Friday, November 28, 2008

Watu karibu 500 walikufa katika Ajali ya Moto mjini Boston mwaka 1942

Ukiwa unatembea maeneo ya Piedmont st. karibu na Arlington St. tafuta hii Plaque. Iko kwenye sidewalk usipoangalia vizuri unaweza kuikanyaga.
Watu wakingojea mortuary kwenda kutambua maiti za ndugu na marafiki zao


Klabu baada ya moto
Jitihada za kuokoa watu

Usiku wa Novemba 28, 1942, miaka 66 iliyopita watu 492 walikufa katika moto uliozuka katika klabu ya Cocoanut Grove. Watu walikuwa wanastarehe huko nakusikiliza muziki na kunywa vinywaji na kula chakula wakati motomkali ulizuka.

Habari zinasema kuwa kuna vijana huko waliokuwa wanataka kupiga mabusu katika giza. Waliondoa taa iliyokuwa juu yao. Kuna mfanyakazi aliyeamuriwa airudishe. Aliporudisha aliwasha kibiriti na kusababisha mapambo yaliyotengenezwa na karatasi kuwaka moto. Moto ulivyosmbaa mle watu walishindwa kutoka maaan mlango wa kutoka ulikuwa moja tu. Mwenye klbau alifunga milango kwa hofu kuwa watu watatoroka bila kulipa bili zao. Na kun watau waliopona huo ajali wanaosema kuwa wakati moto una waka kuna mfanyakazi alikuwa anadai watu walipe madeni yao.

Siku zingine ukipita eneo hiyo karibu na Arlington St., Boston utasikia kwa mbali milio ya watu.

Kutokana ma moto huo sheria za klabu mjini Boston zilibadilishwa. Mfano milango yote inafunguliwa kwenda nje, badala ya ndani.
Kwa habari zaidi someni:



No comments:

Post a Comment