Saturday, September 13, 2008

UDA Bus 1974


Usafiri Dar es Salaam. Makao Makuu yalikuwa Kurasini. Na walikuwa na Ubungo Depot.
Walikuwa na Pass ya Mwezi kwa ajili ya wanafunzi na wakubwa. Mnakumbuka? Ni kabla ya Daladala kuingia.

Wadau mnakumbuka?

10 comments:

  1. Enzi hizo kulikuwa hakuna gari mengi. Mwisho wa mji ni Manzese na Ilala!

    ReplyDelete
  2. Hata kama kulikuwa hakuna magari mengi mbona si tunajua kwamba nchi inaendelea,watu wanaongezeka barabara zimepanuliwa/zimeongezwa Tatizo tetu ni kwamba hajui umuhimu wa public transport.Hayo mabasi ya UDA yalikuwa na ratiba ilikuwa rahisi mtu kupanga safari yako hasa wanafunzi ambao hawawezi kukodi taxi.Kama tumeweza kuleta mambo mengi kama Mabank ya nje kwanini tusiwaite wawekezaji waje washughulikie suala la public transport? Inaonekana serikali imeshindwa kabisa suala la usafiri.kuna nchi nyingi za dunia ya tatu zina magari mengi lakini wana public transport.

    ReplyDelete
  3. Hata kama kulikuwa hakuna magari mengi mbona si tunajua kwamba nchi inaendelea,watu wanaongezeka barabara zimepanuliwa/zimeongezwa Tatizo tetu ni kwamba hajui umuhimu wa public transport.Hayo mabasi ya UDA yalikuwa na ratiba ilikuwa rahisi mtu kupanga safari yako hasa wanafunzi ambao hawawezi kukodi taxi.Kama tumeweza kuleta mambo mengi kama Mabank ya nje kwanini tusiwaite wawekezaji waje washughulikie suala la public transport? Inaonekana serikali imeshindwa kabisa suala la usafiri.kuna nchi nyingi za dunia ya tatu zina magari mengi lakini wana public transport.

    ReplyDelete
  4. Huu ndio usafiri unaofaa kwa jiji la Dar... Sijui kitu gani kilisababisha kuanguka ama kufilisika kwa UDA....ama ndiko ufisadi ulipoanzia?

    ReplyDelete
  5. Yale mabasi ya UDA maikarus na yakle ya Kurasini yaliishia wapi? Si yaligeuzwa mradi wa mafisadi huko mikoani.

    Ikarus Kumbakumba! Twazikumbuka?

    ReplyDelete
  6. Nimefurahia picha hii ilivyo bomba, na zaidi ya yote kwamba ilikuwa ya rangi mwaka 1974...

    ReplyDelete
  7. ah...kudadadek. bongo imetoka mbali...duh

    ReplyDelete
  8. huo ndio ulikua usafiri wetu sisi wanafunzi wa shule za msingi mpakasecondary,namuunga mkono uliyesema kwa nini tusiwaite wawekezaje waje kufufua tena usafiri wa public,kuliko hizi daladala ambazo zimejaza wingi nakutokua na ratiba kamili,zsamani enzi tupo secondary mwanafunzi au mfanyakazi ulikua unajua ratiba ya mabasi yote kwa zile safari ulizokua unataka kwenda..ni aibu kuona serikali alina shirika lake la usafiri kama kamata na uda?duniani karibu kila nchi public transport zipo ,kasoro mafisadi bongo...

    ReplyDelete
  9. JAMANI SIO SIRI NADHANI KWA WANAOTUMIA USAFIRI WA DALADALA KWA SASA WANAWEZA SEMA HERI YA UDA WAKATI ULE MAANA NAKUMBUKA ANGALAU YALIKUWA NA RATIBA FULANI NA UTARATIBU JAPO HAUKUWA MZURI SANA LAKINI NI KASORO ZA KIBINADAMU ZINGEWEZA REKEBISHWA KWA AMA KUONDOA ALIYE SHINDWA KUONGOZA NA KUWEKA MWENYE MKAKATI BADALA YA KULINDANA.
    MATOKEO YAKE SASA DALADALA ZIMEKUWA NI KERO KULIKO KERO YENYEWE KA PALE POSTA WAWEZA KAA MASAA BILA KUONA GARI LA SAFARI YAKO AU PENGINE KULAZIMIKA KUKIMBIZANA NA KILA LINALOKUJA BILA KUWA NA UHAKIKA WAPI LITASIMAMA AU LA HATA MWENYEWE UCHOKE MBALI YA MATUSI YA NGUONI NA KEJELI ZA HAO MAKONDA NA MADERVA WAO. UKWELI NI HADHA SANA KUTUMIA DALADALA.

    ReplyDelete
  10. Cha ajabu ni kwamba usafiri wa umma nchi hii ulikuwa mzuri wakati nchi ilikuwa bado haijaendelea. Sasa hivi tuna Internet, simu za mkononi na ma-shopping mall, lakini hakuna public transport!

    ReplyDelete