuombewa) na alikuwa akiishi Mkuranga(baada ya kuombewa).Mchungaji akasema ivi:Huwa watu wanachukuliwa misukule or kimiujiza/kichawi na kule wanakotoka huwa wanakufa.Anyway,hii kisayansi haipo na tunaamini laba watu wanafanana tu
jamani naomba niwarekebishe kidogo, sio machame mkuu ni machame nkuu. mkuu ipo rombo na sio hai....hii habari ni ya kushangaza kwa kweli isitoshe imetokea katika kijiji nilicho zaliwa,ila ukifuatilia kwa makini habari za huyu binti utagundua kuwa kuna makosa yalifanyika hasa kwa upaende wa shangazi yake lilian
ReplyDelete