Tuesday, February 17, 2009

Wizi Ocean Road Hospital

Wadau, mnaweza kuamini kuwa vifaa hivi vya chemotherapy vimeibiwa kutoka Ocean Road Hospital. Ocean Road ni hospitali kuu Bongo ya kutibu ugonjwa wa saratani (cancer). Yaani wametoa huo mtambo mkubwa bila mtu yeyote kuona kweli? Walinzi walikuwa wapi? Wafanyakazi walikuwa wapi? Najua pale kuna manesi na madaktari 24/7!
Yaani huo wizi lazima ilikuwa ni inside job. Lazima kulikuwa na watu waliojua kuitoa huko bila kuiharibu. Hivi wanausalama wanafanya nini siku hizi huko Bongo?
***********************************************************************
Picha na Maelezo ya chini kutoka Michuzi Blog:
Hii ndo aina ya mashine zilizoibwa yapata wiki mbili zilizopita pale ORCI zaitwa Control Console, zimenunuliwa tena mpya kwa gharama ya Dola za US 22,000/- na hivyo wagonjwa wameanza tena leo kupata huduma baada ya kusimama kwa muda wote huo.

Mdau Bernard Rwebangira anashindwa kuelewa mashine kubwa na nyeti kama hii iliiniwaibiwaje? ungana naye kujadili hilo kwa kubofya hapa

4 comments:

  1. Lakini madkatari na manesi walihusika. Wanaenda kufungua hospitali yao na huo mtambo!

    ReplyDelete
  2. Dawa ni kutembeza bakora kwa wafanyakazi wote mpaka waseme nani kaiba. Hivyo vitu si vinaandikishwa na wizara ya afya? Wizara ya afya inajua nani anayo!

    ReplyDelete
  3. Na kweli huyo jamaa anaweza kuwa mwizi! Bongo BWANA!

    ReplyDelete
  4. Ngai! huo ni uwizi wa hali ya juu ambao lazima ulihusishwa na watu kadhaa wa kila kiwango cha hospitali hiyo. Nina matumaini kwamba hao waliohusika wanasakwa na serikali..


    mbu

    ReplyDelete