Thursday, April 02, 2009

Maisha Music Newsletter

Albamu ya Ashimba “NURU NYIKANI” ipo sokoni

Albamu mpya ya Ashimba “NURU NYIKANI” sasa hivi inapatikana katika maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam, Bagamoyo na Zanzibar. Albamu hii ni yenye vionjo vya pekee na inajumuisha nyimbo mbalimbali zenye usikivu wa kuvutia. Kazi hii imetayarishwa na Jakob Poll ambaye ni mtayarishaji aliyebobea katika fani kutoka Denmark, na ni mseto wa ladha asili na vionjo vya kielektoniki..
Muda si mrefu albamu hii itapatikana katika mitandao mbalimbali pamoja na maduka ya muziki Ulaya……. Tutawajulisha muda ukiwadia!
Kama aumfahamu Asimba basi unaweza kusikiliza kazi zake na taarifa zaidi katika www.maishamusic.com na www.myspace.com/ashimba.

“NURU NYIKANI” inapatikana kwa mauzo katika maeneo yafuatayo:
Maduka ya vitabu ya Novel Idea (mtaa wa Ohio (Steers), Slipway, Shopers Plaza na Mji Mkongwe Zanzibar.
Mawazo Gallery ( Jengo la YMCA)
Dar Alive (zamani Malaika, barabara ya zamani ya bagamoyo)
Maduka ya One Way (Slipway, Sothern Sun Hotel na mji Mkongwe Zanzibar)
Afrikabisa (Bagamoyo)


ASHIMBA Ndani ya 41 Boom Shack

Ashimba atafanya onyesho akiwa na bendi kamili siku ya Jumamosi tarehe 4 Aprili 2009 katika ukumbi waa Alliance Francaise. Hili ni onyesho la kwanza akiwa na bendi tangu alipofanya lile la uzinduzi wa albamu yake uliofana.
Usikose nafasi hii ya kumwona na kumsikiliza Ashimba.
Onyesho hili litapigwa picha (video) kwa ajili ya maandalizi ya DVD ya matangazo, jiandae kwa maajabu mbalimbali siku hiyo…

Onyesho hili limeandaliwa na 41 Records kwa ushirikiano na Maisha Music. Huu pia utakuwa ni mwanzo wa mwendelezo wa maonyesho yya yatakayojulikana kama “41 Boom Shack – Mobile Sound System” ambayo yatakuwa yakifanyika kila Jumamosi katika ukumbi wa Alliance Francaise. Burudani itakuwa ni ya muziki wa Reggae, Dancehall na Hip Hop/RnB kutoka kwa wasanii na nyimbo ambazo ni ngeni masikioni na machoni mwa wengi katika klabu za hapa Dar es Salaam.
Kutakuwa na burudani kutoka kwa ma-DJ kama vile DJ Niki wa East African Radio ambaye atakuwa pia ni mwenyeji wa ma-DJ na wasanii mbalimbali waalikwa.

Nini: 41 Boom Shack – Mobile Sound System
Nani: Ashimba na DJ Niki
Lini: Jumamosi tarehe 4 Aprili, kuanzia saa 2 Usiku mpaka usiku mkubwa
Wapi: Alliance Francaise
Kiingilio: Shilingi 5000/ tu

Ashimba kwenda kufanya maonyesho Scandinavia

Kwa mara ya kwanza Ashimba atafanya maonyesho mbalimbali katika nchi za Scandinavia mwezi wa Mei na Juni 2009. Ingawa ni mara ya kwanza kwake kutembelea nchi hizi zenye hali ya hewa ya baridi kali kwa kipindi kirefu, ziara hii itafanyika katika kipindi kizuri zaidi kwa mwaka!!! Atafanya maonyesho katika kanivo ya Copenhagen na sehemu mbalimbali za nchi za Scandinavia. Ratiba kamili ya ziara hii itatolewa baada ya muda si mrefu.


www.maishamusic.com

Hatimaye ile tovuti yetu ipo hewani www.maishamusic.com inapatikana kwenye mtandao. Shukrani za pekee kwa wajenzi Ravn na Kristianna Matras Nordoy kwa kazi kubwa ya kuiandaa. Inapendeza!! Ingawa kwa sasa bado haijakamilika kabisa lakini taratibu itakuwaa tayari. Taarifa zaidi kwa waandishi wa habari, gulio, muziki na picha zinapatikana. Vile vile kuna kitabu cha wageni, hivyo tafadhali wasiliana nasi kama kuna maoni au maswali.. tunakutegemea kwa ajili ya kutusaidia katika ujenzi na maendeleo ya taasisi yetu katika info@maishamusic.com. Kumbuka kuwa tumabadilisha anuani yetu ya myspace na sasa inajulikana kama www.myspace.com/maishamusictz.


Kwame Mchauru – Sura mpya ndani ya Maisha Music

Maisha Musici imeungana na meneja wa mradi Kwame Mchauru. Sasa hivi Kwame anafanya kazi kubwa ya kuratibu na kuitangaza albamu mpya ya Ashimba “Nuru Nyikani”. Kwame amewahi kufanya kazi kama mkurugenzi msaidzi wa Busara Promotions ya Zanzibar na kwa sasa anafanya kazi kwa mkataba na British Council kama mratibu wa tamasha la WaPi Zanzibar na pia ni meneja wa muda wa mradi wa wasanii wa sanaa za mikono unaofadhiliwa na ubalozi wa Denmark. Kwame pia ni meneja wa makundi ya Jagwa Music (Mchiriku) na Splendid Theatre zote kutoka Dar es Salaam. Ni matarajio yetu kuwa Kwame atakuwa nasi kwa muda mrefu kwani ni mmoja wa wachache wanaofaa kwa kazi hii. Karibu sana…


Kwa ufupi

Toleo Jipya

Maisha Music ipo katika hatua za mwisho wa maandalizi ya kurekodi mseto wa nyimbo kutoka kwa wasanii mbalimbali utakaojulikana kama Maisha Lounge Vol. 1. Mchanganyiko huu utajumuisha nyimbo za taratibu za kitanzania na vionjo vya kielektroniki.
Albamu hii inatarajiwa kuzinduliwa mwezi wa Septemba 2009.

Likizo ya uzazi
Jakob Poll atasafiri kuelekea nchini Denmark kuanzia tarehe 7 aprili kwa ajili ya kuwa na mama watoto wake ambaye anatarajia kujifungua “wa pili” mwanzoni mwa mwezi wa Agosti. Kwame Mchauru ataratibu shughuli zote za Maisha Music kwa hapa Tanzania na Jakob atafanya kazi zinazohusu maslahi ya Ulaya akiwa Denmark. Jakob ataratibu uzinduzi na usambazaji wa “Nuru Nyikani” kwa nchi za Ulaya.

Video
Maisha Music kwa sasa inafanya kazi na kampuni ya Reel 2 Reel katika upigaji picha na utengenezaji wa video ya kwanza ya Ashimba. Wimbo uliotumika katika kazi hii ni kutoka katika albamu ya “Nuru Nyikani na unajulikana kama “Yaya” na imepigwa picha katika maeneo mbalimbali ya Mwananyamala. Shukrani kwa wale wote walioshiriki katika kuifanikisha.

Maisha Music
info@maishamusic.com
www.maishamusic.com
www.myspace.com/maishamusictz

No comments:

Post a Comment