Wadau, mnakumbuka majuzi niliposti habari ya binti Neema Mushi kufufuka? Alirudi kijijini na kusema hawajahi kuugua kwa muda mrefu na alikuwa anaishi Tanga na ndugu zake. Sasa ni ktendawili....nani alizikwa kwenye kaburi hilo? Na huyo aliyedai ni Neema Mushi hapo mwanzo ni nani?
**************************************************
Kutoka Lukwangule Blog:
MAMIA ya wakazi wa mkoa wa Kilimanjaro leo walifurika katika kijiji cha Nkuu Sinde wilayani Hai mkoani Kilimanjaro kushuhudia ufukaji wa kaburi ambalo miaka mitatu iliyopita lilizikwa binti mmoja ambaye amerejea kijijini kwake akiwa mzima.
Uwepo wa binti huyo akiwa mzima huku jamii ikifahamu kuwa amekufa kulifanya familia kutafuta njia ya kuliondoa kaburi hilo lenye jina la binti yao Neema Mushi ambaye ndiye waliamini wamemzika.
Wafukuaji walitoa jeneza na kukuta mabaki ya mwili wa binadamu ambaye hata hivyo hakuweza kutambulika kwa kuwa alipoletwa kuzikwa hapo na shangazi mtu aliaminika ni yeye Neema Mushi.
Swali linabaki huyu binti aliyezikwa ni nani?Awali ilidaiwa kuwa Neema ambae ni mkazi wa Machame wilayani humo baada ya wazazi wake wote kufariki aliondoka mkoani Kilimanjaro na kwenda kuishi Tanga kwa bibi yake mzaa mama pamoja na mama zake wadogo.
Katika hali ya kushangaza ilidaiwa kuwa mwaka 2004 shangazi yake Neema aliyefahamika kama Mama Peter ambaye ni mfanyabiashara Namanga alipewa taarifa na wenzake kuwa kuna mtoto aliyefika katika eneo lake la kazi na kudai ni ndugu yake na kuahidi atarudi siku nyingine baada ya kumkosa.
Ilielezwa kuwa Neema alirudi tena siku nyingine na kumkuta shangazi yake ambapo alijitambulisha kuwa ni mtoto wa marehemu kaka yake aliyeitwa Eliapenda Mushi na kwa kuwa shangazi yake hakumuona kwa muda mrefu alimpokea na aliamini hivyo na wakaishi nae.
Baada ya kuishi nae mwaka 2005 ilidaiwa binti huyo alianza kusumbuliwa na kifua ambapo shangazi huyo alimuuguza na ilipofika Septemba 5 mwaka 2005 alifariki dunia na kutokana na aneo alilokuwepo kushindwa kuuuhifadhi mwili huo aliwasiliana na ndugu zake waliopo Machame ambapo walifanikiwa kuuzika mwili huo Septemba 7 mwaka 2005.
Katika hali ya kushangaza na hisia za Neema zikiwa zimetoweka katika vichwa vya watu wakiwemo ndugu zake, binti huyo alirejea kijijini kwao Machame kwa bibi mzaa baba Julai 19 mwaka huu majira ya saa 11 jioni.
Kwa upande wake Neema alipohojiwa alidai kuwa hajawahi kufika Namanga na wala hajawahi wadogo. kuugua kwa muda mrefu na siku zote alikuwa akiishi Tanga kwa bibi yake na mama zake.
Habari na mdau wa kaskazini .
Hivi ndugu hawajuani?
ReplyDeleteKwa hiyo huyo binti alienda kamdanganya huyo shangazi kuwa ni fulani kakaa naye katunzwa. Kumbe ni mtu mwingine kabisaaa!
ACHENI HADITHI WADANGANYIKA...HII NI MURDER CASE YA WAZI WAZI....ILA KWA UMASIKINI WETU ITAISHIA HIVI HIVI NA WATU KUJIDAI KUENDELEA KUSHANGAA....MNASHANGAA NINI HAPA.....SHANGAZI ANA KESI YA KUJIBU NA KATU ASIJIDAI KUELEZA HADITHI ZA KUSADIKIKA HAPA....IDENTITY YA MTU ALIYEZIKWA HUYO SHANGAZI ANAIFAHAMU VIZURI NA KILE KILICHOPELEKEA UMAUTI WA HUYO MTU PIA SHANGAZI ANAFAHAMU.....SASA MUMESHAFUKUA...MMEKUTA MAITI...THEN WHAT NEXT?
ReplyDeleteKwa kweli shangazi ana maelezo ya kutoa. Haiwezekani kumpokea mtoto wa kaka yako, ukakaa naye, pasipo ndugu kujua, akaugua, pasipoo ndugu kujua, akafa na kwenda kuzikwa halafu kimyaaa. Pili huyo Neema ana vitu vya kujibu. Haiwezekani akakaa muda wote huo bila kufahamika alipo. Jamani sisi wabantu kuna mjomba, shangazi, baba mdogo, mama mdogo, wifi, shemeji, jirani na marafiki. Yaani wote hao wasifahamu chochote. HAPANA!!!!! TUNATAKA MAELEZO
ReplyDeleteShangazi abanwe vizuri atueleze mwili uliozikwa ni wa nani? Haiwezekani umpokee mtoto ukae naye bila kuwasiliana na ndugu yoyote. Pili pengine DNA itasaidia pia katika suala hili
ReplyDeleteHuyo marehemu huenda alikuwa mtoto haramu wa baba Neema naye kaitwa Neema. Ingekuwa vizuri kama tungejua ni nani aliyefariki na kuzikwa.
ReplyDelete