Monday, December 22, 2008

Shujaa wa Taifa - Major Alex Nyirenda Afariki Dunia


Kutoka Michuzi Blog:

MAJOR ALEX GWEBE NYIRENDA, SHUJAA ALIYEPANDISHA MWENGE WA UHURU JUU YA KILELE CHA MLIMA KILIMANJARO SIKU YA MKESHA WA UHURU WA TANZANIA BARA, HATUNAYE TENA.

HABARI ZILIZOINGIA SASA HIVI TOKA KWA FAMILI YAKE ZINASEMA MAJOR NYIRENDA ALIFARIKI JANA SAA MOJA JIONI KATIKA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI ALIKOLAZWA. ALIKUWA NA UMRI WA MIAKA 72.

ALIKUWA AKISUMBULIWA NA MARADHI YA KANSA KWA MUDA MREFU NA AMESHAKWENDA MARA KADHAA NCHINI INDIA KWA MATIBABU.

KWA MUJIBU WA HABARI HIZO ZA KIFAMILIA, MAZISHI YATAFANYIKA DAR JUMATANO KATIKAMAKABURI YA KINONDONI. MSIBA UKO NYUMBANI KWA MAREHEMU MBEZI BEACH, FLETI ZA NATIONAL MILLING, KUCHEPUKA NJIA YA KWENDA AFRICANA, DAR.

GLOBU YA JAMII INATOA RAMBIRAMBI KWA FAMILIA, NDUGU, JAMAA NA RAFIKI WA MAJOR NYIRENDA AMBAYE ATAKUMBUKWA DAIMA KWA HISTORIA ALIYOIWEKA SIKU YA MKESHA WA KUPATA UHURU DESEMBA 9, 1961.

SOMA MAHOJIANO ALIYOFANYA NA BONGO CELEBRITY HIVI KARIBUNI KWA KUBOFYA HAPA:
************************************************************
Wadau,
Mnakumbuka ule wimbo wa halaiki, maneno sikumbuki vizuri hivyo naomba mnisahishe:
Sisi tumeuwasha Mwenge
na kuiweka Mlima Kilimanjaro
Kuwasha Mwenge
Kuwasha Mwenge

Na kuiweka Kilimanjaro

3 comments:

  1. Buriani mzee wetu, tutakukumbuka daima ingawa katika historia ya Tanzania jina lako lilifichwa sana. Sijui kwa nini?

    Tiwonane kuchanya, chiwuta akusunge chomene mdala witu.

    UK

    ReplyDelete
  2. One cannot change history. Alex Nyirenda ndie aliye pandisha bendera na mwenge katika kilele cha mlima kilimanjaro siku ya uhuru. Je utaibadilishaje kama hamtaki ukweli ujulikane...?

    ReplyDelete