Tuesday, July 08, 2008

Rudini Zimbabwe - Uingereza!


Loh! Kumbe waingereza ni wakatili. Wameamuru wakimbizi 11,000 walioko Uingereza warudi Zimbabwe. Hali ilivyo mbaya huko Zimbabwe hao wakimbizi watakuwa salama kweli? Washenzi wa Mugabe watawauliza, "ehe mlikimbia nini?" halafu watanyanyaswa ile mbaya.

Nashangaa waingereza kwa uamuzi wao. Wanajua kabisa kuwa Zimbabwe kuna matatizo sana hasa kuhusuiana na haki za binadamu. Na wenyewe wamesemea serikaliya Mugaba si ya halali. Waingereza si wanadai wao ni watetezi wakuu wa haki za binadamu. Lakini hawashutuki kurudisha watu kwenye hali ambayo inahatarisha maisha yao.

Hali ya waZimbabwe wakimbizi huko Uingereza ni mbaya. Hawapati huduma ya serikali (welfare) na pia hawaruhusiwi kufanya kazi. Kutokana na hali hiyo wengine wanazagaa mitaani na kuwa ombaomba huko Uingereza.

Nauliza wangekuwa wakimbizi kutoka nchi ya kizungu kama Bosnia wangewarudisha kweli?

Kwa habari zaidi someni:




3 comments:

  1. This is not true jamani ni media tu hakuna wazimbabwe wanaozagaa mitaani most of my friends are from zimbabwe.wazimbabwe wameruhusiwa kukaa hapa mpaka machafuko ya hali ya hewa kwao yaishe.may be this is something to do na kuwa haribia jina waingereza anyway siwezi kujua mengi ni mtazamo wangu

    ReplyDelete
  2. Hivi Chemi wakati unafanya "kozi" yako ya uandishi wa habari, uliwahi kufundishwa suala zima la kuwa "objective"?
    Una bahati sana umezaliwa katika familia yenye mwamko wa elimu. Laiti kama ungezaliwa kwetu vingunguti wewe, kwa kiwango chako kidogo cha uelevu, ungekuwa mnywa kangala na mpika wanzuki tuu wewe.

    ReplyDelete
  3. Si elewi wabongo bwana. Habari zinasema kuwa hao wazimbabwe huko Uingereza wana hali mbaya kutokana na kunyimwa ruksa ya kufanya kazi. Wanasema wanaishi kwa misaada na wengine wanaishi sehemu za kufulia nguo. Hebu wachambe hao akina CNN, Fox News na AP kwa kupotosha ukweli basi.

    ReplyDelete