Monday, April 06, 2009

The No. 1 Ladies Detective Agency

(kutoka kushoto - Anika Noni Rose, Jill Scott, Lucian Msamati)

Wadau, mkipata nafasi hebu tazama TV show, The No. 1 Ladies Detective Agency. Kama mnakumbuka niliwadokeza mwaka jana kuwa walikuwa wanapiga sinema huko Bostwana. Hiyo sinema imekuwa 'pilot' (Show ya kwanza) na sasa HBO wameagiza iwe series. Hivyo kila wiki tutafaidi show kutoka Botswana. Kwa sasa inaonyeshwa kwenye stesheni za HBO na BBC.
Stelingi wa The No. 1 Ladies Detective Agency ni mwimbaji Jill Scott ambaye ni MMarekani. Anayoigiza utadhani ni MBotswana. Stelingi mwingine ni Anika Noni Rose ambaye utamkumbuka alikuwa kwenye sinema Dreamgirls.

Stelingi mwingine ni Lucian Msamati, ambaye ana asili ya Tanzania ingawa ni MZimbabwe. Wazazi wake ni waTanzania. Alizaliwa Uingereza na alipelekwa Zimbabwe akiwa mdogo.
Nimefurahi kuona jinsi watu wanavyofurahi The No. Ladies Dectective Agency. Wazungu wanaipenda kweli na sasa tayari wameanza kusema kuwa huenda Jill Scott atapata Emmy Award! Hayo ni makubwa!
Botswana wanasema kuwa utalii kwenda Botswana unaongezeka na wanaishukuru hiyo show maana inaonyesha Botswana ilivyo ukweli. Serikali ya Botswana iliwaunga mkono hao watengeneza show na imekuwa na mafanikio makubwa. Kuna aerial shots (scenes zilizopigwa kutoka kwenye ndege) safi sana. Watu wanapata ajira kama wafanyakazi wa filamu, na pesa zinaingia kwenye kukodi mahoteli, chakula, usafiri na megineo.

Je, Tanzania tuko tayari kuwa na show ambayo inapigwa huko? Je, serikali itawaunga mkono watengeneza TV show wakiomba kupiga nchini Tanzania?
Na kwa wasiojua miaka ya 60, kulikuwa na TV show, 'Daktari' ambayo ilikuwa inapigwa Kenya.
Ilihusu daktari wa wanyama ambaye alikuwa mzungu. Stelingi wake alikuwa marehemu Marshall Thompson.

9 comments:

  1. Asante sana da Chemi kwa taarifa nzuri ya hawa The no 1 Ladies detective agency. Nimesoma vitabu vyao vyoote toka mwanzoni mwa miaka ya 2000 walipotoa Tears of the Giraffe. Napenda sana vitabu vyao.
    BBc wanaonyesha hiyo kitu muda gani kwa saa za Scandnavia? Niko tayari nisilale nione hiyo kitu.

    ReplyDelete
  2. Nimeiona jana usiku its so nice Jill utadhani ni mtswana kabisa I cant wait for next sunday to come. Inaonyesha pia culture za waafrika HBO wanaonyesha saa mbili au tatu kama sikosei

    ReplyDelete
  3. Bongo, watu watakanyagana kupata chochote! Ndoto ya Ndaria hiyo Da Chemi!

    ReplyDelete
  4. Safi sana, BBC wanaonyesha kuanzia saa 9.00pm kila j'pili,kweli hawa wadada wamejitahidi sana huwezi kujua kama sio wa Botswana ni mpaka mtu akwambie,mimi nampenda zaidi Anika noni Rose, anavituko sana.

    ReplyDelete
  5. Chemi, hii series nami naifuatilia sana sijawahi kuikosa! Pia ile pilot ya mwaka jana niliiona na kununua DVD yake (£13.99 in October) ila sasa imeshuka bei kidogo. Na hii series mopya itatoka kwenye DVD June 16, 2009. Bei ya pre-order ni £16.99 (series ya 1 yenye michezo 6).
    Uingereza BBC wameshaonyesha sehemu 4 bado 2 kukamilisha series ya kwanza!

    Samahani Chemi; mimi nakufananisha sana na Jill Scott (Mma Ramotswe), yaani mnafanana sana utadhani mapacha!! Na birthday zenu zimekaribiana pia!

    Nampenda pia Anika Rose Noni (Mma Makutsi - siku hizi kapandishwa cheo ni 'assistant detective' akifanya na u-sekretari wake pia!

    BK nae ni muigizaji mzuri

    ReplyDelete
  6. Chemi, hii series nami naifuatilia sana sijawahi kuikosa! Pia ile pilot ya mwaka jana niliiona na kununua DVD yake (£13.99 in October) ila sasa imeshuka bei kidogo. Na hii series mopya itatoka kwenye DVD June 16, 2009. Bei ya pre-order ni £16.99 (series ya 1 yenye michezo 6).
    Uingereza BBC wameshaonyesha sehemu 4 bado 2 kukamilisha series ya kwanza!

    Samahani Chemi; mimi nakufananisha sana na Jill Scott (Mma Ramotswe), yaani mnafanana sana utadhani mapacha!! Na birthday zenu zimekaribiana pia!

    Nampenda pia Anika Rose Noni (Mma Makutsi - siku hizi kapandishwa cheo ni 'assistant detective' akifanya na u-sekretari wake pia!

    BK nae ni muigizaji mzuri

    ReplyDelete
  7. Kwa wapenzi wa The No.1 ...:

    Film ya 'The No.1 Ladies Detective Agency' inahusu kitabu kilichoandikwa na Alexander McCall Smith chenye jina hilo hilo.

    Kitabu hicho pia kinapatikana madukani kwa bei ya £6.99 (hii ni bei ya mwaka jana April).
    (Sijui kule Marekani au kwingineko kinauzwa bei gani au kinapatikanaje!)

    Kwa UK mchezo unaonyeshwa kupitia BBC One. Kama hujaona michezo minne iliyopita - unaweza kuiona yote kupitia 'BBC i-player' (mtandao)

    ReplyDelete
  8. Hii kitu bomba lakini nakiri ninaudhaifu na kazi na yeye tu Jill Scott

    ReplyDelete
  9. HABARI ZA KAZI DA CHMPONDA, MIMI NASOMA HII BLOG YAKO KARIBU KILA SIKU NA NAIPENDA KWA SABABU UNATUONYESHA AU UNATUFUNGUA MACHO WATU WENGI KWA MAMBO KIBAO UNAYOYATOA KILA SIKU.DUKU DUKU LANGU NI KUHUSU HUYU KIJANA ANAJIITA MR.NICE KITENDO ANACHOKIFANYA NI CHA KINYAMA KWANZA ALIANZA KWA KUSEMA YEYE AJALELEWA NA BABA YAKE, HALAFU ALIPOKUJA KUHOJIWA KWENYE STATION MOJA YA TV BONGO ANASEMA HAJUI MTOTO WAKE YUPO WAPI, SASA KAMA YEYE HAJALELEWA NA BABA YAKE ANA HAKI YA KUMFANYIA MTOTO WAKE HIVYO .

    ReplyDelete