Wadau, nilivyokuwa mdogo nakumbuka wazee wakisema kuwa Mjerumani alikuwa mkatili, bora mwingereza alivyoingia Tanganyika. Nilisikia kuwa hao wajerumani walikusanya wazee wengi na walemavu karibu na Bagamoyo na walikuwa na mpango wa kuwaua. Kumbe halocaust (Mauaji ya wayeheudi kwa mkono wa mjerumani) haikutaokea miaka ya 40 tu! Ni mila yao! Leo nimeona hizi picha za ukatili.
Ukiwa hujafanya kazi ya kutosha unachapwa! Ukizidi kuwa mvivu, unakatwa mikono!
Samahani da Chemi, hizi picha si za wajerumani, ni za wabelgiji na ukatiri was DRC... picha zima kwenye kitabu cha "king leopolds ghosts"
ReplyDeleteDuh!, hivi huwa wanajisikiaje hii leo kwa vitendo walivyotufanyia?.
ReplyDeleteNi unyama wa hali ya juu, unadhani unyama huu umekwisha?, mi nasema hapana. bado wanatuchapa bakora, sio za matakoni bali za kifikra.
Wanajenga mazingira tujione hatuwezi, maskini na wanyonge.
Ukatili wao nadhani haujaisha kwani sidhani kama ni wadau wa kweli ya ukombozi wa kiuchumi wa muafrika.
Hata kam ni wabelgiji hao waafrika wanaona sawa kushika mkiono ya wenzao!
ReplyDeletedada chemi yaliyopiata yamepita tu ndg yangu ile chuki hamna watu tushasahau na hakuna kisasi nao ndo maana ndg zetu wengi wanaolewa na wajerumani na wengine wanaoa huko. maisha yanakwenda tu kama kawa.
ReplyDelete