Wednesday, August 13, 2008
Walimu wa sinema 'stunts'
Hao ndo walifundisha akina Peter Omari, Shaffi Abdul na Charles Magali stunts zao kwenye sinema Bongoland II. Nilishangaa waigizaji Bongo walivyoniambia kuwa eti watu wanapigana kweli hadi kuumizana wakiwa kwenye shuti. Hizi sinema za Hollywood hakuna kuumizana ingawa utadhani mtu kapigwa kweli kweli.
Tulivyokuwa Bongo niliwashauri watu wajifunze hizo stunts maana walikuwa wanatoa mafunzo bure. Zaidi ya kipigana aliwaonyesha kidogo defensive driving (yaani kuendesha gari kwa stunt). Hapa Marekani watu wanalipa maelfu ya dola kujifunza.
Mwalimu Jason Hilton alitaka kufundisha wabongo wengi lakini hakuna aliyejitokeza zaidi ya waliokuwa kwenye sinema. Nilivyowauliza vijana fulani kama wanataka kujifunza waliuza eti watalipwa shilingi ngapi. Somo inatolewa bure halafu unataka ulipwe? Si ukachukua huo utalaamu uliyopata na uende ukatengeneza pesa? Au, ni wazo baya kwangu?
Nitaenda kuiona. Mdau Chi-Town.
ReplyDelete